Mkuu uko sahihi!NATO walipanga bajeti ya kuisaidia Ukraine kwa takribani miaka mitano, mwanzoni wakasema wanaisaidia Ukraine ili wajilinde tu na sio kushambulia.
Kwa sasa wanatoa silaha za mashambulizi ili Ukraine ashambulie ndani ya ardhi ya Russia. Hii inatupa picha kwamba kuna namna wameshamuweza Russia ndo maana wanamchokonoa wanavyotaka ili Russia aingie kwenye 18 mazima.
Nlichogundua ni kwamba, nchi za Magharibi wanafanya mambo yao kwa akili nyingi sana, jamaa wanaitazama 2070 wakiwa leo 2024. Kila move wanayopiga hawa jamaa hawaipigi kwa bahati mbaya.
Kitu ambacho nimeona NATO walifanya ni kupima Defensive Systems za Russia! Sasa hivi zile S400 ambazo Russia ilijivunia hazina efficiency yo yote!
Mfano ziliwekwa pale Crimea zilipigwa na storm shadow na drones na sasa pale Russia Navy inapigwa vizuri tu.