Hata kama mkeo na watoto unawapenda usisafiri nao kwenye gari moja; wahenga waliishi muda mrefu kwa kukwepa haya

Uaishi Mtwara, kwenu Bukoba, mmechukua likizo na mnapaswa kusafiri mwezi wa 12, una ki VANGUARD chako cha mkopo, hapo mtafanyaje?
Anza kusevu hata laki 1 Kila mwezi Kwa mwaka ni milion 1.2

Ukiongezea Hela kidogo unapata Hela walau ya ndege kwenda na kurudi.
 
Wee mm naenda likizo niache kwenda na wanangu kwenye gari yao wakapande bus. Cha msingi ivunje safari kwa km 500 kila sikuusisafiri moja kwa moja tumia siku 2 ama 3 kama ni mbali sana
Mkuu haya mambo ni ya kuomba sana Mungu akuepushe..
Ukiendesha polepole sana highway kuna hatari..

Kuna mtu alikuwa anaendesha taratibu tuu.. Akafuatwa upande wake na Fuso.. na biashara ikaishia hapo
 
Nimeipita hyo ajali jana mbwewe alooo sikieni tu ajali, ni janga kwa familia
 
Ni kweli hasa Kama mnawindwa kiroho.
Japo kifo ni kifo kikifika kimefika kinaweza fika kikachoma moto nyumba yote mkaondoka familia nzima ilitokea Ukonga akapona mmoja tu hakuwepo nyumbani.
 
Daima ningejua huja baada ya maafa.

Umenena vyema mno. Kubwa ni kuomba stara kwa Muumba na hatma iliyokuwa njema, yaliyobaki ni kwa kudra ya Mwenyezi Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…