Hasira za Gen Z ya Kenya; Chanzo Chake ni Umaskini Uliotopea

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
Wengi wanaona Watanzania ni legelege au hawatambui haki zao ndiyo maana hawachukui hatua dhidi ya maamuzi ya wanasiasa. Wanatamani vijana wetu wangekuwa kama vijana wa Gen Z wa Kenya ambao kwa siku mbili wameteketeza mali zenye thamani ya mamilioni kwa hasira za financial bill 2024.

Matajiri wanne nchini Kenya, utajiri wao unazidi karibu nusu ya wakenya wote(40%) wakichanganywa kwa pamoja. Matajiri hao wana utajiri unaofikia Ksh. bilioni 333( Tsh. trilioni 6.26).

Utafiti unaonesha ukuaji wa tofauti kati ya walio nacho na wasio nacho ambapo wakenya 130 matajiri zaidi wanamiliki mali sawa na 70% bajeti ya Kenya kwa mwaka. Matajiri watano zaidi nchini Kenya ni Merali, Shah, Bedi, Kenyatta na Mahendra wakiwa na utajiri wa jumla ya dola za kimarekani 3.2.
Screenshot_20240627_104531_Chrome.jpg

Baada ya hapo ongeza na Manu Chandaria, Moi family, William Ruto & Associates

Wakenya wengi wanaishi chini ya dolla moja, pesa yao kuipata ni kazi. Karibu na Nairobi CBD kuna makazi ya slums 3 Kibera, Mathare na Makuru kwa Njenga ambazo zinaishi watu zaidi 2.5 Milioni.

Screenshot_20240625_194102_Google.jpg

Umaskini huu na tofauti ya kipato ndiyo unatia hasira kwa vijana mpaka hawafikiri mara 2 whether wachome bunge au magari ya Seikali.
Screenshot_20240625_194027_Google.jpg
 
Wengi wanaona Watanzania ni legelege au hawatambui haki zao ndiyo maana hawachukui hatua dhidi ya maamuzi ya wanasiasa. Wanatamani vijana wetu wangekuwa kama vijana wa Gen Z wa Kenya ambao kwa siku mbili wameteketeza mali zenye thamani ya mamilioni kwa hasira za financial bill 2024.

Matajiri wanne nchini Kenya, utajiri wao unazidi karibu nusu ya wakenya wote(40%) wakichanganywa kwa pamoja. Matajiri hao wana utajiri unaofikia Ksh. bilioni 333( Tsh. trilioni 6.26).

Utafiti unaonesha ukuaji wa tofauti kati ya walio nacho na wasio nacho ambapo wakenya 130 matajiri zaidi wanamiliki mali sawa na 70% bajeti ya Kenya kwa mwaka. Matajiri watano zaidi nchini Kenya ni Merali, Shah, Bedi, Kenyatta na Mahendra wakiwa na utajiri wa jumla ya dola za kimarekani 3.2.
View attachment 3027359

Baada ya hapo ongeza na Manu Chandaria, Moi family, William Ruto & Associates

Wakenya wengi wanaishi chini ya dolla moja, pesa yao kuipata ni kazi. Karibu na Nairobi CBD kuna makazi ya slums 3 Kibera, Mathare na Makuru kwa Njenga ambazo zinaishi watu zaidi 2.5 Milioni.

View attachment 3027353
Umaskini huu na tofauti ya kipato ndiyo unatia hasira kwa vijana mpaka hawafikiri mara 2 whether wachome bunge au magari ya Seikali.
View attachment 3027354
Kama ni umasikini Tanzania ndo ingekua ya kwanza kuandamana, wewe angalia wadamanaji vijana wameva vizuri hata kupita waalimu wa Tanzania,
 
Katika nchi maskini duniani LDC kwa Africa Mashariki, ni Kenya tu ndio haipo.
Kenya mpaka uwe na hali ya ahueni aisee lazima umepigika mno, Kenya kukuta vijana ni matajiri au viongozi wa ngazi za juu serikalini au kwenye organizations ni ngumu sana, Tanzania ukienda maeneo ya Iringa kule matajiri wengi sana ni vijana wadogo from early 20s wamepata pesa kwenye miti, avocado's etc

Ukienda kanda ya ziwa vijana wengi sana ni matajiri wamepata pesa kwenye madini, uvuvi, wtc

Ukienda kaskazini utakutana na vijana wengi wanamiliki expedition companies na tour operators wametajirika ni vijana wadogo yaani kila eneo Tanzania kuna fursa ya mtu yeyote kufamikiwa tofauti na monopolised Kenya, waliofanikiwa ndio wataendelea kufanikiwa na maskini wanazidi kua fukara.
 
Back
Top Bottom