Hasheem Thabeet kurudi NBA?

Hasheem Thabeet kurudi NBA?

Haijakudanganya... uliangalia past NBA Players! Wapo ambao Hasheem akisimama ni cha mtoto; mtu kama Gheorghe Mureșan; Hasheem anasubiri! Kuna Mchina fulani hivi, nimesahau jina lake... hadi leo sijapata jibu yule ni Mchina wa aina gani... manake alienda hewani na ameshiba vile vile! Huyu hajaacha basket zamani lakini kwa sasa sio active.
huyu muresani nimemwona ni hatarii duu
 
Hasheem akaze buti ila ajue chama la wana saiv tumeongeza mnyama mwingine KD alaf kuna clay thompson,andre iguodala,draymond green n the beast himself chief curry lazma tubebe uchamp
 
Nimeona ile article, na jamaa wanashangaa eti kwa kipindi chote cha yeye kuwa NBA hajafundishwa vitu alivyotakiwa kuwa amefundishwa!

So ni kama wanaanza naye mwanzo, ngoja tuone kama itawork out.
Inasikitisha sana kwa kweli! Na suala la physique, ni kweli Hasheem hakuwa fit kivile... ile body ilimzidi na matokeo yake hakukuwa na coordination kati ya mwili na uchezaji!
 
Ndo maana mkuu big gift nilimuuliza ushawahi muona ngongoti live?

Hasheem ni mrefu acheni maskhara nyie, labda hao kina Jordan ambao sijawaona live

Ni mrefu kila mtu bills alikalishwa! Mi moyo ulikuwa unanidunda alipofika mezani kwetu!
Ukikutana nae kwa mara ya kwanza, halafu ndo usiku uchororoni; lazima utoke ndoki na kwenda kusimulia kwamba umekutana na jini!!!
 
Inasikitisha sana kwa kweli! Na suala la physique, ni kweli Hasheem hakuwa fit kivile... ile body ilimzidi na matokeo yake hakukuwa na coordination kati ya mwili na uchezaji!

Nakumbuka kuna interview alifanya Jahazi na kina Kibonde baada ta kuacha Portland Trail Blazers na kuchukuliwa na kina OKC, akaulizwa kwa nini timu zinamwacha, haoni kama kuna umuhimu wa kufanya jitihada zaidi ili aweze kudumu na timu kwa muda mrefu, yeye aliwajibu akisema hajali sana as long as mshiko unabaki ni ule ule (kwenye ule mkataba alikua na USD 1.2 m kwa mwaka na alikuwa amebakiza misimu 3 au 2 sikumbuki vizuri).

Sasa kwa mentality ile ilikuwa ni lazima haya yamkute, alichokuwa anajali ni pesa na kutumia, hope unajua skendo zake za hapa TZ, na kule majuu nako inasemekana ana watoto wanne au zaidi kwa mama tofauti tofauti.
 
Mkuu Chige wewe ni moja ya watu ninaowaheshimu sana humu JF. Na sidhani kama wenye heshima hiyo mnazidi watano..

Swali bado hujalijibu, je kati ya hawa ambao walifanikiwa kunaliza training kwa huyo HELL ni wangapi walifanikiwa kuingia NBA? Maana nadhani hapa tunajihaminisha kwamba as long as amefanikiwa kumaliza training kwa huyo jamaa basi ni lazima apate timu.

Lakini mbaya kabisa, hizi Preseason hakuna hata timu moja iliyomuita.. At least angeitwa kwenye timu hata moja kwenye preseason tungejipa matumaini ya yeye kurudi.

Ukweli mchungu ni kwamba Hasheem bado kwa season hii.. Labda aendelee kujifua asubiri timu zikitaka kujiimarisha dirisha ndogo kwa ajili ya kusaka play offs na kujiandaa kwa play offs.. Mwaka jana Cavs walifanya hivyo kumchukua jamaa mwenye 34 kutoka D-League
Hii post nilichelewa kuiona! Bila shaka uliiandika kabla sijakupa lile jibu kwahiyo nadhani jibu lishapatikana; au sio?
 
Pamoja mkuu, unajua ukicheki juu juu utaona wacheza basket ni matalu sana, mimi mwenyewe nilishangaa kusikia eti Hasheem ni The Tallest active player by that time ndo nikaanza kucheki stats za urefu, imagine hata Shaque hafiki kwa Hasheem lakini ni bonge la jitu.
Aah Shaquel O'Neal ni noma ni jitu hasa mi namfatiliaga kwenye stand up comedy za Chris Tucker....asee kama Hasheem anamzidi na huyu ni nyokolost

Mi nilivyomuona siku hiyo live nikasema kweli TV inadanganya asee
 
kwa tunaofatilia basketball kwa ujumla kuanzia college ball ya usa.. ueroleague na nba tunajua ukweli...

kupata chance ya kucheza nba kwa mara ya pili ni ngumu sana na sana...

maana kila mwaka kuna wachezaji kibao wanaisaka hiyo chance...

nba rules kila timu haitakiwi kuwa na wachezaji wanaozidi 15,, na nba ina team 30... so total.nba players per year ni 450 tu...

sasa kuna wachezaji maelfu na maelfu kuanzia usa kwenyewe na duniani kote wanagombea chance kila mwaka...

ni rahisi sana kutokea euroleague na kuingia nba kuliko kutokea d league kuingia nba
 
Ndo maana mkuu big gift nilimuuliza ushawahi muona ngongoti live?

Hasheem ni mrefu acheni maskhara nyie, labda hao kina Jordan ambao sijawaona live

Ni mrefu kila mtu bills alikalishwa! Mi moyo ulikuwa unanidunda alipofika mezani kwetu!
mh sijawahi kukutana na hao watu si ajabu nitimue mbio kusikofahamika
 
Nakumbuka kuna interview alifanya Jahazi na kina Kibonde baada ta kuacha Portland Trail Blazers na kuchukuliwa na kina OKC, akaulizwa kwa nini timu zinamwacha, haoni kama kuna umuhimu wa kufanya jitihada zaidi ili aweze kudumu na timu kwa muda mrefu, yeye aliwajibu akisema hajali sana as long as mshiko unabaki ni ule ule (kwenye ule mkataba alikua na USD 1.2 m kwa mwaka na alikuwa amebakiza misimu 3 au 2 sikumbuki vizuri).

Sasa kwa mentality ile ilikuwa ni lazima haya yamkute, alichokuwa anajali ni pesa na kutumia, hope unajua skendo zake za hapa TZ, na kule majuu nako inasemekana ana watoto wanne au zaidi kwa mama tofauti tofauti.
Dah! Sikupata fursa ya kuisikia hiyo interview... ni very stupid response! Ndo matatizo ya unaanza kuangalia hadi mwisho wa mwaka unakuwa na mpunga kiasi gani; halafu unaanza kuhesabu washikaji wa Sinza na Kinondoni kuangalia ni nani anaweza kuwa na kiasi kama hicho! Yaani ki ukweli ndo vile tunalazimika kumuombea Mungu lakini Hasheem alijisahau sana! Huku kushituka alikoshituka sasa angefanya mara baada ya kutoka Memphis Grizzlies; hivi sasa jamaa ingekuwa kesharudi NBA! Kwanza body yake ni mtaji mzuri sana lakini alipoharibu ni pale alipodhani body peke yake ingetosha kumweka NBA!
 
Aah Shaquel O'Neal ni noma ni jitu hasa mi namfatiliaga kwenye stand up comedy za Chris Tucker....asee kama Hasheem anamzidi na huyu ni nyokolost

Mi nilivyomuona siku hiyo live nikasema kweli TV inadanganya asee

Umeona eeh, Shaq ana 7'1" wakati Hasheem ana 7'3", unaweza kuona ni kwa kiasi gani Hasheem ni tall, maana ukimwangalia Shaq kwenye TV kwenyewe hatoshi.
 
kwa tunaofatilia basketball kwa ujumla kuanzia college ball ya usa.. ueroleague na nba tunajua ukweli...

kupata chance ya kucheza nba kwa mara ya pili ni ngumu sana na sana...

maana kila mwaka kuna wachezaji kibao wanaisaka hiyo chance...

nba rules kila timu haitakiwi kuwa na wachezaji wanaozidi 15,, na nba ina team 30... so total.nba players per year ni 450 tu...

sasa kuna wachezaji maelfu na maelfu kuanzia usa kwenyewe na duniani kote wanagombea chance kila mwaka...

ni rahisi sana kutokea euroleague na kuingia nba kuliko kutokea d league kuingia nba
mkuu jamaa kweli ni keylaza inamaana muda wote aliokaa huko hajajifunza tuu?
 
kwa tunaofatilia basketball kwa ujumla kuanzia college ball ya usa.. ueroleague na nba tunajua ukweli...

kupata chance ya kucheza nba kwa mara ya pili ni ngumu sana na sana...

maana kila mwaka kuna wachezaji kibao wanaisaka hiyo chance...

nba rules kila timu haitakiwi kuwa na wachezaji wanaozidi 15,, na nba ina team 30... so total.nba players per year ni 450 tu...

sasa kuna wachezaji maelfu na maelfu kuanzia usa kwenyewe na duniani kote wanagombea chance kila mwaka...

ni rahisi sana kutokea euroleague na kuingia nba kuliko kutokea d league kuingia nba
Na ndio maana mwisho nikatoa ushauri si vibaya akitupa jicho kwenye league zingine... ninachopenda mimi ni determination yake ya kutaka kurudi NBA... hii determination ndiyo itakayomwezesha kuwa bado active na kumwea rahisi hata akitaka kwenda kwenye ligi zingine! But all in all, hakuna kinachoshindikana... ni ngumu kupata second chance lakini wapo wanaopata!
 
Haijakudanganya... uliangalia past NBA Players! Wapo ambao Hasheem akisimama ni cha mtoto; mtu kama Gheorghe Mureșan; Hasheem anasubiri! Kuna Mchina fulani hivi, nimesahau jina lake... hadi leo sijapata jibu yule ni Mchina wa aina gani... manake alienda hewani na ameshiba vile vile! Huyu hajaacha basket zamani lakini kwa sasa sio active.
Yao ming alistaafu 2011
 
Back
Top Bottom