Down To Earth
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 21,940
- 16,643
Nini kinamfelisha Russia kushindwa kumaliza vita huko ukraine
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo vita itakuwa fupi kwa Ukraine kushindwa kushambulia ndani ya Urusi?kichwani kuna contents gani?Hizi ni hatua za kijinga kabisa! Lengo la nchi za NATO ni kutaka Russia na Ukraine ziangamizane kabisa huku nchi hizo zikishangilia.
Hizo silaha hazitabadili cho chote kwenye uwanja wa Vita bali kurefusha mgogoro na kusababisha maafa makubwa kwa Russia na Ukraine.
Niseme tu US na EU zinahitaji mabadiliko ya utawala!
Dimitri Peskov alisema Crimea ikiguswa itakuwa ni "judgement day", kwa sasa Ukraine anajipigia Crimea kadiri anavyotaka. Urusi ni kelele tu, kwa sasa silaha zinakata, Putin kashaanza kupiga magoti Korea Kaskazini na China.Kitakachofuata hapo Kiev mimi yangu macho
Nadhani Urusi inatakiwa kuonyesha nguvu zake sasa Choma Ukraine kutoka Angle zote ikalie kabisa halafu tuanzie hapo mjadala
kwamba Russia alichokozwa kwa kushauliwa asivamie Ukraine ? au alichokozwa kwa kuchochea uasi ndan ya Ukraine , hii nchi haipigi hatua sababu watu mmekuwa wanafiki sana , KWEL mnafanya iwe uongoHuwezi kuitafuta amani ya Dunia kwa kumchokoza Dubu.
Amani ya kweli itspatikana kwa maridhiano
.Hili jambo litaleta maafa siku za karibuni
Tunaenda mwaka wa 3 Kiev ikishambuliwa , kwahiyo hakuna jipya.Kitakachofuata hapo Kiev mimi yangu macho
Umeeleza vitu unavyovijua wewe mwenyewe. Wakati vita vinaanza Ukraine hakuwa na silaha zozote za maana zaidi ya silaha za zamani za USSR, ndio maana hata USA walimshauri Rais wa Ukraine akimbie ikihofiwa Kyiv ingetekwa ndani ya siku chache. Silaha nyingi kama HIMARS, vifaru, stingers, ndege vita etc vilikuja baada ya vita kuanza. Hivyo, hoja ya silaha na mamluki haina mashiko yoyote.nadhani unawa-overestimate sana nato mkuu,
hao ni watu wenye akili za kawaida kama mimi na wewe, tofauti tu ni kwamba wao wako nchi hizo na sisi huku tunaongozwa na wagonjwa, thats all.....
nirudi kwenye hoja yako,
nato walianza kujiandaa na hii vita toka 2014 (au kabla ya hapo), ndio maana kwa kuanzia wakampindua raisi pro russia wa ukraine mwaka 2014.... reaction ya fadta ya putin ikawa kuichukua crimea (fuatilia umuhimu wa crimea strategically kwa russia)
wakaanza kutrain jeshi la ukraine toka hapo, wakapeleka vifaa vingi vya kisawa n.k.... (rejea trip za senetors wa US kule kiev)
kwahio, wakati hii vita inaanza mwaka juzi, nato walikua na uhakika ukraine atawasumbua warusi, maana walipeleka pia mercenaries wa kutosha, lkn matokeo yake ndio hivyo, alipigwa na vifaa vyote alivyopewa vikateketezwa......
ndipo wakaanza kutoa msaada wa silaha, ambazo nazo zinateketezwa kila siku....... mpk leo tuko hapa wanazidi kuchapwa,
kwaio hii ya leo sio mpya, bahati mbaya hapa atakayeumia zaidi ni ukraine, maana urusi ataanza kuwafukuza mbali na mipaka yake, usishangae kusikia kiev haikaliki ndani ya miez kadhaa ijayo.......
muhimu, tuwaombee wafanya maamuzi akili ziwarudi, maana wanakoelekea zitapigwa kavu kavu
Miaka 20 NATO wakiwa KabulTunaenda mwaka wa 3 Kiev ikishambuliwa , kwahiyo hakuna jipya.
Sahihi kabisa. Alikuwa us au NATO?Miaka 20 NATO wakiwa Kabul
Matokeo yake walipakimbia na kuwaacha wa Taliban na nchi yao
Kama sijakosea umoja wa kisovieti walipakalia takribani, miaka 8 wakapakimbiaSahihi kabisa. Alikuwa us au NATO?
Kabul pagumu, hata Russia aliwahi pakimbia.
Jamaa una siyo tu mahaba na magharibi bali hayo ni mahabati maana ukisema NATO wanatumia akili kwenye vita sijui ni nani ambae hatumii akili kwenye vita, na kusema kuwa kuna 18 za kumuingiza Russia sijajua hiyo ni nchi gani itakayothubutu kuiweka hiyo 18 maana vikwazo maelfu havijafua dafu ndo iwe 18? Sasa subiri makombora yaingie urusi halafu tuone huko KIEV kitabaki kitu ganiNATO walipanga bajeti ya kuisaidia Ukraine kwa takribani miaka mitano, mwanzoni wakasema wanaisaidia Ukraine ili wajilinde tu na sio kushambulia.
Kwa sasa wanatoa silaha za mashambulizi ili Ukraine ashambulie ndani ya ardhi ya Russia. Hii inatupa picha kwamba kuna namna wameshamuweza Russia ndo maana wanamchokonoa wanavyotaka ili Russia aingie kwenye 18 mazima.
Nlichogundua ni kwamba, nchi za Magharibi wanafanya mambo yao kwa akili nyingi sana, jamaa wanaitazama 2070 wakiwa leo 2024. Kila move wanayopiga hawa jamaa hawaipigi kwa bahati mbaya.