Hata hii mbinu ya kupata pesa ikikushinda, rudi tu kijijini ukalime

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Elimu ya bure kabisa hii;

Ingia Mabibo sokoni ama Buguruni. Kapoint matikiti manne ya elfu nne nne. Kila tikitiki likate vipande 40 vya Tsh. 200 @1.

Kwa kila tikiti itatoa gross amount ya 8,000. Ukitoa mtaji wa 4,000 @1, unabaki na faida ya 4,000.

Kwa tikiti zote nne = 4,000 × 4 ~ 16,000

Usihangaike kuuza. Tafuta vijana wanne, wapatie vipande 40 kila mmoja. Wakimaliza tu 1,500 ni yao, kila mmoja kwa kila tikiti.

Ukienda round 2 kwa siku, una uhakika wa kulaza 20,000 net. Hujatoboa tu mpaka hapo?

Akili kumkichwa.

Kabla ya kuweka nukta nilitegemea members wote kuwaona hapa Buguruni mkilangua tikiti kwa bei ya jumla kwenye kiosk changu.

Haya naweka nukta
.
 
Hauna ndugu zako masikini uwashirikishe watajirike kwanza kabla ya kutushirikisha sisi? Charity begins at home.
Luka 4:24 Nabii hatambuliki kwao!
ameshafanya mchango wake wa mawazo wa kuwavusha watu kutoka hatua nyingine kwakuwa za kwanza wanazo hivyo mwenye nia na afanye na hii sio lazima matikiti ziko fursa ndogondogo nyingi za kizembe zikifanyiwa kazi unaweza kuvuka na hazihitaji mtaji mkubwa.
 
Nishafanya hii ilikuwa 2014 japokuwa kwa muda mchache kikubwa unatakiwa uwe msafi na usiwe na aibu tu.

Wateja wangu walikuwa askali wa usalama barabarani,maduka ya hardware,watu wa majumbani,saluni na wengine ni hao wa barabarani mmoja mmoja.
 
Kuna mtu amekuuliza ushauri? Pambana na ufukara wako
 
JF kumejaa matajiri wenye magari na pisi zinazojambia mbali aka eksozi aka vishundu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…