Pamoja na Uhuru wa kuongea na kutoa maoni kwa mujibu wa Katiba tuliyonao,, ila Uhuru wa kufikia kiwango Cha kukosa nidhamu na adabu kwa kumkejeli na kumtukana Rais wa JMT kwa ID fake hii haikubaliki!?
Ukiangalia comments nyingi za wadau hapa jukwaan kwa ID fake, ama kwingineko huko utaona watu wengi wanasema Huyu Mama tumepigwa, huyu Mama Ni mweupe kichwani, huyu Mama hamna kitu, huyu Mama tumepigwa, Mara hivi Mara vile na matusi mengi mengi yasiyovumilika!!
Ndugu zangu waTZ , muda wa Mama utapita, uzuri kaulj zile za atake asitake tutampa uraisi wa kudumu zimeexpire na Bwana yule, hatuna haja ya kutukana au kumkejeli Rais.
Ni kweli, gharama za maisha zimepanda, Ni kweli tozo Ni nyingi kuzidi kipato Cha mtu mmoja mmoja, lakini Kuna namna Mama huyu anajitahid kuwakwamua wananchi wake, mathalani, kakubali nyongeza ya mshahara kwa watumishi, ametangaza neema ya ajira kwa vijana , kakubali kuweka luzuku kwenye mafuta na huku miradi mengineyo hatuoni ikikwama popote ingawa Ni miradi ya gharama z juu!!
Kama Ni suala la kupanda kwa Deni la taifa, no dought, mtangulizi wake kwa usiri mkubwa kachangia Sana Sana!!
Tumkosoe kwa staha, na si kejeli na matusi ya hapo na pale!