Rwandobi Jr
Member
- Oct 5, 2026
- 33
- 66
Kuna wakati mtu anapata mafanikio anatamani kupartika na watu hata wa nje, kushare furaha yake ila wa pembeni tunachukulia ni kafara...Niffer Jovin kafanya party yake kachinja ng'ombe ale na mashabiki wakasema ni kafara, je? Unahisi ni rahisi mtu kuchinja ng'ombe tu afu anapata utajiri, Kama rahisi watu tungetafuta pesa ya kununua ng'ombe wa kafara afu tukae tusubiri kutajirika kwanza nani angekubali kubaki masikini kama ni rahisi hivyo
Masikini tumenyimwa na uwezo wa kufikiri tunafikiria njia rahisi rahisi, yaani masikini muulize yule pale kapataje hela! Wee atakusimlia makafara hayo mpaka koo linamkauka anaomba maji! Ni sawa anachinja ng'ombe anafanya kafara na wewe umeshindwa nini kufanya kama yeye kama ni rahisi hivyo?Na ingekuwa rahisi hata hizo ng'ombe sasa hivi ingekuwa vigumu kuzipata
kumbe dunia ipo hivi? Mungu nishike mkonoHaya ndio mambo huwa wanafanyiana si ajabu hata huyo ni mashosti zake walifanya yao.
Ilikuwaje mzeeKilinikuta hiki kitu