Wala hamna cha maana , zaidi wanakuvuta tu sio muda unaangua kilio..
Wao wanasema wanashirikiana na wafanya biashara wakubwa na taasisi mbalimbali ulimwengu ili kukuza maudhui yao hivyo wao wanakushirikisha video mbali mbali wewe uzi like na ku subscribe kila video wanayo kupa link yake kupitia mtandao wa telegram, ambayo wanasema kila link ya video wanayokutumia ni jukumu au kwa lugha yao task, sasa kila task inabidi ufanyie kazi , task moja wapo ni ya kutuma kiasi cha fedha kiwango cha kuanzia ni laki , huo laki watalipa namba ya kutuma, ilishatuma watalipa link ya mtu wa kukuongoza, huyo mtu atakupa link ya mtandao wa jumia huko utajisajili na kununua vifaa kama vile jagi, redio , tv ama chochote kwa thamani ya hip laki na kuendelea kisha baada ya kununua hio bidhaa atakupa code namba unarudi kwa mtu wako wa awali na kufanya mchakato wa kurudisha hela yako na asilimia 30 ya faida.
Kule kwenye mchakato wa kununua bidhaa ukikosea hata kidogo hela yako imeenda.