Hata kama hamumpendi Rais Samia msifikie hatua hii

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Kuna mengi mnaweza msingizia Rais nikanyamaza. Nikasemehe. Lakini hili la kusema ana maono.... Hapana hapa mnamkosea sana.

Mlisema haijengi nchi, nchi haina uelekeo nikanyamaza. Nikasema anyway watu husema kile wanachoona wakifananisha na uzoefu wao. Mkasema anauza nchi nikanyamaza. Nikasema moyoni anyways.

Leo kweli kuna mtu anasema Samia ana Maono. Kweli tumefikia hatua hii akina Lucas mwashambwa ? Ninyie mnapaswa mnyongwe.... "

Akumulikaye mchana usiku atakuchoma moto"

Ninyi ni watu wabaya kabisa na mnatumia uhuru wa kuongea vibaya kumtukana Samia kuwa ana maono. Mnatumia uhuru huo kumsingizia kuwa ana maono. Mtaenda motoni kweli nawaambia.
 
Ngoja chawa na kunguni wake waamke
 
Yafaa uwaulize hao watu kwamba ana maono gani??
Huenda pengine kweli ana maono.
Kumbuka, hata kubomoa nchi nako pia ni maono, ingawaje ni maono hasi.

"The problem of Africans, those with ideas have no power, and those with power have no ideas."
 
" Kuanzia Sasa ni marufuku Kununua ardhi isiyopimwa. Ardhi itauzwa na afisa ardhi tu" unadhani matamko kama haya atampenda nani? Ni wapi wamepima kijijini kwako? Afisa ardhi utampata wapi kijijini na kwa gharama Gani? Madhaifu mengi ya serikali hii jaman. Bora aende zake tu huyo anaumiza wananchi
 
Hahaha. Wewe ndugu unachekesha sana. Dah!
 
We lofa pambana na umaskini wako hayo mengine yako juu ya uwezo wako
 
Maono yake ni uarabuni na Zanzibar tu
 
Mtu na akili zake eti anasema maono ya fulani badala ya uelekeo wa nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…