Hasira yatawala Moscow baada ya NATO kuiruhusu Ukraine kushambulia ndani ya Russia kwa silaha za NATO

Kwa hiyo vita itakuwa fupi kwa Ukraine kushindwa kushambulia ndani ya Urusi?kichwani kuna contents gani?
 
unahis waliingia Ukraine mwaka wa pili huu ili kupiga selfie tu ?
Nadhani Urusi inatakiwa kuonyesha nguvu zake sasa Choma Ukraine kutoka Angle zote ikalie kabisa halafu tuanzie hapo mjadala
 
Huwezi kuitafuta amani ya Dunia kwa kumchokoza Dubu.
Amani ya kweli itspatikana kwa maridhiano
kwamba Russia alichokozwa kwa kushauliwa asivamie Ukraine ? au alichokozwa kwa kuchochea uasi ndan ya Ukraine , hii nchi haipigi hatua sababu watu mmekuwa wanafiki sana , KWEL mnafanya iwe uongo
 
Umeeleza vitu unavyovijua wewe mwenyewe. Wakati vita vinaanza Ukraine hakuwa na silaha zozote za maana zaidi ya silaha za zamani za USSR, ndio maana hata USA walimshauri Rais wa Ukraine akimbie ikihofiwa Kyiv ingetekwa ndani ya siku chache. Silaha nyingi kama HIMARS, vifaru, stingers, ndege vita etc vilikuja baada ya vita kuanza. Hivyo, hoja ya silaha na mamluki haina mashiko yoyote.
Tabia ya Urusi kuvamia majirani na kukwapua maeneo haijaanza leo, kwa mfano kuchukua Crimea tena kwa sababu za kijinga, ahakamia Georgia akachukua jimbo la Oceatia, na sasa akarudi Ukraine kuchukua eneo zaidi. Putin ni rais mjinga anayeamini anaweza kuirudisha USSR.
 
Sahihi kabisa. Alikuwa us au NATO?
Kabul pagumu, hata Russia aliwahi pakimbia.
Kama sijakosea umoja wa kisovieti walipakalia takribani, miaka 8 wakapakimbia
USA na washirika wake miaka 20 na wenyewe mbio
 
Jamaa una siyo tu mahaba na magharibi bali hayo ni mahabati maana ukisema NATO wanatumia akili kwenye vita sijui ni nani ambae hatumii akili kwenye vita, na kusema kuwa kuna 18 za kumuingiza Russia sijajua hiyo ni nchi gani itakayothubutu kuiweka hiyo 18 maana vikwazo maelfu havijafua dafu ndo iwe 18? Sasa subiri makombora yaingie urusi halafu tuone huko KIEV kitabaki kitu gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…