Hata kama ni umaskini lakini jamani tuwe na Ubinadamu

Kuna Baba Mmoja jirani yangu hapa juzi, katoka kwao Mbulu kwenye kilimo basi katika maongezi yanayohusu kilimo huko alikotoka Kuna jambo kidogo lilinishangaza sana na kufanya siku yangu yote kuharibika.

Ni hivi huyu bwana mara ya mwisho kutoka hapa kwenda huko kwao kwenye kilimo Kwa maelezo yake alikuwa na nauli ya kwenda TU na ilikuwa msimu wa kulima Sasa nikamuuliza, je vibarua hao wanaolima aliwalipa nini wakati alikuwa Hana pesa nyingine?

Alichonijibu ni hiki; kule kwao Yan sehemu kubwa ya maisha ya huko au utamaduni unaotumika kuwalipa vibarua ni kuwanunulia Gongo kwenye galoni ya Lita 5 au kitoto ndoo Cha Gongo kulingana na ukubwa wa shamba na wingi wa vibarua,

Huko shambani ambapo watafanya kazi kuanzia Asubuhi Hadi jioni Kwa ujira wa kunywa Gongo TU tena wakiwa huko huko shambani .

Hakuna malipo mengine wala chakula watakachopewa huko shambani au baada ya kumaliza kazi aidha ya kulima ,kupalilia au kuvuna. Na Maisha yanaendelea kama kawaida.

Je waungwana Kwa aina hii ya malipo je ni ubinadamu? Hata kama mtu atasema si wamekubali wenyewe je kiubinadamu ni sawa? Hata kama mtu ni maskini ndo umtese kiasi hicho jamani 🥲?
Tujitaidi kuchakata habari kabla ya kuileta humu, hii habari ni ya uongo na ni ya upotoshaji.
 
Comment yako imetawaliwa na Selfishness,

Wewe walipe hela zao,wao ndio wataamua hizo hela watazitumia vipi kuliko kuwapo gongo,hapo unakua umehusika direct kuwalisha sumu,
Halafu tambua kua Gongo ni pombe haramu,so hili ni kosa kisheria,
Ina maana wewe ukiona mtu anahatarisha afya yake,huna jukumu la kumpa tahadhari kisa hakuhusu au haina madhara kwako?

Huwezi kumtumbukiza kwenye majanga binadamu mwenzako kisa eti wapo binadamu wengine wanazaliwa na utawatumia,
Kila binadamu ni unique.

Hela zao zipi Mkuu?😃😂
Hawana hela kwangu,

Hela ni medium ya exchange tuu.
Sio lazima ulipwe pesa. Sijui kwa nini watu wamekariri hivi.

Mwingine anaweza kukuambia anahitaji mahindi tuu. Kwamba akulimie alafu utampa mahindi. Ndio hitaji lake.

Kwamba unafanya kazi kwa mahitaji yako.
Hao Wakulima hitaji lao sio mahindi. Huenda wanachakula nyumbani.
Hitaji lao ni Pombe. Hivyo wanafanya kazi ili wapate wasichonacho(pombe)

Pombe, gongo ni haramu kwako au serikali lakini sio haramu kwa Kila MTU.
Gongo ni local beer ilikuwepo tangu kabla ya ukoloni.
Wanaokataza gongo ni kwaajili ya kudhibiti pombe za kienyeji tuu ili pombe za kizungu kama konyaji, sijui KVant ziuzwe.

Hoja iwe je pombe wanayopewa inalingana na kazi wanayoifanya? Mazingira ya kazi yakoje?

Lakini kusema wasilipwe Gongo kisa UTU hapo nitakataa.

Tukija kwenye suala la Ubinafsi.

Maisha kama maisha ni mfumo wa ubinafsi naturally hivyo tunapojitahidi kuondoa ubinafsi ni tunajaribu ku-fake lakini sio asili
Jambo au mahusiano yoyote unayoyaona hayana ubinafsi ujue ni FAKE, Utapeli. Ndio maana Sisi Watibeli hatuamini

Binadamu ni Mnyama. Kama unavyomuona Mbwa, mbuzi, ng'ombe, Simba.
Nature inatambua hivyo.

Ni ubinafsi WA binadamu kujifanya wao sio wanyama😂😂 lakini nature inakataa.
Ndio maana wajanja kwa kulijua Hilo mapema hutumia fursa hiyo kujinufaisha.

Binadamu akishakuwa na uungu ndio anakuwa MTU. Uungu wengi mnauita UTU.
Sio Kila binadamu ni MTU.
 
Kama jamii inafumbia macho hayo kwa kigezo cha ridhaa kwamba wanataka wao basi tunatengeneza taifa lenye watu wajinga wajinga wengi na wagonjwa kila siku.
 
Ila wewe bwana.
Mtu katoka mkoa mwingine kwenda Mbulu akiwa na nauli ya kwenda tu kwakua vibarua wanataka gongo tu.

Logically, inamaanisha huyu alitoka akiwa na nauli tu kwavile malipo ya vibarua wa Mbulu hua ni gongo tu. Siyo kwamba aliongea nao kabla hajaenda ni kwavile anajua malipo ni hayo.

Soma tena alichoandika ili uelewe kwanini niliandika vile
Rudi ukasome upya kuanzia mwanzo kasema vibarua walichotaka awape ni gongo sio pesa na gongo sio ya bure inanunuliwa kwa maana hio hapo hapo kwenye kodumu ka lita 5 wanakadiriana vikombe wanajua kila kikombe kimoja cha gongo bei gani?
 
Kuna Baba Mmoja jirani yangu hapa juzi, katoka kwao Mbulu kwenye kilimo basi katika maongezi yanayohusu kilimo huko alikotoka Kuna jambo kidogo lilinishangaza sana na kufanya siku yangu yote kuharibika.

Ni hivi huyu bwana mara ya mwisho kutoka hapa kwenda huko kwao kwenye kilimo Kwa maelezo yake alikuwa na nauli ya kwenda TU na ilikuwa msimu wa kulima Sasa nikamuuliza, je vibarua hao wanaolima aliwalipa nini wakati alikuwa Hana pesa nyingine?

Alichonijibu ni hiki; kule kwao Yan sehemu kubwa ya maisha ya huko au utamaduni unaotumika kuwalipa vibarua ni kuwanunulia Gongo kwenye galoni ya Lita 5 au kitoto ndoo Cha Gongo kulingana na ukubwa wa shamba na wingi wa vibarua,

Huko shambani ambapo watafanya kazi kuanzia Asubuhi Hadi jioni Kwa ujira wa kunywa Gongo TU tena wakiwa huko huko shambani .

Hakuna malipo mengine wala chakula watakachopewa huko shambani au baada ya kumaliza kazi aidha ya kulima ,kupalilia au kuvuna. Na Maisha yanaendelea kama kawaida.

Je waungwana Kwa aina hii ya malipo je ni ubinadamu? Hata kama mtu atasema si wamekubali wenyewe je kiubinadamu ni sawa? Hata kama mtu ni maskini ndo umtese kiasi hicho jamani 🥲?
Hapo kuna mambo ya kikazi na stahiki za wafanyakazi hazipo sawa.
 
Hii ishakua kama utamaduni kwa jamii fulani unakutana wanaalikana katika kulima shamba la mtu so baada ya pale wanapongezwa kwa chakula tu ila sasa hii ya gongo ni mbaya sana
Kwetu Ungonini inaitwa "mkumi" ila mnaandaa chakula kizuri na kitamu, km wali na nyama,
Na sio kila siku, ni siku chache kwa kila mwananchi.
 
Kama jamii inafumbia macho hayo kwa kigezo cha ridhaa kwamba wanataka wao basi tunatengeneza taifa lenye watu wajinga wajinga wengi na wagonjwa kila siku.
Mwaka 2011 babu Mzee Samunge wa Loliondo marehemu, aliitisha watu wakanywe kikombe kimoja cha dawa inayotibu mpaka ukimwi kwa gharama ya shilling 500 tu kwa kila kikombe, watu walitoka ndani ya afrika mashariki, kasikazini, magharibi mpaka kusini kuja kwa Mzee Samunge kupiga kikombe, hivi unataka kuniambia Mzee Samunge aliwashikia fimbo watu hawa au walikuja wenyewe kunywa dawa na kulikua na msululu wa magari foleni kubwa zote zinawahi kwa babu aliwashikia fimbo si walienda wenyewe? Hakuna mtu anaeshikiwa fimbo ili apewe gongo ni hiari yake mwenyewe

Kuna mwamba yeye alikua ili akulimie hataki pesa nyingi wewe mtafutie misokoto yako kadhaa tu ya bangi mpelekee anakulimia vizuri tu ila alikua na sharti moja tu la ziada ukivuna usimsahau yaan km ulivuna ukapata gunia 10 basi mpe hata gunia 1 kwake sio mbaya ndio malipo yake hayo
 
Kuna Baba Mmoja jirani yangu hapa juzi, katoka kwao Mbulu kwenye kilimo basi katika maongezi yanayohusu kilimo huko alikotoka Kuna jambo kidogo lilinishangaza sana na kufanya siku yangu yote kuharibika.

Ni hivi huyu bwana mara ya mwisho kutoka hapa kwenda huko kwao kwenye kilimo Kwa maelezo yake alikuwa na nauli ya kwenda TU na ilikuwa msimu wa kulima Sasa nikamuuliza, je vibarua hao wanaolima aliwalipa nini wakati alikuwa Hana pesa nyingine?

Alichonijibu ni hiki; kule kwao Yan sehemu kubwa ya maisha ya huko au utamaduni unaotumika kuwalipa vibarua ni kuwanunulia Gongo kwenye galoni ya Lita 5 au kitoto ndoo Cha Gongo kulingana na ukubwa wa shamba na wingi wa vibarua,

Huko shambani ambapo watafanya kazi kuanzia Asubuhi Hadi jioni Kwa ujira wa kunywa Gongo TU tena wakiwa huko huko shambani .

Hakuna malipo mengine wala chakula watakachopewa huko shambani au baada ya kumaliza kazi aidha ya kulima ,kupalilia au kuvuna. Na Maisha yanaendelea kama kawaida.

Je waungwana Kwa aina hii ya malipo je ni ubinadamu? Hata kama mtu atasema si wamekubali wenyewe je kiubinadamu ni sawa? Hata kama mtu ni maskini ndo umtese kiasi hicho jamani 🥲?
Sizani kama aliyekujibu ana akili timamu mfano hata kama ingekuwa kweli ningejibu Huwa wanalima mazao yakiiva tunauza Kisha tunawalipa
 
Rudi ukasome upya kuanzia mwanzo kasema vibarua walichotaka awape ni gongo sio pesa na gongo sio ya bure inanunuliwa kwa maana hio hapo hapo kwenye kodumu ka lita 5 wanakadiriana vikombe wanajua kila kikombe kimoja cha gongo bei gani?
Aisee. Haya sawa
 
ALIME KWA GONGO BILA C ATAKUFA.HUYO MLETA MADA HAJAMWELEWA HUYO MZEE.MBULU NIMEISHI PALE VIJIJIJI VYOTE NAVIFAHAMU HAKUNA KITU KM HICHO.ZAMANI WATU WALIKUWA WANALIMA KWA UMOJA LEO KWA HUYU KESHO KWA YULE ILA UNAANDAA POMBE NA MAKANDE NA POMBE ENYEwe ni ya mtama inaitwa busa.hyo gongo ndyo nasikia toka kwako
 
Kuna mchangiaji kasema huyo dingi aliona jamaa ni snitch kwahiyo akaficha siri.
 
Back
Top Bottom