Dunia pana.View attachment 3702335
Kuna matukio mengine ukisikia unajiuliza, ila unakosa majawabu.
Nimekutana na story ya binti anayeitwa Afrah ambaye inadaiwa amefariki dunia zikiwa zimebaki siku tatu tu kabla ya harusi yake.
Kwa mujibu wa taarifa , siku ya send-off akiwa ukumbini alianza kucheka cheka bila sababu zinazoeleweka na kuonesha mabadiliko ya ghafla ya tabia. Familia ikachukua hatua ya kumpeleka kanisani kwa ajili ya maombi, lakini kwa masikitiko makubwa, Afrah akafariki dunia.
Yaani binti alikuwa anajiandaa kuanza maisha mapya, lakini ghafla furaha ya harusi ikageuka kuwa maombolezo.
Sasa hapa ndipo maswali yanapoanzia
Ilikuwaje apate changamoto siku ya tukio la send off?
Kama kuna binadamu kamfanyia huu ubaya yeye anapata faida gani akiona kaburi la huyu binti?
Kuna haja ya kujiweka fresh ili kuepusha husda kama hizi kwenye matukio ya ndoa au yanayofanana na ili au tunaogopa kuitwa washirikina?
Kama kweli kuna watu wanaoweza kutumia nguvu, muda na akili zao kuharibu maisha ya wengine badala ya kujenga maisha yao, basi hilo ni jambo la kusikitisha sana.
Mwisho wa siku, maisha ya binadamu ni mafupi na hatujui kesho yetu.
Mungu ailaze roho ya Afrah mahali pema na awape faraja familia yake.
Ukitaka kujua uchawi upo Anza kupata mafanikio
DuuuuhUkitaka kujua uchawi upo Anza kupata mafanikio
Huyo mganga amfanyie hivyo yule bimaza anaetembea na hirizi kwenye hijabu tuone km kweli inawezekanaInauma sana
Waguse kikurambembona watu kibao maelfu ya watu wanapata mafanikio hawapati madhara?
diamond, mo dewji. fei toto, mama samia, netc
Wakiijua weak spot yao tu kwisha, kuna kiongozi niliambiwa alichanjiwa kucha ya Simba, miiba za Nungunungu zikachangamywa na magamba ya KakakuonaWaguse kikurambe
Ma ex wanaroga balaa ukiwaacha vibaya, kuna watu wanakua over obsessed na mapenz especially yanapoanza kuyumba na kuelekea ukingoni wanqkua tayar kufanya lolote,
So kabla yakuqchia mtu manyoya muangalie kwanza level yqke ya kuzima na uwezo wa ku handle break-up unless otherwise utatupiwa tu mapepo wachafu
Ilkuaje mkuu ?๐๐Kilinikuta hiki kitu
Swali la kitoto kabisa, kwa akili yako unajua hawana Kinga kwenye miili yaombona watu kibao maelfu ya watu wanapata mafanikio hawapati madhara?
diamond, mo dewji. fei toto, mama samia, netc
R.I.P Afrah ๐นView attachment 3702335