Hata kama ni umaskini lakini jamani tuwe na Ubinadamu

Kwani Gongo unapewa bure sio ya pesa, mbona gharama za vinywaji vya bar ziko juu kuliko mama tilie au mghahawa, tafakari kwa makini mkuu.
 
Wanywaji wengi wa pombe hasa wale waliokolea vizuri sio walaji wa chakula labda nyama, ndio maana pombe zinatafuna baadhi ya viungo vyao vya ndani. Kazi wanayofanya kutwa nzima kwa kushindia gongo ni sumu kwenye miili yao, hawatakuwa na maisha marefu wataanza kuumwa.
 
Hii ngumu kuiamini,

Kwasababu mimi nalima na Kwa Dunia ya Leo si kijijini si mashambani watu wanaijua pesa vibaya mno ,hata iwe ndogo lakini utampa.

Tena walevi wa pombe ndiyo kabisa,wao hata ununue pombe Lita ngapi basi hela yao utawapa
 
Mbona ni kawaida, unashangaa nini? Walevi wenyewe wanapenda pombe kuliko chakula. Huku ukiandaa pombe ukaalika walevi watakulimia/kuvuna shamba kwa nguvu zote ila ukiandaa chakula hawaji shughulini
 
Je waungwana Kwa aina hii ya malipo je ni ubinadamu? Hata kama mtu atasema si wamekubali wenyewe je kiubinadamu ni sawa? Hata kama mtu ni maskini ndo umtese kiasi hicho jamani 🥲?
Kuna watu wanapenda gongo sana sio kawaida sema sirikali inapoteza mapato kwa hizo za uchochoroni hazinagana risti ugomvi ndio unaanzia hapo sio kwamba hazileti stimu hapana hazina risti hapo ndio utaona mapipa yanakuja kukamatwa
 
Hii ngumu kuiamini,

Kwasababu mimi nalima na Kwa Dunia ya Leo si kijijini si mashambani watu wanaijua pesa vibaya mno ,hata iwe ndogo lakini utampa.

Tena walevi wa pombe ndiyo kabisa,wao hata ununue pombe Lita ngapi basi hela yao utawapa
Kiukweli hili jambo lilinishangaza na nikamuambia sio kweli, ili kuniaminisha alipiga simu huko Kijijini tukiwa pale pale akaweka sauti huku nasikia akawa anauliza hivi vibarua huko wanalipwa Nini ndo yule mtu huko akajibu kuwa tofauti na Gongo ni kingine tena?
 
Wee jamaa Una akili sana
Hakika unastahili pongezi.
Dunia hii umfanyishe kazi usimlipe.ni uongo
Kidumu cha lita 5 cha gongo unajua ni bei gani? Glass 1 ya gongo ile inakua ndogo zaidi kuliko kikombe cha kahawa unajua inauzwaje kupiga shoti mwili? Hizo ni hela kwa hio amemwambia anawalipa ila anawalipaje wao ndio wanampangia tulipe hivi na hivi usitupe hela mkononi hio hela wewe nunua gongo
 
Anawalipa kidumu cha lita 5 cha gongo bei yake unaijua inauzwaje huko kwa mama muuza au alikwambia hio gongo anawatengenezea mwenyewe hawanunulii?
 
Mtoto gongo na mnya gongo nani mjinga?

Kwangu naona mnywa gongo ndie mjinga, japo sio sana.

Inawezekana hiyo gongo ndio inawapa nguvu za kufanya kazi zaidi ya vile wangefanya wakila ugali.
 
Haya mambo yame asisiwa na c.c.m kuwapa watu chumvi, kofia, na kanga awamu hii wame jitahidi kidogo, baiskel na pikipiki kwa wewe ume shangazwa Hilo tu.
 
Huyo Baba Yeye hanywagi pombe Kabisa
Anatoa hela
Ananunua gongo
Vibarua wanasema ili tulime sisi wewe tununulie gongo tu tunalima vizuri sana

Wewe ulitaka afanyaje hata ungekua wewe ungefanyaje ujitie tajiri umpe kila mlimaji million 10?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…