Harusi bila wazazi wa kiume wala ndugu upande wa baba pande zote

Harusi bila wazazi wa kiume wala ndugu upande wa baba pande zote

akajasembamba

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2010
Posts
1,179
Reaction score
1,794
Hivi karibuni nikiwa mkoa mmoja kaskazini mwa nchi yetu, nilihudhuria sherehe ya harusi, ambayo pamoja na kushangaa na waliojitambulisha ni wenyeji wa mkoa wa kaskazini na siyo mwambao, sherehe nzima nyimbo zilizotawala ni taarabu za kisasa(rusha roho na mipasho) kingine kilichonishangaza ni kifuatacho:-

Kwa mara ya kwanza niliona ktk utambulisho bwana harusi na bibi harusi wotehawakuwa na baba wala ndugu upande wa baba yaani mashangazi wala mababa wakubwa wala wadogo, waliokuwepo na kutambulishwa ni WAJOMBA, MAMA WADOGO NA MAMA WAKUBWA wa mama wa maharusi yaani madada na makaka wa wamama wa bwana na bi harusi.

Tafsiri niliyopata ni kwamba sasa vijana wengi wanalelewa na single mothers na wanaozwa na single mothers bila kushirikisha wazazi wenzao. Wanashirikisha ndugu zao tu na mjomba anasimama kama baba.

Wanaume wenzangu hili ni janga kubwa watoto kutoshirikisha baba zao ktk harusi, tujitathimini wapi tulikosea je tumetelekeza watoto???? Kama tumetelekeza turudishe mapenzi kwa vijana wetu,Au tumeruhusu serikali ilete sheria za mfumo jike hadi watoto wanaegemea kwa mama na wajomba zao. Sheria hizo zipigwe vita kurudisha haki na heshima za kina baba
 
Usiwaze Sana Mkuu
Punguza Pressure Hilo Jambo Ni Kawaida Sana Pia Inategemea Na Uwezo Wa Mtu Mwenyewe
RC Wao Unaweza Kufunga Ndoa Alfajiri Ukiwa Na:-
Mume, Mke Na Wapambe Wenu Tu Bila Kuhitajika Suit, Shella

Kupanga Ni Kuchagua!!!
 
Usiwaze Sana Mkuu
Punguza Pressure Hilo Jambo Ni Kawaida Sana Pia Inategemea Na Uwezo Wa Mtu Mwenyewe
RC Wao Unaweza Kufunga Ndoa Alfajiri Ukiwa Na:-
Mume, Mke Na Wapambe Wenu Tu Bila Kuhitajika Suit, Shella

Kupanga Ni Kuchagua!!!
Ndoa inafungwa pakiwapo mke na mme
Na mashahidi wawili.
Zingine ni mbwembwe.
 
kwenye swala la ndoa... nakubaliii sanaa ndoa za kiislamu no complications kabisaa yan
 
Haki huendana na wajibu, kama hukulea unapata guts wapi za kutaka haki...
 
Ndoa inafungwa pakiwapo mke na mme
Na mashahidi wawili.
Zingine ni mbwembwe.
Huu Ndiyo Ukweli Wenyewe Tena Mchungu 🤨😑😶😏😐😏
Ndoa Ni Hao Wahusika Tu Na Mfungishaji Tu
Yaani Watu Watano Tukio Tayari
Maandalizi Mengine Ni Ujanjaujanja Tu!!!


Mnaweza Kuandaa Lolote Lile Lakini Mfungishaji Akitoa Udhuru, Ama Muoaji/Muolewaji Ujue Hakuna Ndoa Hapo
Chakula Vinywaji Niko Bure
 
Usiwaze Sana Mkuu
Punguza Pressure Hilo Jambo Ni Kawaida Sana Pia Inategemea Na Uwezo Wa Mtu Mwenyewe
RC Wao Unaweza Kufunga Ndoa Alfajiri Ukiwa Na:-
Mume, Mke Na Wapambe Wenu Tu Bila Kuhitajika Suit, Shella

Kupanga Ni Kuchagua!!!
Sidhani kama ni uwezo kuna tatizo ktk malezi dunia ya sasa, yaani harusi wawepo makaka na madada wa mama wa maharusi tu, ndugu upande wa mama tu wa baba wa bwana harusi wala wa baba wa bi harusi hayupo hata mmoja
 
Mnatongoza wanawake msiokua na malengo nao..niya ikiwa Ni kujiburudisha..huku mkiwaaminisha kuwa.mnawapenda....Siku akikwambia Ana mimba ndo unaanza kuhaha.
 
Back
Top Bottom