kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Unaposema utakwenda kuzuia uchaguzi Mkuu wa kikatiba unaoipatia Jamhuri yetu viongozi wake wakuu kama Rais, Mkuu wa nchi na Amirijeshi Mkuu, Makamu wa Rais, wabunge na madiwani usifanyike maana yake unadhamiria nchi ama iendelee kuongozwa na viongozi batili ambao muda wao kwa mujibu wa katiba umekwisha au nchi isiwe na viongozi kabisa; imeanguka. Ingetokea hivyo ingekuwaje?
Je, wakati mtuhumiwa anasema anakwenda kukinukisha na kusitisha uchaguzi usifanyike alifikiria kwanza sisi wananchi wa kawaida (wapiga kura) tungeitikia vipi wito wake ule? Je, alidhani wapigakura tungeyapuuza maneno yake na kwenda kupiga kura kwa wingi? kwakuwa hakuweka wazi atakwenda kukinukisha kwa njia gani siku ya uchaguzi alidhani wapigakura wasingeogopa kwenda kupiga kura? .
Hivyo, Kwavyovyote vile kauli zake zile jukwaani zimeingilia uchaguzi wa oct29 kwakuwa lazima kuna watu hawakwenda kupiga kura Oct29 kwa kuogopa kinachoweza kutokea wakati wa kuzuia uchaguzi usifanyike.
Pili, Lissu ni kiongozi mkuu wa chama chake chenye wafuasi wengi, Hivyo, kuwashawishi wafuasi wake ambao pia ni raia wa nchi hii wasiende kupiga kura ni kosa la kisheria pia; ameingilia uchaguzi wa kikatiba. Hakutaka wanachi watumie utashi wao wa kwenda kupiga kura . Yeye alizuia wafuasi wake kuchagua na kuchaguliwa.
Ushahidi kuhusu shitaka hili ulikuwa uko wazi mno kiasi kwamba hata jaji angekuwa mimi ningemkuta na kesi ya kujibu.
Mungu ibariki Tanzania.