Uchaguzi 2020 Hata CHADEMA wasiposhirikiana na ACT-Wazalendo, bado CCM itapigwa chini. Membe na Lissu “watakula vichwa vingi” vya wanachama wa CCM

Maccm walianza kuimba wimbo wa mapambio mapema kiasi kwamba wananchi wamechoka mistari yao.
Na hawana tena ujanja wa kutunga mistari mipya.
 
Nakubaliana na wewe 100% , Lakini Maswali yangu ni haya:
1. Katika chaguzi ndogo zilizopita tumeona wapinzani wakikamatwa wakati wa kurudisha fomu, uchaguzi huu nini kimebadilika?
2. Tumeona mkurugenzi/ watendaji kata wakijificha ili wasipokee fomu za wapinzani kwa sasa nini kimebadilika
3. Tumeona kamata kamata imeanza wapinzani wanapofanya vikao hata vya ndani, Octoba nini kitahakikisha haya hayatokei
4. Chaguzi ndogo tumeona wapinzani wakiporwa fomu na kutokimea kusikojulikana je hili limepata tuba?
5. Chaguzi ndogo tumeona aliyeshinda mwingine na anayetangazwa ni wa CCM mbele ya polisi, uchaguzi huu nini kimebadilika
6. Tumeona wapinzani wakishinda mkurugenzi huufuta uchaguzi, nini kitabadilika
7. Mahakama zimekuwa zikitupilia mbali madai ya wapinzani yanayohusiana na uchaguzi au kuvuliwa ubunge, je huko mbele itakuwaje
8. Tumeona msajili wa vyama mara nyingi akitamani kuifuta CHADEMA kwa hisia za kufikirika je kwa sasa amebadilika?
9. Tumeona tume ya uchaguzi ikionywa isiwatangaze wapinzani ushindi, je kauli hii iliwahi kukanushwa na tume ya uchaguzi
Na mengine mengi. NAONA GIZA.
 
Mwenzio kakwambia hamuwezi kutangazwa washindi kwa tume hii, wewe umekuja na matusi! Haya twanbie nyie wapinzani mtatangazwa washindi na tume hii?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
Kwani yeye kuniambia hivyo ina maana kuwa anakubaliana na maoni ya Shura ya Maimamu?
 
Pitia waraka wa “Shura ya maimamu”, maswali mengi yamejibiwa tu. Mfano kuhusu wakurugenzi, waraka unatamka wazi kuhusu watumishi wa umma kutokutumika kisiasa pamoja na mambo mengine.
 
Porojo nyingi kujaribu kufunika frustrations.

Wajiandae kuikabidhi kijiti ACT. Zito moyoni atakuwa anayacheka sana yalivyomtengenezea zengwe na kumfukuza.
Hivi unadhani ni wana ccm wote ambao hawana huruma? Na kwamba hawamuonei huruma mtanzania mwenzao aliyeponea kuuwawa? You’re banking on the devil’s side to be honest.
 
Hivi unadhani ni wana ccm wote ambao hawana huruma? Na kwamba hawamuonei huruma mtanzania mwenzao aliyeponea kuuwawa? You’re banking on the devil’s side to be honest.

Sijakupata vizuri; wewe unawafahamu waliotaka kumuua lisu?

Kuna wana-ccm wengi (mimi si mmoja wao) wanaoamini kuwa ile ilipangwa na wanachadema wenzake, hujawahi kuisikia hiyo?
 
Sijakupata vizuri; wewe unawafahamu waliotaka kumuua lisu?

Kuna wana-ccm wengi (mimi si mmoja wao) wanaoamini kuwa ile ilipangwa na wanachadema wenzake, hujawahi kuisikia hiyo?
Hao wanaoamini hivyo, either ni vichaa, au wameamuwa kujitoa ufahamu, ama ndo wahusika wenyewe wanaotoa propaganda za kufunika na/ama kujaribu kuwachanganya wananchi akili.
 

Wewe ndiye MPUMBAVU kwa kuwachagulia waZanzibari mgombea urais Mzaramo ni nani alikwambia Zanzibar wanataka rais mzaramo? kama siyo upumbavu wako ni kwanini mlimchagua mgombea urais bara huku mkilia utadhani mpo msibani au mpo ndani ya dhoruba ya meli ya Titanic?

Sasa baada ya kufuta machozi unakuja kutuvimbia huku utadhani chura mabaka umejikaza utadhani unakata GOGO na kwa taarifa yako kule dodoma hata ukuta mngeshikishwa, mmetoka kule macho yamelegea ooh tumemchagua kwa kura %100 kumbe mnajitekenya na kucheka.
 
Hujakosea mkuu, hata Yanga alikuwa na Imani kubwa ya kumpiga Simba mechi ya jana! niishie hapo.
 
hahahahaa! hata wewe? kila siku unaongelea tume, tayari unabariki kitu kama hiki mkuu, haya bhana!
Haya maneno nimeyasikia yanazungumzwa sana mtaani na maofisini na watu makini. Lakini nimejaribu kuunganisha dots nimeshindwa kupata maana, jee ni nini kinategemewa na wengi kutokea kabla ya uchaguzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…