Hata hiki kidubwasha tunaagiza China!

Sawa tumekuelewa, haya tuambie nawewe umegundua nn kweli hili taifa bwana mjuaji.?
 
Hicho ni kitu kikubwa sana,
Toothpick yenyewe tunaagiza China. Haihitaji hata utaalam wowote wala haina mechanism yoyote ile useme hatuwezi kutengeneza.
Ukiitengeneza hapa nyumbani utaandamwa na kodi, ushuru, tozo na mkusanyiko wa mamlaka hadi iwe ghali kuliko itokayo China.
 
Huko wanaenda kujaza vyoo tu
Na wakitoka huko na vyeti vyao wanatafuta ajira serikalini ili waje kutuomba rushwa ya lazima hata kama unataka ku renew kitu
 
Hiki kikubwa sana! Office pin mnatengeneza wapi?
 
Unashangaa hicho kidude!?

Mimi nilishangaa Toothpick (vile vijiti vya kutolea mabaki ya nyama/chakula kwenye meno) vya jero eti vinatoka China
 
Teh teh teh koh koh koh aaaarrrhhh.

Kwa hiyo mkuu kunya sahihi ndiyo kunyaje huko, au mtu hadi apelekwe kozi akajifundishe kunya ndiyo aweze kunya sawa sawa?
Kweli unakuta mtu hajui kwamba unapokata gogo hutakiwi kusukuuuuuma la. Ni unavuta pumzi nyingii unaitoa, shuuuuush... mambo yanaenda menyewee.

Aani ni kama meditation vile😂😂

Unakuta mtu badala atoke kukata gogo ametabasamu, anatoka amekunja sura utadhani alikuwa anagombana. Ujinga tu.

Halafu usiwashangae hao wa kujisaidia, kitu ambacho unajifunza utotoni ndio hadi ujue. Kuna vitu mtu unazaliwa unafanya lakini watu hawakijui. Kupumua kwa mfano. Wapo watu kibao tu hawajui kupumua. Wengi tu😳. Wengi sana

Mnabisha! Unabisha eeeh!??...... basi ingia Youtube, tazama search 'proper breathing technique' au how to breathe well angalia, elewa: halafu jipe maksi
 
Ila inafikirisha sana, inafika hatua mimi ambae sijawahi kwenda shule kabisa naona bora hata mimi najua kushawishi mtu anunue bidhaa zangu.
 
Mleta uzi tunaomba utuonyeshe ugunduzi wako ujitoe kwenye kundi la watanzania wajinga😁😁😁😁
Mm siyo mgunduzi na wala sina elimu ya chuo, ninacholaumu ni ninyi mliofika hadi chuo kikuu mnashindwa kutoa ugunduzi utakaotufaidisha hata sisi tusiokuwa na elimu ya chuo kikuu!...
Ni hayo tu kwa leo.
 
V8 LC300 tunaagiza Japan pia
 
Kaka, hatuna stainless steel. Tukitengeneza vya kwetu tutaweka mabati yanashika KUTU siku mbili tu. Sisi tuache tuendelee kufurahia porojo za chalamila. BURE KABISA
 
Mm siyo mgunduzi na wala sina elimu ya chuo, ninacholaumu ni ninyi mliofika hadi chuo kikuu mnashindwa kutoa ugunduzi utakaotufaidisha hata sisi tusiokuwa na elimu ya chuo kikuu!...
Ni hayo tu kwa leo.
Kwanza tuanzie hapa,wewe Kwa Nini hukufika chuo kikuu?sisi wakati tunapambana na masomo wewe ulitakiwa uwe hata umegundua kitu maana sisi wenzio huko chuo kikuu tulikuwa hatujifunzi ufundi
 
Kaka, hatuna stainless steel. Tukitengeneza vya kwetu tutaweka mabati yanashika KUTU siku mbili tu. Sisi tuache tuendelee kufurahia porojo za chalamila. BURE KABISA
Mmmh hiyo I'd yako hutokaa ukaribishwe ikulu Wala Kizimkazi
 
Wenye viwanda vya vyombo vya nyumbani vya plastic kama Jambo Plastic na Cello Plastic wamelala, fursa hizo kwao
 
Kwanza tuanzie hapa,wewe Kwa Nini hukufika chuo kikuu?sisi wakati tunapambana na masomo wewe ulitakiwa uwe hata umegundua kitu maana sisi wenzio huko chuo kikuu tulikuwa hatujifunzi ufundi
SWALI: Kama tungesoma wote, nani angetawaliwa?.
Huku mtaani bila elimu huo ufundi ningejifunzaje?.
Nadhani twende kwanza na swali juu ya swali kabla ya majibu sahihi.
 
Daaah!!! Vyuoni huko ni nadharia na kukariri kwa sana.

Ukianza kufikiri nje ya boksi unakuta unaenda njia tofauti na lecturers unaliwa kichwa na habari yako inaishia hapo.

Elimu yetu bado ni tatizo, inalaza watu usingizi sana.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…