akajasembamba
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 1,179
- 1,794
Hivi karibuni nikiwa mkoa mmoja kaskazini mwa nchi yetu, nilihudhuria sherehe ya harusi, ambayo pamoja na kushangaa na waliojitambulisha ni wenyeji wa mkoa wa kaskazini na siyo mwambao, sherehe nzima nyimbo zilizotawala ni taarabu za kisasa(rusha roho na mipasho) kingine kilichonishangaza ni kifuatacho:-
Kwa mara ya kwanza niliona ktk utambulisho bwana harusi na bibi harusi wotehawakuwa na baba wala ndugu upande wa baba yaani mashangazi wala mababa wakubwa wala wadogo, waliokuwepo na kutambulishwa ni WAJOMBA, MAMA WADOGO NA MAMA WAKUBWA wa mama wa maharusi yaani madada na makaka wa wamama wa bwana na bi harusi.
Tafsiri niliyopata ni kwamba sasa vijana wengi wanalelewa na single mothers na wanaozwa na single mothers bila kushirikisha wazazi wenzao. Wanashirikisha ndugu zao tu na mjomba anasimama kama baba.
Wanaume wenzangu hili ni janga kubwa watoto kutoshirikisha baba zao ktk harusi, tujitathimini wapi tulikosea je tumetelekeza watoto???? Kama tumetelekeza turudishe mapenzi kwa vijana wetu,Au tumeruhusu serikali ilete sheria za mfumo jike hadi watoto wanaegemea kwa mama na wajomba zao. Sheria hizo zipigwe vita kurudisha haki na heshima za kina baba