Harusi ya Joti mcity, harusi ya prof jay vs harusi za wasomi za kusumbuana waajiriwa michango

Harusi ya Joti mcity, harusi ya prof jay vs harusi za wasomi za kusumbuana waajiriwa michango

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
habari wadau..

hivi wasomi wa kuajiriwa taasisi za uma na private sector.. kipato chao hakiruhusu kufanya harusi za ukweli.. kama ambao hawajaenda shule kina joti wanavyozifanya...

je ni vipato vidogo au network zao..

maana harusi za wafanyabiashara na wasanii zinakuwa za ukweli.

usawa wa magu huu.. nikiicheki harusi za hawa watu mpaka wananitisha
 
Ndio maana huwa nasema mtu ukitaka kuandaa harusi jipange...mambo ya kutafuta michango ya kizamani...sio lazima ualike kila mtu....watu wa karibu wachache wanatosha...unakuta mtu anaalika kijiji kizima [emoji38][emoji38][emoji38]
 
DSTV wamempa maneno KIBONDE,SI kwa kuwataja huko,kwenye zawadi maalum Azam sikuwaona wala kuitwa kwa namna ya pekee.
 
Mkuu, watumishi wa umma wanapenda na wao kufanya harusi zenye ubora. Tatizo ni kuwa, wasipochangisha jamii wataundiwa tume na takukuru kuwachunguza wametoa mapesa wapi! Ni vema wakaishi kishaitwan! Ni hivyo tu. Egemea kwenye mfano wa "Masamaki" wa nyumba nyingi.
 
habari wadau..

hivi wasomi wa kuajiriwa taasisi za uma na private sector.. kipato chao hakiruhusu kufanya harusi za ukweli.. kama ambao hawajaenda shule kina joti wanavyozifanya...

je ni vipato vidogo au network zao..

maana harusi za wafanyabiashara na wasanii zinakuwa za ukweli.

usawa wa magu huu.. nikiicheki harusi za hawa watu mpaka wananitisha
Ndugu harusi za kifahari zimeongezeka sana licha ya kauli hizi: 'vyuma vimekaza', pesa hakuna n.k. Kama vyuma vingekuwa vimekaza kwa nini harusi za kifahari zinaongezeka?
 
Ndugu harusi za kifahari zimeongezeka sana licha ya kauli hizi: 'vyuma vimekaza', pesa hakuna n.k. Kama vyuma vingekuwa vimekaza kwa nini harusi za kifahari zinaongezeka?
Yani hata mi sielewi huwa wanapataje hayo mahela?
mfano hapa mtaani kuna familia ya kawaida tu..sio wa kipato kikubwa..walifanya vikao vya sendoff ..nashangaa ndan ya mwez mmoja tunaletewa kadi ati inafanyika sijui ndani ya serena..wengine hyatt!
ni sherehe ya kufuru..ukipiga hesabu ni zaod ya milion 20 zimetumika...
watu wana hela bado!
 
Michango miiiiiingiii, kuwe na ratiba ya mwaka mzima ili tujiandae kwa wanaotaka kufunga nikai, ghafula sitoi
 
Wewe unashangaa milioni 20 ??
je harusi ya joti ya milioni 100 haushangai
 
Ndugu harusi za kifahari zimeongezeka sana licha ya kauli hizi: 'vyuma vimekaza', pesa hakuna n.k. Kama vyuma vingekuwa vimekaza kwa nini harusi za kifahari zinaongezeka?
Vyuma vimekaza ndio lakini tembo hata akonde vipi hawezi kuwa kama mbuzi.matajiri nao mdororo wa uchumi umewaathiri lakini bado hawawezi kufanana na sie pangu pakavu.mtu aliyekuwaanaingia milioni kumi lwa siku enzi hizo alafu hivi sasa awe anapata nane atasema hali ni mbaya lakini haiwezi kuwa mbaya kama ya yule aliyekuwa anaingiza alfu 30 saiz anapata 5
 
Basi una lako jambo
nyie ndo wale ambao mna lawama mwisho wa siku mseme kama sio nyie kuchangia harus isingefanyika
michango yenye lawama

Kila mtu na maoni yake. Huku kwetu tunashirikishana kwenye shida na raha. Usiponipa kadi ya mchango kwenye harusi siji.
 
Vyuma vimekaza ndio lakini tembo hata akonde vipi hawezi kuwa kama mbuzi.matajiri nao mdororo wa uchumi umewaathiri lakini bado hawawezi kufanana na sie pangu pakavu.mtu aliyekuwaanaingia milioni kumi lwa siku enzi hizo alafu hivi sasa awe anapata nane atasema hali ni mbaya lakini haiwezi kuwa mbaya kama ya yule aliyekuwa anaingiza alfu 30 saiz anapata 5
Jambo la kushangaza ni kuwa unakuta familia inatamani kufanya harusi ya gharama za milioni kumi ilhali wao wanachangia milioni moja. Hebu fikiria mtu ana shilingi mia tano, anakuomba umuongezee elfu mbili ili anunue bia, utamwelewa kweli?
 
Michango miiiiiingiii, kuwe na ratiba ya mwaka mzima ili tujiandae kwa wanaotaka kufunga nikai, ghafula sitoi
Wengi wa wale unaowachangia hutawaona wewe ukiwa na ukiitisha mchango. Hii mambo itafikia kila mtu atapambana na hali yake.
 
Alafu si lazima ufanye sherehe kubwa ya watu wengi,tujifunze kwa wenzetu,fanya kilicho ndani ya uwezo wako,sherehe za maturembeta mashela,liukumbi likubwa watu 300,na makorokoro mengine zimepitwa na wakati.Harusi hivi sasa ni biashara/industrial complex,mnapigwa hela kijingajinga.Hii industry imebeba wenye makumbi,wapambaji kumbi,wapambaji wanaharusi,watu wa catering,muziki,matarumbeta,washereheshaji etc wote wanapiga hela zenu,fanya shuhuli ndogo ya watu wachache wa karibu isiyo na gharama kubwa.nimeshahudhuria harusi ya watu 30 tu tena ilifana balaa,gharama ndogo.ajabu ni kwamba wale tuliokuwa tunawaiga washabadilika tumebakia sisi tu waafrika kufanya sherehe zisizokuwa na kichwa wala mguu zilizo na maudhui ya tamaduni za ulaya.bado mkoloni anatawala vichwa vya wengi wetu.

Unakuta mtu hana hata kiwanja lakini yuko radhi afosi kufanya sherehe ya siku moja itakayounguza zaidi ya milioni 20 ndani ya siku moja.alafu sherehe zenyewe sasa,zote zinafanana hazina ubunifu wowote.mi ndo maaana huwa harusini naingia saa nne kasoro,nakaa nje mpaka nianze kusikia nyimbo laini najua mida ya buffet tayari ndo naingia
 
Back
Top Bottom