Hasheem Thabeet kurudi NBA?

Frank Matrisciano ni NBA Trainer kwahiyo ka-train wengi tu lakini ame-specialize kwenye physique ambalo ndo tatizo kuwa la Hasheem. We Google tu Hell's Trainer na utapata habari zake! WHY Hell? Wengi wanazikimbia training zake soon baada ya kuanza!!!
Mkuu Chige wewe ni moja ya watu ninaowaheshimu sana humu JF. Na sidhani kama wenye heshima hiyo mnazidi watano..

Swali bado hujalijibu, je kati ya hawa ambao walifanikiwa kunaliza training kwa huyo HELL ni wangapi walifanikiwa kuingia NBA? Maana nadhani hapa tunajihaminisha kwamba as long as amefanikiwa kumaliza training kwa huyo jamaa basi ni lazima apate timu.

Lakini mbaya kabisa, hizi Preseason hakuna hata timu moja iliyomuita.. At least angeitwa kwenye timu hata moja kwenye preseason tungejipa matumaini ya yeye kurudi.

Ukweli mchungu ni kwamba Hasheem bado kwa season hii.. Labda aendelee kujifua asubiri timu zikitaka kujiimarisha dirisha ndogo kwa ajili ya kusaka play offs na kujiandaa kwa play offs.. Mwaka jana Cavs walifanya hivyo kumchukua jamaa mwenye 34 kutoka D-League
 
Basi hapa sasa I salute.. Ila tuombe aendelee kukaza asubiri dirisha ndogo.. Timu tayari zimeshatangaza roster zao kwa sasa..
 
Proved mkuu mimi wikipedia ilinidanganya

poa mkuu naona wikipedia ilinidaganya

Pamoja mkuu, unajua ukicheki juu juu utaona wacheza basket ni matalu sana, mimi mwenyewe nilishangaa kusikia eti Hasheem ni The Tallest active player by that time ndo nikaanza kucheki stats za urefu, imagine hata Shaque hafiki kwa Hasheem lakini ni bonge la jitu.
 
Basi hapa sasa I salute.. Ila tuombe aendelee kukaza asubiri dirisha ndogo.. Timu tayari zimeshatangaza roster zao kwa sasa..
Yah, matumaini ni kwenye dirisha dogo; kwa sasa ndo basi tena manake hivi sasa tunahesabu masaa!!! Ile workout iliyofanywa na LA Lakers, Wizards na Knicks inaweza kuwavutia wengi zaidi na hivyo kupata fursa ya kuonesha kwamba Hasheem wa sasa sio yule wa zamani!
 
You better lose yourself in the NBA, The moment
You own it, you better never let it go.You only get one shot, do not miss your chance to blow.This opportunity comes once in a lifetime.....[HASHTAG]#Looser[/HASHTAG]...Bahati haiji mara mbili...Ashapotea kama walivyopotea Eastcoast,Wanaume et al.
 
Kwa hiyo banker wangu chige huyu dogo anarudi NBA?Maana kwa kweli mimi mtiririko wa usajili na namna ligi hiyo inavyoendeshwa mimi ni "ignorant" sana
 

Ila mkuu kuna tofauti ya hao na Hasheem, hao wengine walienda kwa ajili ya kushape-up lakini tayari walikuwa ni proven players.

Hasheem anashape-up na anafanya extra ball game training, hapa nadhani pana tofauti, mimi personally namwombea ila nidhamu inahitajika sana, nimeona jamaa wanajaribu kufananisha situation ya Hasan Whiteside wa Heats na hii ya Hasheem, ila tofauti nayo iona ni kwamba baada ya Hassan kuchemsha NBA alienda ligi za nje, ila Hasheem kwenye maelezo yake anasema hayuko tayari kwenda kucheza nje ya NBA.

Hii ego inaweza ku-cost career yake, kwa sababu nadhani hii misimu mitatu aliyoipoteza alitakiwa awe nje anakipiga huko.
 
Proved mkuu mimi wikipedia ilinidanganya
Haijakudanganya... uliangalia past NBA Players! Wapo ambao Hasheem akisimama ni cha mtoto; mtu kama Gheorghe Mureșan; Hasheem anasubiri! Kuna Mchina fulani hivi, nimesahau jina lake... hadi leo sijapata jibu yule ni Mchina wa aina gani... manake alienda hewani na ameshiba vile vile! Huyu hajaacha basket zamani lakini kwa sasa sio active.
 
Haaa haaa eti ngongoti!?!!


We Chige utakuwa ni Hasheem sio kwa kuumia huku! (Speaking in a jest)
 

Ni Yao Ming, Hall of Famer class of 2016.

Mwaka huu wameingia yeye, Shaq na Allen Iverson.

Jamaa alikuwa mrefu si mchezo.
 
Pamoja na training ya Frank Matrisciano for body fitness lakini pia alikuwa anapata game training toka kwa Milt Newton ambae ni ex-NBA Professional!
 
Pamoja na training ya Frank Matrisciano for body fitness lakini pia alikuwa anapata game training toka kwa Milt Newton ambae ni ex-NBA Professional!

Nimeona ile article, na jamaa wanashangaa eti kwa kipindi chote cha yeye kuwa NBA hajafundishwa vitu alivyotakiwa kuwa amefundishwa!

So ni kama wanaanza naye mwanzo, ngoja tuone kama itawork out.
 
Ndo maana mkuu big gift nilimuuliza ushawahi muona ngongoti live?

Hasheem ni mrefu acheni maskhara nyie, labda hao kina Jordan ambao sijawaona live

Ni mrefu kila mtu bills alikalishwa! Mi moyo ulikuwa unanidunda alipofika mezani kwetu!
 
Ni Yao Ming, Hall of Famer class of 2016.

Mwaka huu wameingia yeye, Shaq na Allen Iverson.

Jamaa alikuwa mrefu si mchezo.
Sure! Ni ya Yao Ming... jamaa kaenda hewani bhana, duh! Tena unlike Gheorghe Mureșan, Yao kashiba vile vile...! Na ukimuona kwa sasa ndo unapata picha halisi ya giants ni watu wa aina gani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…