Hasira yatawala Moscow baada ya NATO kuiruhusu Ukraine kushambulia ndani ya Russia kwa silaha za NATO

Hasira yatawala Moscow baada ya NATO kuiruhusu Ukraine kushambulia ndani ya Russia kwa silaha za NATO

NATO walipanga bajeti ya kuisaidia Ukraine kwa takribani miaka mitano, mwanzoni wakasema wanaisaidia Ukraine ili wajilinde tu na sio kushambulia.

Kwa sasa wanatoa silaha za mashambulizi ili Ukraine ashambulie ndani ya ardhi ya Russia. Hii inatupa picha kwamba kuna namna wameshamuweza Russia ndo maana wanamchokonoa wanavyotaka ili Russia aingie kwenye 18 mazima.

Nlichogundua ni kwamba, nchi za Magharibi wanafanya mambo yao kwa akili nyingi sana, jamaa wanaitazama 2070 wakiwa leo 2024. Kila move wanayopiga hawa jamaa hawaipigi kwa bahati mbaya.
Mkuu uko sahihi!
Kitu ambacho nimeona NATO walifanya ni kupima Defensive Systems za Russia! Sasa hivi zile S400 ambazo Russia ilijivunia hazina efficiency yo yote!
Mfano ziliwekwa pale Crimea zilipigwa na storm shadow na drones na sasa pale Russia Navy inapigwa vizuri tu.
 
NATO walipanga bajeti ya kuisaidia Ukraine kwa takribani miaka mitano, mwanzoni wakasema wanaisaidia Ukraine ili wajilinde tu na sio kushambulia.

Kwa sasa wanatoa silaha za mashambulizi ili Ukraine ashambulie ndani ya ardhi ya Russia. Hii inatupa picha kwamba kuna namna wameshamuweza Russia ndo maana wanamchokonoa wanavyotaka ili Russia aingie kwenye 18 mazima.

Nlichogundua ni kwamba, nchi za Magharibi wanafanya mambo yao kwa akili nyingi sana, jamaa wanaitazama 2070 wakiwa leo 2024. Kila move wanayopiga hawa jamaa hawaipigi kwa bahati mbaya.
Uko sahihi. Na kwa kuongezea, Marekani na Ulaya siku zote wamekuwa wakitaka kuidhoofisha Russia ili kuleta Amani Ulaya na duniani. Kilichokuwa kinasubiriwa ni kisingizio. Na bila kujua Putin na Russia yake wakaingia kichwakichwa.
 
nadhani unawa-overestimate sana nato mkuu,
hao ni watu wenye akili za kawaida kama mimi na wewe, tofauti tu ni kwamba wao wako nchi hizo na sisi huku tunaongozwa na wagonjwa, thats all.....

nirudi kwenye hoja yako,
nato walianza kujiandaa na hii vita toka 2014 (au kabla ya hapo), ndio maana kwa kuanzia wakampindua raisi pro russia wa ukraine mwaka 2014.... reaction ya fadta ya putin ikawa kuichukua crimea (fuatilia umuhimu wa crimea strategically kwa russia)

wakaanza kutrain jeshi la ukraine toka hapo, wakapeleka vifaa vingi vya kisawa n.k.... (rejea trip za senetors wa US kule kiev)

kwahio, wakati hii vita inaanza mwaka juzi, nato walikua na uhakika ukraine atawasumbua warusi, maana walipeleka pia mercenaries wa kutosha, lkn matokeo yake ndio hivyo, alipigwa na vifaa vyote alivyopewa vikateketezwa......

ndipo wakaanza kutoa msaada wa silaha, ambazo nazo zinateketezwa kila siku....... mpk leo tuko hapa wanazidi kuchapwa,

kwaio hii ya leo sio mpya, bahati mbaya hapa atakayeumia zaidi ni ukraine, maana urusi ataanza kuwafukuza mbali na mipaka yake, usishangae kusikia kiev haikaliki ndani ya miez kadhaa ijayo.......

muhimu, tuwaombee wafanya maamuzi akili ziwarudi, maana wanakoelekea zitapigwa kavu kavu
Russia mlisema ataichukua Ukraine in 2 weeks, miaka mingapi sasa😂
 
Uko sahihi. Na kwa kuongezea, Marekani na Ulaya siku zote wamekuwa wakitaka kuidhoofisha Russia ili kuleta Amani Ulaya na duniani. Kilichokuwa kinasubiriwa ni kisingizio. Na bila kujua Putin na Russia yake wakaingia kichwakichwa.
Huwezi kuitafuta amani ya Dunia kwa kumchokoza Dubu.
Amani ya kweli itspatikana kwa maridhiano
 
Huwezi kuitafuta amani ya Dunia kwa kumchokoza Dubu.
Amani ya kweli itspatikana kwa maridhiano
Ngoja wamchokoze tuone. Taarifa za Pentagon zinasema wanatarajia Vita vya Ukraine vichukue zaidi ya miaka kumi na wamejiandaa. Huyo Dubu at survive!?
 
Putin ni muoga na dhaifu, anaigopa Nato. Putin ana mikwara kibao lakini action sifuri.
 
Putin anapukuchuliwa kidogo kidogo!

Maumivu yake ataanza kuyapata baada ya miaka kama 5 inayokuja
 
Urusi imeishutumu Nato na Marekani kwa "kuchochea kiwango kipya cha mvutano" baada ya Marekani na Ujerumani kuwa washirika wa hivi punde kuruhusu jeshi la Ukraine kutumia silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi kushambulia maeneo ndani ya Urusi.

Msemaji wa Berlin alisema Ujerumani ina imani kuwa Ukraine ina haki ya kujilinda dhidi ya Urusi, haswa kutokana na mashambulizi ya mpakani kwenye mji wake wa pili kwa ukubwa wa Kharkiv.

Chanzo: BBC
Urusi anatafuta nini Ukraine kwanini asirudi kwake
 
Hizi ni hatua za kijinga kabisa! Lengo la nchi za NATO ni kutaka Russia na Ukraine ziangamizane kabisa huku nchi hizo zikishangilia.
Hizo silaha hazitabadili cho chote kwenye uwanja wa Vita bali kurefusha mgogoro na kusababisha maafa makubwa kwa Russia na Ukraine.
Niseme tu US na EU zinahitaji mabadiliko ya utawala!
Russian ndo wa kulaumiwa. Ukraine ni wa kuurumiwa tu, kuwa na jirani mkorofi kama Russia ni changamoto. Russia amegombana na majirani zake wengi.
NATO kuzuia ukraine kumshambulia ndani ya Russia ni ujinga. Yahani Russia wnaorganise majeshi na silaha kisha kuzileta mpakani wanaangaliwa tu, kisha wanavuka mpaka na kuanzia kuwaua ndo mnaanza kujibu?. Tena wakati mwengine Russia anawaua wa Ukraine bila kuvuka mpaka!.
 
Uko sahihi. Na kwa kuongezea, Marekani na Ulaya siku zote wamekuwa wakitaka kuidhoofisha Russia ili kuleta Amani Ulaya na duniani. Kilichokuwa kinasubiriwa ni kisingizio. Na bila kujua Putin na Russia yake wakaingia kichwakichwa.
Naam, japo nachelea kuamini kuwa amani ya dunia inahatarishwa na Russia.
 
Russian ndo wa kulaumiwa. Ukraine ni wa kuurumiwa tu, kuwa na jirani mkorofi kama Russia ni changamoto. Russia amegombana na majirani zake wengi.
NATO kuzuia ukraine kumshambulia ndani ya Russia ni ujinga. Yahani Russia wnaorganise majeshi na silaha kisha kuzileta mpakani wanaangaliwa tu, kisha wanavuka mpaka na kuanzia kuwaua ndo mnaanza kujibu?. Tena wakati mwengine Russia anawaua wa Ukraine bila kuvuka mpaka!.
Russia hairudi nyuma! Inaendelea na offensive kama kawaida.
 
Fact:
Kwani Russia akipiga Nuclear Ukraine, unadhani West watafanya nini? ,
Jibu ni hakuna watakachofanya zaidi ya makelele
 
Back
Top Bottom