Hata kama Rais Samia haumkubali, si sahihi kumpuuza na kumwandikia jumbe zisizo na staha

Tanzania kwa sasa tunahitaji mtu mwenye akili nyingi kichwani na maono ya miaka 100 mbele kama Mwalimu Julius Nyerere.

Hatuhitaji akina Hadija Koppa, Aisha Mashauzi, Abdul Misambano, Badi Bakule, Mwinjuma Muumini, Dr. Manyau nyau, Babu Tale, nk kuendelea kutuamulia hatma ya Taifa letu.
 
Tumefikaje hapa na tunafikaje hapo?
 
Kumuondoa spika kwa kutofautiana misimamo ni dalili ya kutosha kuonyesha ubovu wa fikra na katiba yetu.
 
Great!. Sasa tuende namna ya ku-break the circle.
Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba irudishwe kwenye Bunge la Katiba lenye Wanasiasa wachache na wataalam wengi kutoka kwenye makundi mbalimbali ya kijamii.
 
Unataka kumwondoa kwa utaratibu gani? Kumdhoofisha ni kulidhoofishsa taifa na haina maslahi kwa yeyote. Anapopungukiwa, tumpe nguvu ili tusonge mbele. Kosa lake kubwa ni lipi kwa mjibu wa kwako?
Kosa lake kubwa ni dhihaka kwa mtangulizi wake Dkt Magufuli ambaye alimuamini Mama. Na dhihaka inajidhihirisha hasa kwenye matamko yake (mara tunafungua nchi, etc). Mama angebaki yeye kama yeye badala ya kutaka kupata umaarufu kupitia kumdhihaki Dkt Magufuli mbona hakuwa na shida. Lakini sasa kitu ambacho hakijui ni kuwa yeye hana connection ndani ya CCM, Dkt Magufuli alitengeneza connection ndani ya CCM kwa miaka 5 na ushindi wa kiti cha urais ni ushahidi wa huko kukubalika kiasi kwamba hakuna anayeweza kumsaliti Dkt Magufuli, sasa hivi watajipendekeza ila siku hakika wakimtoa Mama tutasikia mengi.
 
🐒🐒🐒
Your browser is not able to display this video.
Your browser is not able to display this video.
 
Pamoja na Uhuru wa kuongea na kutoa maoni kwa mujibu wa Katiba tuliyonao,, ila Uhuru wa kufikia kiwango Cha kukosa nidhamu na adabu kwa kumkejeli na kumtukana Rais wa JMT kwa ID fake hii haikubaliki!?

Ukiangalia comments nyingi za wadau hapa jukwaan kwa ID fake, ama kwingineko huko utaona watu wengi wanasema Huyu Mama tumepigwa, huyu Mama Ni mweupe kichwani, huyu Mama hamna kitu, huyu Mama tumepigwa, Mara hivi Mara vile na matusi mengi mengi yasiyovumilika!!

Ndugu zangu waTZ , muda wa Mama utapita, uzuri kaulj zile za atake asitake tutampa uraisi wa kudumu zimeexpire na Bwana yule, hatuna haja ya kutukana au kumkejeli Rais.

Ni kweli, gharama za maisha zimepanda, Ni kweli tozo Ni nyingi kuzidi kipato Cha mtu mmoja mmoja, lakini Kuna namna Mama huyu anajitahid kuwakwamua wananchi wake, mathalani, kakubali nyongeza ya mshahara kwa watumishi, ametangaza neema ya ajira kwa vijana , kakubali kuweka luzuku kwenye mafuta na huku miradi mengineyo hatuoni ikikwama popote ingawa Ni miradi ya gharama z juu!!

Kama Ni suala la kupanda kwa Deni la taifa, no dought, mtangulizi wake kwa usiri mkubwa kachangia Sana Sana!!

Tumkosoe kwa staha, na si kejeli na matusi ya hapo na pale!
 
Luzuku ndo Nini mkuu?
 
Naunga mkono hoja.
P
 
Wana Imani kwa kufanya hivyo watamkatisha tamaa. Lkn huyu Mama atafanya vizuri kuliko matarajio ya yule muongo.
 
Watanzania ni washenzi sana. Wanamtukana Mhe. Rais wakati kuna kipindi jamii forums ilifungiwa wakawa wanatumia jamii forums ya Kenya na VPN.

Yote hayo Wamesahau
Inatakiwa waongozwe na mtu kama Aliekua rais wa Uganda Idd Amini
 
Nilipoona umeandika neno Luzuku tuu, nikaahirisha kusoma uzi wako. All in all hakuna anayependwa na wote ndugu. Alichukiwa Yesu Kristo sembuse mwanadamu wa kawaida? Tuwe na vifua, tukubali kutokukubalina. Tunaoimba wimbo wa #Mama anaupiga mwingi, tusianze kutoa nduru tukizidiwa sauti na hao wanaosema hayo uliyoyasema.
 
wanaokejeli ni wale wafuasi wa Jpm na Wafuasi wa Ndugai.

Hawa washughulikiwe. Wasituharubie nchi.
 
ama kwingineko huko utaona watu wengi wanasema Huyu Mama tumepigwa, huyu Mama Ni mweupe kichwani, huyu Mama hamna kitu, huyu Mama tumepigwa


mkuu
mbona hats wewe unakoleza rangi..!?
 
Watanzania ni washenzi sana. Wanamtukana Mhe. Rais wakati kuna kipindi jamii forum ilifungiwa wakawa wanatumia jamii forum ya Kenya na VPN.
Yote hayo Wamesahau
Inatakiwa waongozwe na mtu kama Aliekua rais wa Uganda Idd Amini
Una mchango mzuri lakini kutukana sio kaliba nzuri na wewe umefanya kosa lileliwe na mbaya zaidi umemtukana yeye na watanzania wote wakiwemo wazazi wako, viongozi na kila mtu.Soma comment yako tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…