battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,712
- 2,577
Maneno yako swafi na ukweli mtupu.Wanajamvi,
Kama heading ya uzi huu inavyojieleza, ni kwamba hakuna haja ya upinzani ku panic! Hayo ni ya wana ccm na kamwe siyo upinzani. Wao Kwani wamezuiwa siasa? Wamekuwa wakifanya kampeni toka awamu hii iingie madarakani, sasa wananchi kama ni kuona na kusikia, wameshasikia na kuona vya kutosha. Ni wazi sauti nyingine zikija watakuwa na shauku kubwa. Hiyo ni kawaida kwa hulka ya mwanadamu. Ni kiumbe mwenye kutafuta habari kila uchao!
Sasa nimeona watu wanasumbuka sana kuhusiana na suala la nani atakuwa mgombea kwa upande wa upinzani. Vyama vya ACT-Wazalendo na CHADEMA vikizungumziwa na kuhusishwa na wagombea wawili, yani Tundu Antipas Lissu, sambamba na Bernard Membe ambaye inasemekana yumo ACT-Wazalendo.
Tathimini rahisi, inaonyesha wazi kabisa kuwa ACT-Wazalendo, ni chama mbadala cha CUF. Na ndiyo kinategemewa kumsimamisha mgombea kule Zanzibar, kama sikosei, ni Maalim Seif. Kwahiyo kwa upande huo wa kushirikiana inapokuja kwa upande wa Zanzibar, ni kawaida tu.
Na kwa upande wa bara, mambo yalikuwa ni kati ya Lipumba, na mgombea wa CHADEMA, ambapo CHADEMA walikuwa ndo wanaotoa mgombea wa urais kwa upande wa bara.
Lakini tofauti iliyoko kwa sasa, ni Bernard Membe. Huyu yeye ndiye anayeleta mjadala mkali, na mjadala ambao unachochewa sana na wana ccm, kwasababu wao wameshamaliza upande wao na watu kuzimwa hata nafasi ya kuchukuwa fomu za kugombea kwenye nafasi ya urais. Na ndiyo matokeo yake Bernard Membe kujitoa. Huyu tayari ana watu wengi tu ndani ya ccm wanaoona ameonewa na ccm. Jambo lilokuwa ni kinyume hata na katiba ya chama.
Kwa maoni yangu, hata kama vyama hivi vikiamuwa kuwasimamisha wagombea wao, bado idadi ya kura watakazozipata, zitawazidi ccm. Huu ni ukweli mchungu kwa ccm na ndiyo maana wanahaha sana kuleta mijadala ya kuwachanganya na kutaka kuleta migawanyiko! Lakini hili halitafanya kazi.
Kule Kenya, hili liliwahi kutokea pia, na ndipo hapo chama cha KANU kilipoanguka chali! Kama sikosei, mara ya pili ilibidi wafanye muungano, kwasababu kura zao zote, zliwashinda KANU, lakini wao walikuwa hawajaungana, na hivyo KANU kubakia madarakani.
Kwa upande wa Tanzania, siasa zetu ni za tofauti kidogo na zile za Taifa la Kenya. Sisi kwanza siasa za ukabila siyo kivile! Pamoja na kwamba ccm wamejitahidi sana kuzitumia. Lakini hazijafanikiwa, na ndiyo maana upinzani ulipata nguvu sana hadi ccm kutishika! Na hata wengine wakisema uchaguzi uliopita, kama siyo kwa “goli la mkono”, ambalo Nape, January pamoja na Kinana, walifanya kazi ya ziada!
Sasa miaka mitano ndo hiyo imeshakata, Kinana ni juzi tu kaomba msamaha, ni baada ya Nape na January kufanya hivyo! Lakini nao walifanya kwa shingo upande, kwasababu nguvu za mwenyekiti ni kubwa mnoo! Hao nao sura zao halisi zingeonekana kama wengine wangeruhusiwa kuchukuwa fomu ya kugombea urais ndani ya ccm. Hata mzee Makamba naye ni hivyo hivyo tu. Mzee Mkapa naye alizungumzia umuhimu wa kuwa na tume huru ya uchaguzi nchini!
Kura za ccm ndizo zitakazogawanywa, cha msingi, kuwepo na makubaliano baina yao mapema iwezekanavyo, ninaamini uchaguzi huu utatuletea viongozi wanaowakilisha kada zote za wananchi pamoja na masilahi yao ya moja kwa moja jamii, na pia kama watanzania. Hili amelizungumzia vyema sana Sheick Ponda kwenye ule waraka wa Shura ya Maimamu, ambapo walizungumzia kuhusu upatikanaji wa katiba mpya baada ya uchaguzi.
Hapa ina maana kwamba kuna mengi yanayowaunganisha watanzania dhidi ya ccm kuliko yale yanayowatenganisha! Hayo ni machache sana ambayo siyo lazima kupewa kipaumbele! Maana yenyewe ni ya kuwagawanya wapinzani ili kuwadhibiti! Yani “devide and rule”. Kwetu ni tofauti kabisa na kule Kenya ambapo siasa za ukabila ndizo zinawaumbuwa. “Coalitions”, ama miungano yao, ni ya misingi ya kikabila. Na Kwahiyo tuna nafasi nzuri zaidi kwa wapinzani kuiangusha ccm, na bado tukapata serikali itakayowatumikia wananchi vyema, na kwa mujibu wa katiba ya nchi! Na hao wakifanya uzembe, tuwe na nafasi na uwezo wa kuwandoa madarakani kwa sanduku la kura!
Siyo siri, chama cha CUF, kilikuwa na wanachama wengi wa maeneo ya mwambao wa Pwani! Na hivyo wengi kuwa waislam. Majimbo mengi ya waislam, ni hao CUF waliyabeba, lakini mengine ni ccm. Hata hivyo, kama nilivyosema hapo awali, ACT-Wazalendo ndiyo ambao sasa wameichukuwa nafasi hiyo ya chama cha CUF. “It has simply been replaced”, haswa baada ya Maalim Seif kuondoka huko, na Zitto kuitumia nafasi hiyo kumsajili.
Sasa endapo ACT-Wazalendo watamsimamisha Membe, nadhani siyo mbaya hata kidogo kwa upande wa CHADEMA na upinzani kwa ujumla!Kwanza kuna malalamiko mengi sana ya uwepo wa udini. Malalamiko ambayo yanaelekezwa kwa utawa wa ccm! Na wala siyo mara ya kwanza! Na ndiyo maana hata CUF ilipata nguvu sana! Malalamiko yao hayajaanza leo chini ya utawala wa ccm! Hawa watu sauti zao lazima zitakuwa zinataka mwakilishi. Hata waislam wale ambao walikuwa hawaipigii CUF kura, na wakawa wanaipigia ccm, basi sasa wataipigia kura ACT-Wazalendo.
Hata wale ccm wasioipenda CHADEMA, wataipigia kura ACT-Wazalendo. Maana tunafahamu propaganda za ccm inapokuja kwenye udini na ukabila! Tuhuma zao wenyewe, lakini wamekuwa wakiwasingizia upinzani. Sasa ccm mmetawala toka uhuru, upinzani ndo umeleta shida za waislam toka lini? Hili huwa najiuliza sana wakati ccm inapokuja na mgombea wao huku wakitutajia maendeleo waliyoyaleta, na kujifananisha na upinzani ambao hawajawahi kuongoza nchi. Hili lenyewe, lilitakiwa liwe sababu nzuri kabisa ya kuwa na uchaguzi huru! Maana nani mwingine ambaye ameshafanya “mazuri” zaidi yao tokea December 31st 1961?
Hivyo ni kweli kabisa kuwa uchaguzi wa huru na haki, utawaondoa ccm madarakani, upinzani uungane, ama usiungane, moto ni ule ule! Membe atakula vichwa vya ccm, chadema nao watakula vichwa vya ccm. Hata yule Sipunda anaweza kula vichwa!
Cha msingi, ni makubaliano yafanyike mapema! Makubaliano ambayo yatahusisha nia ya dhati kabisa ya pande zote mbili! Ni za kuwa na tume huru ya uchaguzi pamoja na katiba mpya ya wananchi kutoka kwa wananchi! Na siyo hii ya mkoloni yenye viraka vya ccm ambayo inaendelea kutushikia chini kiasi cha kwamba uhuru wetu ukawa mashakani!
Sababu ziko nyingi sana, ila nimeamuwa kuanzia na hizi!
Nguruvi3
Lakini Mwaka huu hakuna huo uchaguzi,
Inavyo onesha ni kata Buti tangaza matokeo ya mfukoni,
Zuia mikutano ya siasa, hakuna kampeni wala kuteua wagombea,
Siku ya kurudisha fomu ofisi mutakuta zimefungwa ili CCM wabaki wawe wagombea pekee,
Ikishindikana hivyo matokeo yatapinduliwa na katu Hakuna Mpinzani atakaye tangaazwa
Kwa mujibu wa Mwendelezo wa chaguzi zilizotangulia chini ya utawala wa Jiwe, naona Mbele Kiza kitupu.