Haruna Moshi 'Boban' hajakua bado

Haruna Moshi 'Boban' hajakua bado

Hivi diof wa senegal na Boban nani hana ni dhamu kuna wachezaji wenye nidhamu 0 lakini wana tumikia mataifa yao tatizo kwetu hatuna watu wa kushugulika na watu kama Boban....mwangalie Balloteli,Gaza nk....

To hell. Watanzania Hatuhitaji kutumikiwa na mateja.
 
Jamani ehee hivi lakini huyu Haruna Moshi Boban ana miaka chini ya 23 kweli? kama kweli ana miaka chini ya 23 na amekataa kuchezea U23 team basi anastahili adhabu kali kweli kweli
lakini kama umri umezidi miaka 23 alafu expart kocha anamshawishi ku foji umri ili acheze U23 team basi kocha huyu pamoja na benchi lake lotee la ufundi wanapaswaa kufukuzwaa kwa kuchapwaa bakoraa au mikia taaa isiyopungua 800 hivi kwa maaana likibumbulukaa ni nchi ndio itakayo aibikaa nani anakumbuka sakata la david mwatobe wa serengeti boys?

Ivi kama mtu hujui kiasi hiki ni lazima kuchangia humu?? Pole.
 
Kama Kocha alikuwa na haja ya kumwita kikosi cha kwanza angemuita moja kwa moja, si lazima mpaka acheze under 23. Bombani kacheza game nyingi tu kwenye kombe la Kagame, sasa anachotaka huyu kocha ni nini zaidi? Ku - justfy nini? Bombani ni senior player wa nchi hii na lazima aheshimiwe.

Cha msingi kama hataki kumwita aache, si lazima kila mchezaji achezee nchi yake - huyu kocha naye ameanza kuwa na matatizo kama maximo.
 
Kuna kocha wa timu ya ligi kuu ya uingereza alisha wahi kushangilia goli na timu pinzani baada ya timu yake kufungwa..hivi alifukuzwa...

Wewe kwa mtazamo wako unaona ni sahihi kufanya hivyo? Kama jibu ndio itabidi tukunyang'anye hiyo bendera manake wenye nayo si wavivu kufikiri.
 
Kama Kocha alikuwa na haja ya kumwita kikosi cha kwanza angemuita moja kwa moja, si lazima mpaka acheze under 23. Bombani kacheza game nyingi tu kwenye kombe la Kagame, sasa anachotaka huyu kocha ni nini zaidi? Ku - justfy nini? Bombani ni senior player wa nchi hii na lazima aheshimiwe.

Cha msingi kama hataki kumwita aache, si lazima kila mchezaji achezee nchi yake - huyu kocha naye ameanza kuwa na matatizo kama maximo.

Wewe TFF walipotoa nafasi za ukocha hukuomba sasa unataka kumfundisha kocha kazi yake? Wabongo bana! Wana majibu ya kila kitu!
 
Kufuatia mlolongo wa matukia ya mwanandinga Haruna Moshi Boban kukataa kuichezea timu ya taifa U-23, dhidi ya Ushelisheli hivi karibuni kule Arusha imenikumbusha rekodi yake mbovu ya nidhamu.Si kule Simba tu toka nyakati hizo ila pia aliwahi kuingia na kopo la bia U/Taifa,kukacha mazoezi na hivi majuzi baada ya fainali ya Kagame Cup chap chap alibadili nguo akavaa jeans na T shirt na open shoes, baada ya kukabidhiwa medali akaivua pale pale mbele ya mgeni rasmi.Hii pia imenikubusha ni kwa nini Maximo aliwahi kusema hana nidhamu hata kidogo na humpiga chini jumla kuichazea Stars.

Huyu level yake ni kucheza ndondo au mchangani sijui kwa nini hawa jamaa tulio wapakata juzi wanamng'ang'ania mchezaji ambae hana nidhamu kiasi hiki
 
To hell. Watanzania Hatuhitaji kutumikiwa na mateja.
Ni mtanzania mwezetu na huna haki ya kuamru asilitumikie taifa lake....niteja kwa sababu za baba yako fisadi anae nunua madawa na kutu halibia vijana wetu...
 
Jamani ehee hivi lakini huyu Haruna Moshi Boban ana miaka chini ya 23 kweli? kama kweli ana miaka chini ya 23 na amekataa kuchezea U23 team basi anastahili adhabu kali kweli kweli
lakini kama umri umezidi miaka 23 alafu expart kocha anamshawishi ku foji umri ili acheze U23 team basi kocha huyu pamoja na benchi lake lotee la ufundi wanapaswaa kufukuzwaa kwa kuchapwaa bakoraa au mikia taaa isiyopungua 800 hivi kwa maaana likibumbulukaa ni nchi ndio itakayo aibikaa nani anakumbuka sakata la david mwatobe wa serengeti boys?
Haruna Moshi amezaliwa 31 may 1987..ikiwa na maana umri wake ni miaka 24...Na linapokuja suala la kuitwa katika kikosi cha U23 si jambo la kushangaza na wala huyu kocha hakukusudia kupotosha umma,isipokuwa hili lipo katika soka,mfano mashindani yaliyopita ya European U21 ambayo walishinda Spain,walikuwa na Juan Mata wa Valencia,ambaye umri wake ni miaka 23 na Fainali za michezo ya Olympic kwa upande wa soka inashirikisha wachezaji wa U23 lakini kila timu ina nafasi ya kuita wachezaji watatu waliozidi umri miaka 23.
 
Kha mbona umri mdogo sana 24??? Alafu sura kakomaa kama anapuliza majivu
 
Huyu level yake ni kucheza ndondo au mchangani sijui kwa nini hawa jamaa tulio wapakata juzi wanamng'ang'ania mchezaji ambae hana nidhamu kiasi hiki

Hapo kwenye red umeniacha hoi.Huyu jamaa lazima atakuwa anazipenda sana ndo maana ashindwa kule Sweden.
 
Ni mtanzania mwezetu na huna haki ya kuamru asilitumikie taifa lake....niteja kwa sababu za baba yako fisadi anae nunua madawa na kutu halibia vijana wetu...

Subiri basi uone kama atachezea tena timu ya taifa ndo utajua nina haki ya kuamuru au sina.... Tena Crashwise unitake radhi kwani Baba yangu ni mkulima (Sio kwamba mi mdogo wake pinda), na yupo kijijini na mimi ni kati ya wale wasioamini kama kuna mtu anaharibiwa... Kama nimesoma na wavutabangi tumekaa dawati moja sikuvuta basi kila anayekuwa teja anapaswa kulaumiwa yeye kwa ujinga na tamaa zake na si vinginevyo..... Kwani wewe nawe teja? Kama la kwanini yeye na sio wewe na mimi?

Hapo kwenye Red ni kama sijakuelewa vile....
 
kwa ninavyo jua makabila mengi hapa tanzania mtu alie lika moja na baba yako basi ni baba yako....hivyo basi uuvyazwaji wa madawa ya kulevya una fanywa na watu wazima majina anayo Ki-kwete ndiyo wanaotuhalibbia vijana...kama vijana ndiyo wa kulaumiwa basi wauza madawa tusi wakamate tuwakama watumiaji au unasemaje.....Tena ni hasira na nyie mnao jiita watoto wa wakulima halafu mna tusariti hivi hivi pamoja na kutuzuga na machozi ya kinafiki.....nisamehe kama nilikukwanza
 
Hawa makocha wetu nao wana matatizo sana, Boban kacheza mechi ngapi za mashindano ya Kagame, kama alikuwa na nia ya kumwona kwa nini asingehudhuria mashindano ya Kagame, kwa hiyo kila mchezaji anayetaka kumwona atakuwa anasubiri mechi ya kirafiki ya under 23 ili awaone?
 
Timu ya Taifa kukutana kwake ni mara chache na wachezji wanakaa pamoja kpindi kifupi na klabu wachezaji wanakuwa pamoja muda mrefu,pengine kocha alitaka kumuona anauwezo gani anapokutana na wachezaji ambao hajazoeana nao, na pengine pia alitaka kumuona jinsi atakavyo itikia wito kutokana na mwenendo wa mchezaji husika.
 
Hivi diof wa senegal na Boban nani hana ni dhamu kuna wachezaji wenye nidhamu 0 lakini wana tumikia mataifa yao tatizo kwetu hatuna watu wa kushugulika na watu kama Boban....mwangalie Balloteli,Gaza nk....

Aisee usimtaje huyo mwehu ballotel maana alichokifanya marekani juzi siamini kama anaakili timamu
 
Wewe uliyetoa hiyo thread soma hiyo Makala ndio uandike upupu wako: Genius.[/I]
Neno genius ni mapokeo ya lugha ya kilatini ya neno gigno yaani kuumba au kutengeneza. Kwamba mtu yeyote mwenye kipaji anaweza kufanya jambo ambalo mtu mwingine hawezi kuliwazia wakati huo.
Kuna ma-genius kwenye fani mbalimbali duniani. Albert Einstein kwenye fizikia, Pablo Picasso kwenye uchoraji, Bill Gates kwenye kompyuta na Pele kwenye soka. Wote hao wanafanana kwa vipaji lakini kwenye maeneo tofauti.
Katika kitabu cha Outliers cha Malcom Gladwell, amenukuu utafiti uliofanywa na Anders Ericsson uliobainisha kuwa inachukua takribani saa 10,000 kwa mtu kujifunza hadi kukifahamu kitu. Lakini, utakuta wenzetu ma-genius wamezaliwa tu na vitu hivyo.
Na ndiyo maana kama utawauliza imekuaje waliweza kufanya kitu fulani, wao watakuuliza kwanini umeshindwa kuona kitu kama hicho mapema. Yaani wanajua tu na hawana maelezo ya kwa nini walifanya walichofanya.
Na hawa wana tabia ambazo ni tofauti na tabia zetu sisi watu wa kawaida. Romario alikuwa hataki kufanya mazoezi, George Best alitaka aruhusiwe walau kupiga glasi mbili za pombe kabla hajaingia uwanjani, Rivaldo hakutaka kushea chumba na mtu na Effenberg alikuwa mkorifi balaa.
Kila mtu na kilema chake. Haruna, kwa namna ninavyomfahamu mimi, anataka watu wamwache acheze mpira. Na hata kama hajamwambia yeyote, najua hakufurahishwa na hatua ya yeye kupimwa katika timu ya vijana.
Atapimwaje na vijana ambao kila siku wanaota kuwa na kipaji kama chake? Hivi Boban afanye nini ili tukubali kwamba ana kipaji cha kipekee kwa viwango vya hapa kwetu kwa sasa?
Kama tulivyo sote, Boban naye ana madhaifu yake. Kocha au timu yoyote inayomtaka inatakiwa kujua namna bora ya kumtumia. Lakini si kutaka afanye kila kitu kama sote tunavyotaka. Yeye si kama sisi!
Hatuwezi kumchukia Boban eti kwa sababu alipata timu na kuiacha huko Sweden. Yeye ni mtu mzima na sote tunaishi kwa maamuzi tunayoyafanya katika maisha yetu. Kama alikosea au hakukosea, na kimsingi sote tunakosea, wakati utatuambia.
Vinginevyo, kuna kitu kimoja ambacho Watanzania tunaweza kufanya kwa sasa. TUMWACHE HARUNA MOSHI SHAABANI (BOBAN) acheze mpira.
Makala hii ni mawazo binafsi ya mwandishi na si msimamo wa klabu ya soka ya Simba anakofanyia kazi.
0718 81 48 75]The Official Website of Simba Sports Club
 
Acha unazi,jadili hoja.Huyo Haruna huwezi kumlinganisha hata kwa robo tu ya hao kwenye red na wengineo kama marehemu Hamis Gaga 'Gagarino' tukizungumzia kipaji (acha huo ugenius uliokariri).
 
Back
Top Bottom