Wewe uliyetoa hiyo thread soma hiyo Makala ndio uandike upupu wako: Genius.[/I]
Neno genius ni mapokeo ya lugha ya kilatini ya neno gigno yaani kuumba au kutengeneza. Kwamba mtu yeyote mwenye kipaji anaweza kufanya jambo ambalo mtu mwingine hawezi kuliwazia wakati huo.
Kuna ma-genius kwenye fani mbalimbali duniani. Albert Einstein kwenye fizikia, Pablo Picasso kwenye uchoraji, Bill Gates kwenye kompyuta na Pele kwenye soka. Wote hao wanafanana kwa vipaji lakini kwenye maeneo tofauti.
Katika kitabu cha Outliers cha Malcom Gladwell, amenukuu utafiti uliofanywa na Anders Ericsson uliobainisha kuwa inachukua takribani saa 10,000 kwa mtu kujifunza hadi kukifahamu kitu. Lakini, utakuta wenzetu ma-genius wamezaliwa tu na vitu hivyo.
Na ndiyo maana kama utawauliza imekuaje waliweza kufanya kitu fulani, wao watakuuliza kwanini umeshindwa kuona kitu kama hicho mapema. Yaani wanajua tu na hawana maelezo ya kwa nini walifanya walichofanya.
Na hawa wana tabia ambazo ni tofauti na tabia zetu sisi watu wa kawaida. Romario alikuwa hataki kufanya mazoezi, George Best alitaka aruhusiwe walau kupiga glasi mbili za pombe kabla hajaingia uwanjani, Rivaldo hakutaka kushea chumba na mtu na Effenberg alikuwa mkorifi balaa.
Kila mtu na kilema chake. Haruna, kwa namna ninavyomfahamu mimi, anataka watu wamwache acheze mpira. Na hata kama hajamwambia yeyote, najua hakufurahishwa na hatua ya yeye kupimwa katika timu ya vijana.
Atapimwaje na vijana ambao kila siku wanaota kuwa na kipaji kama chake? Hivi Boban afanye nini ili tukubali kwamba ana kipaji cha kipekee kwa viwango vya hapa kwetu kwa sasa?
Kama tulivyo sote, Boban naye ana madhaifu yake. Kocha au timu yoyote inayomtaka inatakiwa kujua namna bora ya kumtumia. Lakini si kutaka afanye kila kitu kama sote tunavyotaka. Yeye si kama sisi!
Hatuwezi kumchukia Boban eti kwa sababu alipata timu na kuiacha huko Sweden. Yeye ni mtu mzima na sote tunaishi kwa maamuzi tunayoyafanya katika maisha yetu. Kama alikosea au hakukosea, na kimsingi sote tunakosea, wakati utatuambia.
Vinginevyo, kuna kitu kimoja ambacho Watanzania tunaweza kufanya kwa sasa. TUMWACHE HARUNA MOSHI SHAABANI (BOBAN) acheze mpira.
Makala hii ni mawazo binafsi ya mwandishi na si msimamo wa klabu ya soka ya Simba anakofanyia kazi.
0718 81 48 75]The Official Website of Simba Sports Club