Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,891
- 8,448
Rais Kikwete alirudisha hela tuliyopigwa kwenye ununuzi wa rada na hela hiyo ikapelekwa kununua madawati.
Rais Magufuli alirudisha dhahabu iliyokuwa imefichwa Kenya kwa miaka mingi.
Rais Samia unashindwa nini kurudisha hela uliyodai wewe mwenyewe kuwa imefichwa China? Aliyekuwa DPP Biswalo Mganga si bado yupo hai?
Miaka ya nyuma baada ya hayati Benjamini Mkapa kuingia madarakani tulianza kusikia juu ya ukwapuaji wa pesa za umma uliofanyika. Moja ya watuhumiwa alikuwa ni Prof Kighoma malima ambaye alishafariki. Tukaanza kusoma kwenye magazeti kuwa alificha pesa nyiki huko Uingereza. Na baadae tuliskia serikali ilifreeze akaunti yake na kurejesha hizo pesa.
Sasa mkuu wa nchi kusimama hadharani na kutamka kuwa kuna mabil ya pesa yamefichwa China, maana yake anafahamu benki, akaunti na hata walioficha.
Serikali iyarudishe hayo mabil na wahusika walio hai wachukuliwe hatua. Zaidi ya hapo kuna lingine nyuma ya pazia.