Uchaguzi 2020 Hashim Rungwe Spunda atia nia ya kugombea Urais, asema Sera yake ya kuimarisha lishe bora kwa Watanzania ipo pale pale

Uchaguzi 2020 Hashim Rungwe Spunda atia nia ya kugombea Urais, asema Sera yake ya kuimarisha lishe bora kwa Watanzania ipo pale pale

Mzee alisema 2015aliibiwa kura maana waliompa pole ni wengi kuliko kura alizopata
 

Attachments

  • 255710802575_status_9dfc5c32bba340509bf5d5705b51e5d1.jpg
    255710802575_status_9dfc5c32bba340509bf5d5705b51e5d1.jpg
    37.6 KB · Views: 4
Wakili msomi huyu
Hapana Huyu huwa anasikika hata kipindi ambacho siyo cha uchaguzi.

Huwa anaitishaga mikutano na waandishi wa Habari na huwa anazungumza hoja zenye nguvu sana!

Mara kadhaa amekuwa akifanya hivyo.

Ningekuwa na clips zake ningekurushia uone akishusha Nondo na madini mazito!

Jamaa yuko vizuri sana !
 
Chagua Spunda (Hashimu Rungwe), udumavu ni tatizo kubwa sana kwa watanzania, lishe duni inazalisha vijana waliodumaa kimwili na kiakili.

Kijana wa miaka 25 ukimuangalia Afya yake utafikiri mtoto wa miaka 14 bwana, Chagua Spunda tupate lishe bora tujenge taifa la magiant na magenius..

Bado kuna zile sera la kumwagilia mashamba kqa ndege na helicopter, kupeleka bahari mpaka dodoma, tutaunganisha Ziwa victoria na bahari ya hindi ili Maersk line, Mesina nk zifike mpaka Mwanza.. Chini ya Rungwe spunda Taifa litapaa maana ni mtu mwenye IQ kubwa na exposure iliyotukuka..
 
"Nitahakikisha Mtanzania anakuwa na uwezo wa kula kuku mzima na wanafunzi wale ubwabwa mara kwa mara"

[emoji23][emoji23][emoji23] Huyu mzee ana sera nzuri,nashauri wanawake wamuunge mkono maana kuku nje nje,tena mzima

2015 ilikuwa anunue ndege za kumwagilia mashamba ya wakulima nchi nzima,hakuna kusubiri mvua
 
Hashim Rungwe Spunda ametia nia kugombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba kwa tiketi ya CHAUMA

Amesema, "Sera yangu ya kuimarisha lishe kwa watanzania bado iko palepale. Nitahakikisha Mtanzania anakuwa na uwezo wa kula kuku mzima na wanafunzi wale ubwabwa mara kwa mara. Elimu bure bila lishe bora haina tija, hata viwanda bila lishe bora haviwezi kuzalisha kwa manufaa"

View attachment 1509973
Huyu ndo nampa kura yangu
 
Spundanomics = Ubwabwa na Kuku Mzima kwa Kila Mtanzania
Masai Hali kuku Wala mchaga na jaluo Hali ubwabwa Ni ugali Dona la nguvu na wahehe hawali wali wanaita chenga za mahindi ukitwanga kwenye kinu ukipata unga chenga zinazobaki wanapewa watoto wapikie kwenye vikopo wakicheza .Mchele kule Huwezi mwekea mtu mzima kwenye sherehe muwekee nyama choma na ugali wa nguvu Ndio anajua umemheshimu wali anachukulia kuwa umemdharau umempa chenga nilishafanya kazi hotelini nawajua
 
Wala ubwabwa wengi Wana IQ Ndogo akiwemo huyo mgombea Uraisi Rungwe Wala ubwabwa mfululizo wachache Sana wenye akili


Ubwabwa umetumika kama lugha ya picha kuwakilisha chakula cha msingi!

Hata kwenye Biblia takatifu kwenye sala ya Baba yetu uliyembinguni ......

Imeandikwa “utupe mkate wetu wa kila siku”

Sasa nikuulize;

Kwani watu wa mataifa yote duniani mkate kwao ni chakula cha msingi?

Ile ni lugha ya picha ya kuwakilisha chakula cha msingi kutegemeana na tamaduni za watu wa mataifa mbalimbali.

Pia inawakilisha riziki ya kila siku.

Vivyo hivyo bwana Spunda anamaanisha chakula ambapo yaweza kuwa wali, ugali, ndizi , makande n.k

Kwamba atahakikisha vinapatikana kwa wingi ili watu wapate lishe bora na akili njema!

Kwa hiyo muunge mkono tu jamani!
 
Mzee wa mishemishe muzee ya mujini Mh. Hashim Rungwe Spunda ana mawazo mazuri, ma deal ya fursa ndani na nje kwa vijana yataongezeka kila kijana kupewa pasipoti kubwa tushindwe wenyewe kuvuka maboda kwenda kufanya shughuli za halali.
 
15 Julai 2020
EXCLUSIVE INTERVIEW NA HASHIM RUNGWE/ MIPANGO YA URAIS 2020 /TATHIMINI MIAKA MITANO YA RAIS JPM

Hashim Rungwe Spunda : Rais amewasahau wananchi, bado ana deni kubwa tunataka kumsaidia. Baba huwezi kununua Mercedes Benz huku watoto mavazi yao yamechanika na kuwalazimisha wapige makofi...hii haiwezekani...hakuna miujiza amefanya...ni mambo ya kawaida.. mimi nimekwenda Germany bado wajenga... ni mambo ya kawaida....


source : Jicholauswazi
 
Hayo makabila yote uliyotaja kwao ubwabwa ni chakula cha siku ya Kipaimara na Christimass au Eid. Wote wanapenda ubwabwa sema ndiyo hivyo tena....


Ni kweli wote wanapenda sema hali ya uchumi inawafanya wasiweze kumudu kula wali kila siku Ndiyo maana wanaishia kupika siku ya Eid na Pasaka/Xmas tu [emoji108][emoji108][emoji108]

Na siajabu wapo wengi tu hata sikukuu nyingine zinapita bila kula pilau au wali sababu uwezo wa kuwa na pesa ya kununua Mchele hawana.

Kuna watu wengi wanapenda kula ugali siyo sababu wanapenda bali uwezo wa kununua Mchele kila siku hawana!
 
Chagua Spunda (Hashimu Rungwe), udumavu ni tatizo kubwa sana kwa watanzania, lishe duni inazalisha vijana waliodumaa kimwili na kiakili.

Kijana wa miaka 25 ukimuangalia Afya yake utafikiri mtoto wa miaka 14 bwana, Chagua Spunda tupate lishe bora tujenge taifa la magiant na magenius..

Bado kuna zile sera la kumwagilia mashamba kqa ndege na helicopter, kupeleka bahari mpaka dodoma, tutaunganisha Ziwa victoria na bahari ya hindi ili Maersk line, Mesina nk zifike mpaka Mwanza.. Chini ya Rungwe spunda Taifa litapaa maana ni mtu mwenye IQ kubwa na exposure iliyotukuka..
Duh
Mzee Hashimu.R
Hakati tamaa japo umri umeenda Sana💪💪💪
 
Back
Top Bottom