Hata akinunaje ataongea tu...

Hata akinunaje ataongea tu...

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
Tulianza vibaya mwaka mpya na Ma msapu. Kisa kidogo tu nilimwambia sitoweza kumsaidia jambo ambalo yeye aliona ni muhimu nami nikasema sio kama vipi nipe muda.Alikasirika akaniambia hiyo ndio tabia yangu kwake na ananijua lakini ingekuwa mwingine ningempapatikia.

Haikunipendeza lakini nilipoonyesha sikufurahia nae akachukia. Tumenuniana toka Desemba,31,2012, nikimpigia simu hapokei, sms hajibu na nyumbani anatimiza majukumu yote kasoro salamu hanipi wala "kikapu" hatoi.

Baada ya kutafakari sana nikijaribu kutafuta tuongee roho wa Bwana kanijia kaniambia nimtumie sms nikiwa hapa ofisi nimweleze sijisikii vizuri. Hii itapima upendo wake kwangu katika kipindi cha hasira. Nilipotuma ikapita dakika tano kanirejeshea ujembe: "vipi tena jamani?!", nikajibu " siwezi, nashindwa hata kuendesha gari". Ghafla akapiga "ehe wee, baba vipi tena jamanii.mungu wangu, nije nikusaidie?!"

Nikazuga nimemwomba jamaa yangu mmoja ofisi anisaidie,.. Naelekea nyumbani, sasa tunaweza kuwasiliana tena kwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu (sms), anauliza naendeleaje, najisikiaje, nikifika nitamweleza nilikosa mbinu ya kurejesha mawasiliano hilo lilinilazimu kuongopa naumwa!

Raha ya maisha ya ndoa ni kama hivi, mwenzio hata akinunaje itafika wakati ataongea tu kama sio roho yake na kinywa, basi kiungo cha mwili kilichowaunganisha kitamlazimisha kuongea tu..... Huwezi kuzuia kiungo kikidhamiria kutumika, ataonge kwa kinywa au matendo mtawasiliana tu!! Upendo wa kweli katika ndoa hujidhihirisha katika matukio, mwenzio uumia sana juu yako, mke au mume wa kweli hawezi kuvumilia akisikia mwenzie kapatwa na jambo baya, anaumwa, amekosa raha, ametukanwa, anasemwa vibaya nk...mke/mume wa ukweli yu radhi kusimama hata katikati ya nduguze ili kumtetea mwenzie, yu tayari kuonekana hafai kwa maslahi ya mwenzie..

Yu tayari kufia ndoa yake, kudhalilika hata akiitwa "Bw.e.ge" yu radhi!
 
Mkeo ana anakupenda ila alitaka kukujulisha kuwa ulimuudhi katika suala fulani.
TWASOMA:


"Waume, endeleeni kuwapenda wake zenu, kama vile Kristo pia alivyolipenda kutaniko na kujitoa mwenyewe kwa ajili yake…Vivyo hivyo, waume wanapaswa kuwa wakiwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Yeye anayempenda mke wake anajipenda mwenyewe, kwa maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake kwa vyovyote; bali huulisha na kuutunza kwa upendo, kama vile Kristo pia anavyolitendea kutaniko."-Waefeso 5:23, 25-29.

"Endeleeni kuwapenda wake zenu nanyi msiwakasirikie kwa uchungu." (Wakolosai 3:19)

Waefeso 5:33
[SUP]33[/SUP] Hata hivyo, pia, kila mtu mmoja-mmoja kati yenu na ampende hivyo mke wake kama vile anavyojipenda mwenyewe; kwa upande mwingine, mke anapaswa kumheshimu sana mume wake.


Tito 2:4-5
[SUP]4[/SUP] ili kuziamsha akili za wanawake vijana wawapende waume zao, wawapende watoto wao, [SUP]5[/SUP] wawe na utimamu wa akili, safi kiadili, wafanyakazi nyumbani, wema, wakijitiisha kwa waume zao wenyewe, ili neno la Mungu lisitukanwe.



 
Haaaahaaaahaaaaaaaa! Hadi wewe mkuu? Nilikuwa nakuheshimu sana kumbe ndo walewale kina mzabzab, by the way, umenichekesha sana. LOL!
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Mimi nafagilia mambo ya ndoa, na sio mgegedano tu usio barikiwa. So please usiache kuniheshimu.
 
Mkuu tunaomba uje utupe feedback kama 'chakula chako mwenye nyumba cha usiku' kakupa!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kununa si kuzuri kabisa kunawakosesha wana ndoa wote amani na hata kama huwa mnanuniana kuna matukio ambayo lazima kununa kusahauliwe ili kuyashughulikia matuki hayo kama hili la kuumwa. Hongera kwa kuweza kupambana na mnuno ndani ya nyumba kivyako vyako.

 
Last edited by a moderator:
dah hiyo idea nzuri je wewe ukimnunia mkeo itakuwa vp hebu funguka
Unajua pengine maisha ya Ndoa ni kama tamthilia isiyo kwisha...kila kukicha ina Episode yake. Unaweza kujihisi moyoni umtendei mwenzo haki kwa kumnunia tu iwe kwa sababu au bila sababu. Wakati fulani mnaweza kuwa katika ugomvi mkubwa sana kiasi kwamba ukajuta kwa nini ulioa au kuoelewa na huyu jamaa..inakuwa wewe ukiwa sebuleni, yeye yupo chumbani, ukiwa chumbani yeye yupo jikoni, ukiwa kwenye meza ya vipodozi (dressing table) yeye yupo kwenye Sink la kunawia uso. mnapishana kwa ubavu pasi kuangaliana usoni. Lakini unapohitaji, unaweza kusimsemeshe, ukajipeleka karibu yake, ukamsogeleze "kile kilichowaunganishwa" kama ana hasira kasi atakutoa lakini ukifanya mara mbili tatu utaona ametulia, badae utamsikia akigugumia (umegusa). Mkimalizana anaweza kuanza kuongea (ugomvi umesiha) au kama vipi ataendelea na hasira zake .....HIYO NDIO NDOA..

Mimi huwa nanuna lakini mara zote haichukui muda kwa kuepusha kuvuruga afya ya mwili na ndoa yangu...nikiona siwezi kuhimili ugomvi najitoa kuelekea kwenye shughuli za kijamii na pengine kupata "kitu" kidogo , huko nakuwa nimepunguza hasira kwa kiasi kikubwa.,.nikirejea namwomba mamsapu tumalizane tu kwani yanaathari...
 
Mkuu tunaomba uje utupe feedback kama 'chakula chako mwenye nyumba cha usiku' kakupa!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Nimepata mkuu bila shida...nimemweleza kuwa nilihsindwa kuvumulia ugomvi, umeninyima haki yangu tokea tarehe 31.12..nilimwaomba tufungue ukurasa mpya.
 
Hahahaa basi hii tekniki tunaitumia wengi wetu kumbe maana juzi kati nilichelewa kurudi kidogo (yaani saa mbili natakiwa home kitambo tu) basi zikaanza kutumwa sms za maudhi na mimi nikajibu hivyo hivyo, baadae nikakaa kimya, kufika naona mmh hapa hamna amani kabisa hapa, basi nikapitiliza hadi chumbani, nikavua nguo nikajifanya nataka niingie kuoga (kuna choo chumbani) nikajifunga taulo mara nikamuita kwa sauti , hajaitikia wala hajaja nikatoka na taulo hadi Jikoni nikamwambia "yaani mi naumwa nimeanguka chooni huko nakuita halafu umekaa kimya" halafu nikaondoka zangu nikarudi rum mara huyoo anakuja, oooh sikuskia, jamani, tatizo nini? blah blah kibao, moyoni nacheka tu, pale pale nikajilza magotini alikua amekaa kitandani...nikautumia huo muda kuganga yajayo.......................
 
Mwenye kukupenda hangojei mpaa unaumwa ndo akujali!

Mapenzi hayapimwi wakati wa shida tu.

Siku njema, tunakuombea maisha mazuri we na mke wako.
 
Tulianza vibaya mwaka mpya na Ma msapu. Kisa kidogo tu nilimwambia sitoweza kumsaidia jambo ambalo yeye aliona ni muhimu nami nikasema sio kama vipi nipe muda.Alikasirika akaniambia hiyo ndio tabia yangu kwake na ananijua lakini ingekuwa mwingine ningempapatikia. Haikunipendeza lakini nilipoonyesha sikufurahia nae akachukia. Tumenuniana toka Desemba,31,2012, nikimpigia simu hapokei, sms hajibu na nyumbani anatimiza

Yu tayari kufia ndoa yake, kudhalilika hata akiitwa "Bw.e.ge" yu radhi!

Hapo ndo nimempendea,afu kapu hawezi toa automaticaly kama kaudhika!safi lakini mbinu yako
 
Back
Top Bottom