silas maswe
Member
- Jul 28, 2015
- 96
- 130
Naona umeandika kujifurahisha nafsi yako. Nani aliwahi kuthibitisha kiasi cha pesa ambacho alikuwa anamiliki Kambona?
Kama Uingereza ilikuwa inamsaidia Kambona ni kwa nn wakati Mwalimu Nyerere anapinduliwa aliomba msaada kutika Uingereza? Na Uingereza ilituma Kikosi kwenda kuzima vuguvugu la Mapinduzi? Na Uingereza hiyo hiyo ilifanya Msako kwenye Mapori na kuwakamata Waasi
Kama Uingereza ilikuwa inamsaidia Kambona ni kwa nn wakati Mwalimu Nyerere anapinduliwa aliomba msaada kutika Uingereza? Na Uingereza ilituma Kikosi kwenda kuzima vuguvugu la Mapinduzi? Na Uingereza hiyo hiyo ilifanya Msako kwenye Mapori na kuwakamata Waasi
Kuna hypothesis inasema kwamba kukosana kwa Nyerere na Kambona ni kwa sababu Uingereza ilikuwa inamuandaa kichinichini Kambona kumpiku Nyerere. Imenichukua miaka mingi kuiamini hiyo dhana lakini baada ya hii picha sasa ndiyo inaanza kuniingia akilini.
Hebu angalia mazingira ya picha yenyewe. Kwanza Kambona kafungia ndoa Uingereza, siyo Tanganyika. Pesa za bonge la sherehe ya namna hiyo alizipata wapi.
Pili, Kambona alikuwepo TANU ilipoanza kutanuka na hata mwaka 1955 alifungua baadhi ya matawi. Lakini Mwaka 1956 akaenda kusoma, hivyo harusi hiyo ameifanya akiwa mwanafunzi. Tumeshahojia wingi wa pesa za harusi wakati chama chake TANU hakikuwa na pesa. Je, wazungu na askari hao wote pichani walikuwa wanashangialia figure ya aina gani wakati Tanganyia Nyerere alikuwa hakoswi kubambikiziwa kesi na TANU kuonekana chama cha wahuni.
Kama Nyerere alikuwa Best Man basi alimkomesha Kamboa bila kujua maana alijionea kila kitu mwenyewe huko London kuliko angesimuliwa.
OK. Baada ya uhuru inasemekana Kambona alikuwa kila mwaka account yake inaingiziwa mapesa mengi. Kufikia mwaka 1967 Kambona alikuwa ni tajiri kuliko mtu yeyote serikalini. Pesa hizo zilikuwa zinatoka wapi na zilikuwa ni za nini?
Suala la Kambona linahitaji utafiti mwingi lakini hata haya tunaweza kuyamulika na kuyatumia.
Kuhusu Kambona kufika mbali hili ndilo lilikuwa wazo lake na ikiwezekana pia lilimksanisha Nyerere. Kufika mbali maana yake ni kutoka uwaziri na kuwa Rais. Hii ingewezekana kama Nyerere angemzidi kwa miaka kuanzia 15 kwenda juu.
Lakini Kambona na Nyerere hawakuzidiana hata miaka mitano. Hivyo suala la kumrithi lisingewezekana na ndiyo maana Nyerere alilijua akawa na tahadhari na Kambona mapema sana.