Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Tanzania kwa sasa tunahitaji mtu mwenye akili nyingi kichwani na maono ya miaka 100 mbele kama Mwalimu Julius Nyerere.Rais Samia Suluhu Hassan, amekuwa Rais wa JMT kwa mujibu wa katiba, bila matayarisho. Haijalishi ni mwanamke ama nani, lakini Ccm ilipopata 84% ya kura zote kwenye uchaguzi mkuu, maana yakeni kwamba 84% zilikubaliana na Ccm na mambo yake yote akiwemo Rais Samia Hassan, kama Makamu wa Raisi na majukumu yake yote likiwemo la kura Rais wa nchi iwapo ingetokea ndivyo sivyo kwa Rais. 84% ya kura hazikuwa za Rais Hayati Magufuli peke yake bali zilikuwa pia za SSH, ilani ya Ccm na kila kitu cha Ccm kwa mujibu wa katiba.
Sasa yanaibuka malumbano mbali mbali, mara "-
Mama hakuchaguliwa, kitu kinachoonyesha namna gani watoa hoja, hawana uelewa wa mifumo inayoongoza nchi.
Kila mtu anasema anachoweza bila mipaka ili mradi anatumia uhuru wa kujieleza. Sasa, ombi langu ni hili:-
Watanzania tumsaidie Rais kutuongoza ili tusonge mbele. Kumdhoofisha kwa namna yoyote ni kudhoofisha nguvu yake ya kutuongoza na hivyo kudumaza maendeleo na mustakabari wa taifa.
Hulka ya kuwa kila mtu ni mjuzi wa mambo yote, ni dalili ya kushuka kwa thamani ama viwango vya elimu nchini. Lakini hii haiondoi kwamba katika Elimu kuna maarifa na maarifa ni nguvu hivyo, wananchi tunapashwa kuheshimu utaalam ufanye kazi badala ya porojo na kampeni za kisiasa kila mahali.
Ninaona baada ya nafasi za kisiasa, sasa watu wanaanza kupiga kampeni za wataalamu, mtoe huyu, mweke huyu bila kutolewa maelezo ya kitaalam. Hii inafanya wataalam waone hawanathamani na inaweza kuharibu viwango vyao vya utendaji kazi. Taratibu za kuchukuliana hatua pale mtaalamu anapoharibu, zifuatwe lakini si kelele za mtoe huyu, mweke huyu.
Mama ni kiongozi mkuu wa nchi lakini pia ni binadamu kama binadamu wengine. Anapoonekana kukosea, akosolewe kwa adabu na heshima. Hii itampa nafasi yeye na watu wake wa karibu kutafakari na kujipanga vyema namna ya kurekebisha kasoro, bila fedheha. Unapomfedhehesha kiongozi wa nchi, unalifedhehesha taifa na hakuna mtu mwenye akli timamu atakayeona fahari kuwa chini ya uongozi unaodharaulika na kufedheheshwa isipokuwa mtu yule asiyelitakia mema taifa, mwenye nia ya kuasisi machafuko ambayo mwisho wa siku hayamnufaishi mwananchi wa kawaida.
Ccm ndiko chimbuko kubwa la uharibifu dhidi ya taasis ya Urais. Watu wengi wanajigundisha na urais kwa kuamini kwamba kwa kuwa ccm inatawala basi kila kiongozi wa CCM ni mtawala wa wasio ccm katika ngazi yoyote aliyopo, na ni serikali na ananguvu na uhuru wa kufanya lolote. Wana ccm acheni kutuharibia nchi. Kaeni mbali na serikali, mmwache mama afanye kazi na serikali yake.
Tofautisheni Chama na Serikali kwa kuwa kama inavyoonekana, bila hiyo tofauti, migogoro yenu ya chama sasa mnaiunganisha serikalini. Tunafahamu kwamba Ccm mnajifanya mentors na mmejiglue na urais ili kufanya manipulations tu na si kwa sababu nyingine yoyote. Sasa mwacheni Rais kwa sababu Urais ni taaisis kubwa yenye mifumo mingi inayotakiwa kuimarishwa, kutumika na kusimamiwa ipasavyo ili kufanya kazi na Rais kwa maslahi ya taifa.
Kwa mutakabar wa taifa, tunaomba katikba mpya, isiyona ulali kwenye vyama vya siasa, za kisiasa bali kwa ustawi wa Taifa na vizazi vijavyo. Mfano katiba ikiweka bayana kwamba Rais, asiwe na uenyekiti kwa chama chake, bila shaka, machafuko ya kwenye vyama yatabakia huko na hayataliingiza taifa kwenye sintofaham.
Hatuhitaji akina Hadija Koppa, Aisha Mashauzi, Abdul Misambano, Badi Bakule, Mwinjuma Muumini, Dr. Manyau nyau, Babu Tale, nk kuendelea kutuamulia hatma ya Taifa letu.