Hata kama inasemwa ameingia kwa kura za wizi, lakini bado ana sifa za kuwa kiongozi bora hapo kisiwani

Hata kama inasemwa ameingia kwa kura za wizi, lakini bado ana sifa za kuwa kiongozi bora hapo kisiwani

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
12,312
Reaction score
18,194
Kuingia kwa kura za wizi haina maana kuwa hawezi kuwa kiongozi sahihi. Uharamu wa mchakato hauwezi kubadilisha talanta yake kwa uhakika.

Ana hekima, busara, ustaarabu, uvumilivu, anaweza kuchuja kipi aseme na kipi asiseme.

Maalim Seif tupo njia panda kwa sababu anamjua huyu bwana uadilifu wake na ustaarabu wake anaona kuacha serikali kuwa makamo atawadhulumu Wazanzibar.

Nina uhakika kwa namna Hussein Mwinyi anavyo handle mambo kwa hekima basi Maalim seif na ACT WATAKUBALI ZILE NAFASI NA WATAIJENGA ZANZIBAR.

Hussein Mwinyi kakulia kwenye uongozi, anajua uongozi, sio kwamba kasomea tu au kafundishwa akiwa CCM hapana, bali kakulia humo.

Viongozi wengi sana ukiangalia historia zao wameanza kujifunza uongozi walipoingia kwenye vyama, lakini huyu bwana kaanza kujifunza uongozi tokea anazaliwa, bahati nzuri kajifunza kwa baba yake.

Hana ule imbukeni wa urais, hana ulimbukeni wa uongozi, hana ile kujiomesha, hana ile kuwagomea wafanyakazi wake na kutaka wamuogope yeye.

Ni kiongozi mpole ambaye hana Muhali na Mtu

Pengine atakuwa ni Rais wa mwanzo kuwakubalisha na kuwaaminisha Wazanzibar kuwa maendeleo ya Zanzibar yanaweza kuletwa na hata wasiemtaka Wazanzibari.

Laiti Hussein Mwinyi angekuwa amekulia Zanzibar basi pengine angekuwa na tabia za wanaume na viongozi wa kizanzibari za Ufitini, muhali kwa wengine, uoga wa kukemea mambo na kuwaonea shida watu.

Huyu kutokulia Zanzibar kunamfanya awe ni mtu ambae hana muhali na watu wa Zanzibar.

Nakutakia kila la heri Dkt. HUSSEIN MWINYI.
 
Aweza kuwa bora katika uongozi lakini mchakato ni haramu. Hao jamaa wanao watu wazuri lakini hawajiamini. Hawataki kusikia neno katiba ya wananchi au tume huru!
 
Anajitahidi sana...
Ila kumbuka hata walioingia makazini kwa vyeti feki haikumaanisha walikua hawajui kazi...




Cc: mahondaw
 
Aweza kuwa bora katika uongozi lakini mchakato ni haramu. Hao jamaa wanao watu wazuri lakini hawajiamini. Hawataki kusikia neno katiba ya wananchi au tume huru!
Sahihi mkuu.


Wanao watu wazuri sana.
 
Back
Top Bottom