Uchaguzi 2020 Hata CHADEMA wasiposhirikiana na ACT-Wazalendo, bado CCM itapigwa chini. Membe na Lissu “watakula vichwa vingi” vya wanachama wa CCM

Good analysis
 
save uzi wako mkuu, utaufufua october na usisubir hadi tuufufue!
 
hahahahaa! hata wewe? kila siku unaongelea tume, tayari unabariki kitu kama hiki mkuu, haya bhana!
Kwani mimi nimesema sitaki tume? Umesoma vyema post ya kwanza na ukaielewa?
 
save uzi wako mkuu, utaufufua october na usisubir hadi tuufufue!
Kama yote yatatokea, mfano wote kuingia kwenye uchaguzi ambao umezingatia maoni ya marekebisho yanayotolewa na wadau mbali mbali, kwenye kipindi cha mpito, kuelekea kwenye katiba mpya, basi tukutane hapa hata hiyo October. Kwani shida iko wapi?
 
Amechanganyikiwa huyo na ku panic. Nadhani bado, ajiandae zaidi. Ndiyo shida ya kuzuia siasa! Maccm yamekuwa kama mavifaranga ya kuku wa kisasa wale “broilers”. Hawajui shida ya kupingwa na sasa wamepanic, maana ile ni “privileged”, na ni kinyume cha katiba. Yani yamedekezwa, yakadekezeka, maana yanataka mfumo wa chama kimoja.
 
Kwa uchafu uliofanywa na awamu ya 5 hata Hashimu Rungwe wa CHAUMA inaweza kumgaragaza mzee wa chato asubuhi tu sembuse chama kubwa kama CHADEMA?
Uko sahihi kabisa! Haswa kwenye usanii wa ccm! Mfano hapo chini, ni mojawapo ya mapendekezo 20 ya kamati maalum ya uchunguzi wa masuala ya kisheria na uchumi /madini, iliyoongozwa na Osoro! Sasa niambie nani kawajibika?

“Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria, dhidi ya waliokua mawaziri,wanasheria wakuu wa serikali na manaibu wao, wakurugenzi wa idara za mikataba na makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya madini na watumishi wengine wote waliohusika katika kuingia mikataba ya madini.“
 
Sababu ziko nyingi sana, ila nimeamuwa kuanzia na hizi!
Endelea kuota,mwisho utasingizia tume
Hakuna mtu mwenye uwezo mzuri wa kufikiri akampa kura Tundu Lissu huku akijua fika kwamba anapoteza kura yake
 
Endelea kuota,mwisho utasingizia tume
Hakuna mtu mwenye uwezo mzuri wa kufikiri akampa kura Tundu Lissu huku akijua fika kwamba anapoteza kura yake
Kubalini mapendekezo ya wananchi kuhusu uchaguzi mkuu ujao. Kwanini mumemkamata Ponda?
 
Haya yaliishasemwa sana, lakini wapigania madaraka na utawala (CCM) ndio kwwnza wamezidisha uliko huko nyuma. Na Bashiru keshasema watarumia nguvu ya dola kubski madarakani. Hakuna alietia neno hata NEC.
GIZA LINAZIDI.
Pitia waraka wa “Shura ya maimamu”, maswali mengi yamejibiwa tu. Mfano kuhusu wakurugenzi, waraka unatamka wazi kuhusu watumishi wa umma kutokutumika kisiasa pamoja na mambo mengine.
 
Haya yaliishasemwa sana, lakini wapigania madaraka na utawala (CCM) ndio kwwnza wamezidisha uliko huko nyuma. Na Bashiru keshasema watarumia nguvu ya dola kubski madarakani. Hakuna alietia neno hata NEC.
GIZA LINAZIDI.
Wanataka kutumia udini kwa kumtaja Ponda bila ya kujali maoni yaliyomo ndani.
 
Umemjibu vema...japo kasema ukweli ila kashindwa kuongea kistaarabu
Ustaarabu na hawa watu wa ccm ni vitu mbali mbali! Wenyewe wamezoea kulindwa na system. Polisi wenyewe walishaambiwa “wasiguse kijani”. Sasa wanataka kutuletea huo ujinga wao hadi humu. Hawataki maswali.
 
Mkuu Nguruvi3 , ninasubiri maoni yako. Halafu nini kimemfika JokaKuu? Kwa mujibu wa BAK , hajaonekana humu kutokea mwezi wa tatu!Una taarifa zozote?
Mkuu nilikaa kimya kuhusu haya mambo, naona umeamua 'kunichokoza''
Mkuu, kwanza, sina taarifa za Joka na ni muda sasa sijamuona jamvini, natumai yu bukheri aliko.

Pili, nianze na Zanzibar. Kama kuna fyongo iliyochezwa na CCM ni hii ya Hussein. Huyu bwana hakubaliki na kwamba aligombea ''nyumbani'' mkurunga kunamuondolea sifa ya ''uzanzibar'' hata kwa wana CCM a.k.a mapinduzi daima

Hii ilikuwa fursa ya Shamsa Vuai, lakini kamati maalumu Znz ilichezewa akili kwa kuaminishwa ni Mbarawa.
Hussein akaiangizwa katika kundi la Shamsi, Khalidi akisindikiza bila kujua huku bara ilikuwa Bw Hussein.

Kura za CCM 35 kutoka Znz zilikwenda kwa machaguo yao, huku mwana mpendwa akikomba 129 za Bara

Hili limepeleka ganzi visiwani, kwamba, CCM hawana uthubutu wa kunyanyua nyuso, wameuza ''ghala la silaha''. Zanzibar hakuna raha kwa CCM.

Wale wa Maalimu Seif alipo wapo, wakipata CCM kidogo tu hata mbinu ya kupunguza majimbo haifanyi kazi

Tegemeo la CCM Zanzibar ni moja , kupitia sera za 'Jecharism'' .
Tatizo la sera hiyo ni moja, umma ukiamua basi maji yatazidi unga kama si tui kuingia maji.
Shah wa Iran na Nicole Ceuasescu wa Romani wanatambua somo la nguvu ya umma vizuri.

Kuhusu Bara, kuna tatizo kubwa sana. Baada ya Lowassa na Sumaye wengi wanawaangalia wahamiaji kwa jicho la shaka sana.

Ni kwa msingi huo Chadema hawafikirii kurudia makosa yaliyowagharimu muda mwingi sana.
Mwaka 2015 CDM walitumia muda mwingi kwa mtu, kitu ambacho kingewapa wabunge wengi.

Kwa upande wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amekomaa na nia yake si uongozi kama yeye bali uongozi wa kuiondoa CCM kwanza. Mtazamo huu umemfanya awe 'muumini' mzuri wa ushirika kwa Wapinzani.

Zitto amegundua tatizo si yeye kuwa kiongozi bali yeye na wenzake kuongoza kuiondoa CCM.
Hii ni ''maturity'' nzuri sana na nampa big up

Pamoja na hayo, kumpokea Membe kuna maswali kama yale tuliyouliza wakati wa Lowassa.
Je, uwekezaji kwa Membe kuna manufaa? Je, kwanini ajiunge dakika za mwisho?
Lengo ni kugombea au kuamini katika demokrasia?

Je, akiwa Kachero anaweza kuleta mabadiliko gani tofauti na yale ya Waziri mkuu Lowassa?
Membe ana dhima ya kuwahahikishia Wapinzani, ana kitu tofauti vinginevyo itakuwa hadithi ile ile.

Kwa upande mwingine najiuliza sana, nini mkakati wa Wapinzani? Suala hapa si kushinda, wana uwezo huo.

Tatizo ni mfumo uliosukwa ambao sasa unahusisha vyombo vingi. Chaguzi zote za marudio zinathibitisha

Hivi Mkurugenzi anakimbia vipi ofisini kupokea fomu na hakuna kinachotokea kwa kosa hilo?

Hivi hatuoni Polisi wakikamata Wapinzani wakati CCM wakisaidiwa na Magereza kupandisha bendera.

Msajili yupo kimya kama vile ofisi yake ipo likizo, huku tume ya uchaguzi na nakala za matokeo ikifanya yake.

Wengi wanadhani Takukuru kuwakamata CCM ni kupambana na rushwa.

Siku kibao kitakapogeuka Wapinzani ''watakamatwa siku moja kabla ya kurudisha fomu''.

Wakurugenzi wataugua masaa machache kabla ya kurudisha fomu.

Mwaka huu CCM itashinda majimbo zaidi ya 50 bila kupingwa kwa namna. Haya hayajulikani?

Kukokesekana kwa tume huru na kushindwa kuidai ni kosa kubwa sana kwa wapinzani

Uchaguzi wa Afrika hauamuliwi na namba bali namna, na ni kwa wale tu wanaoweza kama Malawi , matokeo mengine hayatakuwa tofauti na zama zile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…