Hata hii nayo tutauza kwa mabepari?

Hata hii nayo tutauza kwa mabepari?


Hivyo visima walichimba watafiti wa gesi na mafuta au kampuni za kuchimba visima vya maji?
Itakuwa wa visima vya maji
Hapo itakua ni Marekani bila shaka.maana kiswaili ndio lugha yao ya Taifa.
Hahahahahahh
Sisi watanganyika ni nyumbu. Tunauziwa Mali asili zetu tupo tu Wala hatuoni umuhimu wetu chadema wakisema tuandamame basi tunawaona ni wachumia tumbo.

Lakini hao hao chadema ndo wanatufundisha namna sahihi ya kurinda rasilimali zetu hata wao wakichukua Dola Bado tutakuwa na uthubutu wa kupinga pale tunapoona wanatuingiza Chaka maana ujasiri huu wote wao ndo walitunoa.

Amini nakuambia mkuu hatutakuwa na majibu ya kuwajibu wajukuu zetu miaka30 tu ijayo itakuwa ni kazi kubwa mnoooo na hakuna majibu.

Sa100 yeye anajua sisi ni vilaza anafanya anavyotaka Wala hazuiliwi
Amini nakuambia mkuu hatutakuwa na majibu ya kuwajibu wajukuu zetu miaka30 tu ijayo itakuwa ni kazi kubwa mnoooo na hakuna majibu.
Daslam ni wengi sana, na wakiwa vigoli ni wazuri kwelikweli.

Vijana wa chuga, elimu iliposimama mnakwama wapi.?
IMG-20241004-WA0052.jpg
 
Mnyundo village, Mambi catchment, kata ya Ndumbwe, halmashauri ya Mtwara vijijiini.
MTWARA - Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeanza uchunguzi kubaini ukweli kuhusu tukio la visima vya maji katika kijiji cha Mnyundo kata ya Ndumbwe, Halmashauri ya Mtwara mkoani Mtwara kuwaka moto.

Wakaguzi kutoka TPDC wamesema taarifa za awali zinaonesha kuna kiwango cha gesi hata hivyo wanahitaji muda kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukubwa wa tukio hilo.

Kwa karibu miezi mitano, Wananchi wa kijiji cha Mnyundo wamesema wamekuwa wakishuhudia visa kwa visima vya maji kuwaka moto.

Wakizungumza na Jamii FM, wananchi hao wamesema hali hii ilianza kutokea baada ya kijana mmoja mwenye tatizo la afya ya akili kufika kisimani hapo kuoga na baada ya kuoga, kijana huyo alishika njiti ya kibiriti na kuiwasha ndipo moto ukaibuka juu ya maji yaliyokuwepo kisimani.

Tukio hili limeendelea kwa zaidi ya miezi mitano, na sasa visima hivyo vimekuwa sehemu ya kivutio kwa watu wanaotaka kujionea wenyewe.



#HabarileoUPDATES
 
Back
Top Bottom