Hasira yatawala Moscow baada ya NATO kuiruhusu Ukraine kushambulia ndani ya Russia kwa silaha za NATO

Hasira yatawala Moscow baada ya NATO kuiruhusu Ukraine kushambulia ndani ya Russia kwa silaha za NATO

Hizi ni hatua za kijinga kabisa! Lengo la nchi za NATO ni kutaka Russia na Ukraine ziangamizane kabisa huku nchi hizo zikishangilia.
Hizo silaha hazitabadili cho chote kwenye uwanja wa Vita bali kurefusha mgogoro na kusababisha maafa makubwa kwa Russia na Ukraine.
Niseme tu US na EU zinahitaji mabadiliko ya utawala!
Ukraine na Russia hakuna aliyetayari kuzungumza kwa sasa, hivyo vita vitaendelea tu.
 
Right to self defence ukivamia nchi ya watu, aliyevamiwa ana haki ya kujilinda na kujibu mashambulizi hata kukufuata hadi ulipotoka unakopanga mashambulizi kama tulivyomfuata Idd Amin Uganda au Israel ilivyoingia Gaza, na ni sahihi watoa msaada wa silaha kwa Ukraine kuondoa masharti ya kuzuia Ukraine kujibu hadi Urusi. Lazma warusi waonje ladha ya kukubali kuongozwa na Rais mwehu na muuaji kama Putin.
 
Nadhani Urusi inatakiwa kuonyesha nguvu zake sasa Choma Ukraine kutoka Angle zote ikalie kabisa halafu tuanzie hapo mjadala
 
Urusi imeishutumu Nato na Marekani kwa "kuchochea kiwango kipya cha mvutano" baada ya Marekani na Ujerumani kuwa washirika wa hivi punde kuruhusu jeshi la Ukraine kutumia silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi kushambulia maeneo ndani ya Urusi.

Msemaji wa Berlin alisema Ujerumani ina imani kuwa Ukraine ina haki ya kujilinda dhidi ya Urusi, haswa kutokana na mashambulizi ya mpakani kwenye mji wake wa pili kwa ukubwa wa Kharkiv.

Chanzo: BBC
Ujerumani ya zamani inarudi kwa kasi sana baada ya kuitawala ulaya
 
Ni sawa kabisa ila shida ni kwamba hizo nguvu ndio hana sasa ka nchi kadogo hivyo mwaka wa tatu bado unajikanyaga tu. Russia ni nyuki wa mashineni tu hana lolote.
USA na washirika wake miaka 20 Afghanistan
Wachunga mbuzi wa kitaliban waliwatoa kamasi
 
Back
Top Bottom