Hata kama Jaji ningekuwa mimi Kavulata angekutwa na kesi ya kujibu

Muwe tayari kuleta mashahidi wake
Yaani Rais wetu aache kazi ya kutuhudumia sisi aende akatoe ushahidi mahakamani kwa wito wa mtu aliyetaka kumpindua. Dhihaka gani hii kwa watanzania.
 

Hapa unapoongea kwenye uchaguzi/kipind cha uchaguzi kuna vipindi vitatu:
1: Kabla ya uchaguzi- Rais husika yupo madarakani
2: Wakati wa uchaguzi- Rais hayuko madarakani
3: Baada ya uchaguzi- Rais kuchaguliwa

Ni kipindi kipi hapa 1, 2 au 3 no reform no election itamwondoa Rais madarakani?
 
Makosa ya uchaguzi yapo kwenye sheria za uchaguzi.....loop holes
 
'Mahakama hii haiangalii uzito wa ushahidi na kuaminika kwake'
Jaji Ndunguru.
 
Shida yake ni kwamba amesema mwenyewe kuwa amepanga kuasi kama njia ya kupata mabadiliko ya haraka na kweli vurugu za kumuondoa Rais kwa nguvu zilitokea Oct29 kama alivyosema na kuahidi. Vurugu zilipoanza na watu wakaanza kuchoma kila kitu na kuvamia vituo vya polisi sisi wananchi tulijua kuwa ahadi ya Lissu ya kuasi inatekelezwa rasmi. Tuliogopa sana na kila mtu alikuwa na hofu na kila kitu nchini kilisimama hadi masomo na kazi nchi nzima. Hapo shida iko wapi? Unataka ushahidi gani aloo?

Nchi haikosi Rais mpaka Rais mwingine aapishwe. Kwahiyo hakuna siku nchi yetu imewahi kubaki bila Rais. Wewe unaongea vipindi vipi hivyo?
 
Makosa ya uchaguzi yapo kwenye sheria za uchaguzi.....loop holes
Hata akishinda kwa loopholes anakamatwa tena na kushitakiwa upya ili kuunganishwa na oct29. Huyu ameikosea sana Tanzania na watanzania. Amekosea kuchoma mali za watanzania, hizi ni zetu sisi sio za Samia.
 
Hili dishi halijui hata limeandika nini linaendeshwa na mihemko
Actually alichonikosea mimi ni kuharibu mali zetu watanzania wakati yeye anadai haki yake, baasi. Namchukia mtu yeyote anaetuibia sisi . Hata siku nikibaini na kuthibitika kuwa Rais anatuibia nitamchukia milele.
 
Kifungu cha 39: Mtu yeyote raia au anayedaiwa kuwa na utii kwa nchi anayefanya vitendo kama kupanga, kujaribu au kufanya njama za kumuua, kumdhuru au kumwondoa Madarakani Rais/Mkuu wa Nchi.
Huu ndiyo ugaidi... Sasa Lissu kafanya kipi kati ya hayo?
 
'Mahakama hii haiangalii uzito wa ushahidi na kuaminika kwake'
Jaji Ndunguru.
Ukiangalia uzito wa ushahidi wakati nchi imechomwa kweli na vurugu za uasi zimetokea kweli kama vilevile alivyosema Lissu tutakuwa wajinga sana nchi nzima. Loopholes za kipuuzi za kisheria tutaziziba sisi wenyewe.

Nadhani alikosea kusema wataasi siku ya uchaguzi, angeacha vurugu zitokee zenyewe kuliko kisema halafu vikatokea kama vikevile alivyotutangazia.
 
Huu ndiyo ugaidi... Sasa Lissu kafanya kipi kati ya hayo?
Hujui alichofanya? Kinachomsumbua Lissu ni kutamka hadharani kuwa wataasi na kusitisha uchaguzi. Lissu ni mwenyekiti wa chadema, wakili na mbunge mstaafu. Hivyo, nafasi na kauli yake vinatosha kabisa kuwashawishi wafuasi wake wamtii na kutekeleza alichoagiza kifanyike siku ya uchaguzi. Na bahati mbaya baada ya maagizo yale ya kuasi siku ya uchaguzi hakuwahi kutoa maagizo mengine ya kufuta maagizo yake ya awali ya kuwataka wafuasi wake kuasi na kukinukisha siku ya uchaguzi.

Swali ni Nini yatakuwa matokeo ya maagizo ya kuasi, kukinukisha na kuzuia uchaguzi wa Oct29, 2025 usifanyike kama yakitekelezwa kama yalivyokusudiwa?

Majibu ya swali hili yangekuwa kati ya haya:
1. Uchaguzi usipofanyika uongozi uliopo ungeendelea kubaki madarakani kinyume na Katiba
2. Vurugu zingeiangusha serikali iliyopo na kupata viongozi wapya waliotokana na waliofanya vurugu.
3. Nchi ingebaki bila kiongozi mkuu na viongozi wengine kwa muda

Majibu yote haya hapo juu ni UHAINI
 
Hakuna Sheria duniani ya kuhukumu dhana. Mimi Leo nikisema nitaua mtu kama nisipolipwa hela yangu.. Kwa ivo wewe utanishtaki kwa mauaji?

Umesikia Jaji Ndunguru alichosema. Hakuna ushahidi wenye uzito wala kuaminika uliowashilishwa mahakamani.
 
Kama Serikali ipo sahihi kwanini inatumia nguvu kubwa kupigana nae
 
Mwamba umenyoosha maelezo uko vizuri
 
Hivi akifungwa maana ake ,Neno kukinukisha linakua ni kosa kisheria kulitamka?
 
Actually alichonikosea mimi ni kuharibu mali zetu watanzania wakati yeye anadai haki yake, baasi. Namchukia mtu yeyote anaetuibia sisi . Hata siku nikibaini na kuthibitika kuwa Rais anatuibia nitamchukia milele.
Kwa mujibu wa Raisi "Waliofanya vurugu ni raia wa nje"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…