Uchaguzi 2020 Hata CHADEMA wasiposhirikiana na ACT-Wazalendo, bado CCM itapigwa chini. Membe na Lissu “watakula vichwa vingi” vya wanachama wa CCM

Maneno yako swafi na ukweli mtupu.
Lakini Mwaka huu hakuna huo uchaguzi,
Inavyo onesha ni kata Buti tangaza matokeo ya mfukoni,
Zuia mikutano ya siasa, hakuna kampeni wala kuteua wagombea,
Siku ya kurudisha fomu ofisi mutakuta zimefungwa ili CCM wabaki wawe wagombea pekee,
Ikishindikana hivyo matokeo yatapinduliwa na katu Hakuna Mpinzani atakaye tangaazwa
Kwa mujibu wa Mwendelezo wa chaguzi zilizotangulia chini ya utawala wa Jiwe, naona Mbele Kiza kitupu.
 
Mkuu punguza kuwa na Lucid dreams.

Jaribu kukubali uhalisia wa mambo
 
Kabisa yaan humu anayeongeaga uhalisia ni tindo
 
Bro sisiem haijawahi kushinda, Hilo linafahamika!
Tusitegemee sanduku la kura maana mwisho wa siku mambo Ni Yale Yale ya miaka yote.
Nape alishatuambia kuhusu bao la mkono, jiwe akaenda mbali kuwatahadharisha wakurugenzi wasithubutu kumtangaza mpinzani kashinda, wataisoma namba. Bashiru alishatueleza kuwa wanatumia dola kubaki madarakani na sio sanduku la kura.

Sasa kwanini tusipange mipango thabiti na iwe coordinated bongo yote Ni namna gani ya kuwaondoa madarakani pale watakapogoma kukabidhi majimbo na nchi baada ya maamuzi ya Watanzania kwenye sanduku la kura?
 
CCM watashinda kirahisi na mapema uchaguzi huu.cdm hamtapata wabunge zaidi ya watatu tu tena kwa mbinde.
 
Halafu nimegundua wengi ni watoto sana humu, hata hawaelewi kwamba tume siyo huru
Samahan bro, tume ili iwe huru unadhan iwe na muundo gan labda na watendaj pamoja na fund vipatikane vp? samahan sana bro.
 
Pitia ule waraka wa “Shura ya Maimamu”, mbona hilo limezungumziwa? Au kwasababu wengi wetu tumelishwa sumu za udini na ccm?

Kwa taarifa yako, mule amesema kabisa ni vigumu kupata tume mpya huru kabla ya uchaguzi, lakini kuna mabadiliko muhimu yanayoweza kufanyika na yakaleta unafuu kidogo. Mengine umma utaamuwa.
 
Pitia waraka wa Shura ya Maimamu iliyotolewa na Sheick Ponda. Halafu uone kama hakuna mambo muhimu ya kusapoti yenye manufaa kwa watanzania wote.
 
Kuna dalili za watu kuwa akili zimeyumba. Baada ya kuona upinzani hauna mwelekeo.
Si munahangaika na upinzani kwasababu huko kwenu hamna sauti? Wewe unadhani ni kitu gani kinachokufanya ufikie mwafaka huo?
 
Kwa zanzibar yes, ila kwa bara tena kwa nafasi ya uraisi haijalishi atasimama nani ukweli ni kwamba magufuli atashinda mchana kweupe.
 
Jiwe hakubaliki hata na wanaccm wenzie ,ila amejitahidi kupanga sanaa kwenye vikao hatari.
 
Kwa zanzibar yes, ila kwa bara tena kwa nafasi ya uraisi haijalishi atasimama nani ukweli ni kwamba magufuli atashinda mchana kweupe.
Siyo kweli. Kwanza kura nyingi za waislam zitaenda ACT-Wazalendo, plus zile za wana ccm waliokuwa wavivu kuingia CUF!

Pia kura nyingi za vijana na wazee zitaenda CHADEMA. Wengi ni uoga na kwasababu ya maslahi ya tumbo ndo maana.
 
Jiwe hakubaliki hata na wanaccm wenzie ,ila amejitahidi kupanga sanaa kwenye vikao hatari.
Toka ameingia tu madarakani, alijipanga sana ili kuweza kuondoa sauti zozote zenye kuuliza ama kupinga lolote. Alianzia ndani ya chama. Hata Makonda mwenyewe ana nguvu sana. Yule katibu mkuu wa ccm ni mpiga nduru tu.
 
Siyo kweli. Kwanza kura nyingi za waislam zitaenda ACT-Wazalendo, plus zile za wana ccm waliokuwa wavivu kuingia CUF!

Pia kura nyingi za vijana na wazee zitaenda CHADEMA. Wengi ni uoga na kwasababu ya maslahi ya tumbo ndo maana.
Magufuli atashinda mchana kweupe na mwendoutakuwa ule ule kuwa kaiba kura. Hizi mambo za JF na mtandaoni zinafanya watu wahisi labda wana wafuasi wengi ila huko vijijini huko wakina mama wauza misosi na biashara ndogo wanamkubari. Labda ubunge lakini uraisi atashinda tena kwa kiasi kikubwa
 
“Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Kamati Kuu ya Siasa ya Shura ya Maimamu pia ilitoa Waraka na hatimaye tathmini. Sehemu ya tathmini mwaka huo inasema:

“Katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, watu wengi waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura hawakuona majina yao kwenye orodha za wapiga kura zilipobandikwa vituoni. Tatizo hilo liliendelea mpaka siku ya kupiga kura ambapo wananchi hao hawakupata haki ya kuchagua viongozi wa nchi."

Baadhi ya vyombo vya habari viliandika kilio cha Wananchi hao kama ifuatavyo:

“Wengi walilalamika kuyakuta majina yao nje lakini walipoingia ndani hawakuyaona katika orodha ya daftari la wapiga kura”.

Chombo kingine cha Habari kiliandika:
_
“Karibu maeneo yote, vifaa vya kupigia kura vilikuwepo lakini lililojitokeza ni mkanganyiko wa majina ya wapiga kura. Baadhi ya majina yalihamishwa kutoka sehemu walizojiandikisha na kupelekwa vituo vingine. Hali kama hiyo ilijitokeza eneo la Mpanda, Arusha ambako watu zaidi ya 100, walihangaika kutafuta majina yao na walipoyapata muda wa kupiga kura ukawa umekwisha. Polisi wa kutuliza ghasia FFU, walitumia nguvu kuwafukuza ilihali wao wakiwa wanabembeleza waweze kupiga kura”_

Tathmini hizi za Waislamu (ambazo hupatikana kutokana na waangalizi wake katika uchaguzi), huwa na mchango mkubwa katika kutambulisha mambo muhimu yaliyojitokeza wakati wa chaguzi hizo).

Tukiingia katika usuli wa kichwa cha mada hii “Umuhimu wa kuboresha Kanuni Kipindi cha Mpito” pamoja na kutokuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi Serikali imesema uchaguzi Oktoba 2020, utafanyika. Na wale watakaotangazwa na Tume za Taifa za Uchaguzi (NEC na ZEC) watapewa mamlaka ya kuongoza Taifa. Kwa Watanzania wanaotaka Tume Huru ya Uchaguzi, Uchaguzi huu kwao ni tukio la kipindi cha mpito katika vuguvugu la madai ya Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. (Waislamu ni miongoni mwa tabaka hilo). (Hata Serikali yenyewe pia imekuwa ikidai kuwa suala hilo ni muhimu kwa sasa lakini tatizo kwao ni fedha).

Katika muktadha huo wito wetu ni kuboreshwa Kanuni za Uchaguzi na Uendeshaji wa zoezi la Uchaguzi ili kuwezesha kufanyika Uchaguzi Huru na wa Haki. Mamlaka za Uchaguzi Tanzania Bara na Visiwani NEC na ZEC zione dharua iliyopo ziitishe mabaraza (au au au) ya kutunga Kanuni za Uchaguzi. Katika hatuwa hiyo muhimu Serikali zishirikishe makundi muhimu vikiwemo vyama vya Siasa. Huo pia ni wito wa Watanzania mbali mbali wamekuwa wakipendekeza maboresho (shirikishi) ya kanuni katika kipindi hiki cha mpito. Miongoni mwa maboresho tunayoyaunga mkono na kupendekeza ni:

1) Kanuni ya Uchaguzi itamke wazi vyama vya Siasa vitapewa nakala ya Daftari la Wapiga kura mapema kabla ya kampeni kuanza.

2) Kanuni itamke na kuweka msisitizo wa hatuwa za kisheria kuwa viongozi wa Serikali kama Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Watumishi wa Umma wasitumike kisiasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

3) Kanuni itamke Mashirika na Taasisi za Umma hwairuhusiwi kufanya kampeni ya mgombea yoyote au chama chochote cha siasa.

4) Aidha kanuni ya zamani ilikuwa inaagiza Wakala wa chama apewe nakala yake ya kiapo mara tu baada ya kuapishwa. Upo mchakato batili unaolenga mabadiliko ya kanuni hiyo ili itamke; atapewa nakala yake siku ya kupiga kura nje ya kituo. Kwakuwa nakala hii ndio tiketi ya wakala ya kuingia ndani ya chumba cha kupigia kura, kanuni itamke wazi kuwa wakala wa chama cha siasa atapewa nakala yake ya kioapo mara tu baada ya kuapishwa.

5) Kanuni itamke Kura zitapigwa na kuhesabiwe katika kituo husika cha kupigia kura. Itamke wazi baada ya kuhesabiwa hazitahamishwa katika kituo hicho na kupelekwa katika kituo kingine chochote kwaajili ya kuhesabiwa upya.

6) Kanuni itamke Mawakala wapewe nakala za Matokeo ya kura katika vituo vyao bila kubabaishwa wala kutishwa.

7) Kanuni itamke Matokeo ya wagombea yatangazwe pale pale katika kituo cha kupigia kura.

8) Kanuni itamke idhini ya Asasi za Ndani na nje kuweka Waangalizi wa uchaguzi na uhuru wa kutoa ripoti zao.

9) Kanuni itamke Vyombo vya dola kama vile Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haviruhusiwi kuingilia mambo ya uchaguzi. Itamke kuwa askari waliovaa sare na kubeba silaha watakaa mita miamoja kutoka kituo cha kupigia kura.

10) Kanuni iwakumbushe Majaji na Mahakimu pamoja na Maofisa wengine wa Mahakama wajibu wa kutenda haki kwa Mashauri yote ya uchaguzi.

Mapendekezo hayo yatapunguza kwa kiasi kikubwa ombwe la kukosekana Tume Huru ya Uchaguzi na yanaleta matumaini ya Uchaguzi Huru na wa Haki katika kipindi hiki cha mpito cha madai ya Wananchi ya Tume Huru (Independent Electrol Commission)”- Waraka wa Shura ya Maimamu
 
Kwahiyo unampinga?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…