#COVID19 Hata kama tunawachukia, tukubali kuwa Rwanda wametuzidi Kimkakati na kwa Fikra za Kimaendeleo

#COVID19 Hata kama tunawachukia, tukubali kuwa Rwanda wametuzidi Kimkakati na kwa Fikra za Kimaendeleo

Mapambano ya ka mkoa kamoja unataka yawe sawa naya nchi kubwa ..amia uko.
Mkuu Kama mnaona hii nchi Ni kubwa Sana kuiletea maendeleo, na Rwanda wameweza kwa sababu ya udogo wa nchi yao Basi kwa nini na sisi tusianzishe serikali za majimbo ili Basi owe rahisi kwa viongozi wa majimbo hayo kubuni mbinu za kuleta maendeleo kwa Kasi na kwa kutumia rasilimali zinazopatikana kwenye eneo husika? Otherwise tukubali tu mazaifu yetu Kama nchi tuna tatizo kubwa linalotukwamisha Ila hatutaki kukubali. Niishie hapo.
 
Kusema kweli Rwanda wameweza mambo mengi Sana kwa kipindi kifupi kutokana na maono ya kiongozi wao na viongozi kwa ujumla. Tatizo ninaloliona Ni muendelezo wa hayo mafanikio maana sioni mipango endelevu na hii inatokana na ukosefu wa utashi kutengeneza succession plan ya kiongozi kutokana na ubinafsi wa viongozi waliopo madarakani. Na hili Ni tatizo kwa nchi zote za Afrika.
 
Yap unakuwa simple kuwatawala pia rais mmoja amekaa mda mrefu ana set mipango nakuoteeleza huku akianzisha huyu anayekuja anakiondoa.
Dawa ya kuendeleza mazuri Ni kuwa na Sera ya pamoja iliyokubalika na wote ili yeyote atakayekuwa kiongozi aifuate bila kupinda na kuja na mambo yake. Aongoze kwa mujibu wa Sera ya nchi siyo matakwa yake na Sheria imtake kufanya hivyo.
 
Mku wewe kama great thinker tufanyaje tuwapite au tuwakaribie.
Tuache ubinafsi na tuwe wazalendo. Tufanye kazi kwa bidii Sana, tuweke vipaumbele siyo tunafanya hili halijaisha tunarukia lingine, tujitathimini kwa kila tufanyalo. Miradi ya maendeleo ipewe kipaumbele tutumia rasilimali zetu nyingi kutengeneza na kunoresha miradi ya maendeleo na tupunguze gharama za utawala kwa kupunguza au kufuta kabisa mavyeo yasiyo na tija.
 
Wizi wa rasilimali DRC na mauaji ya innocent lives kweli wametuzidi, ila Kigali iliyo sawa na Iringa town, na huko mbugani wanakojivunia sokwe 17 tu, sidhani kama wanatuzidi kitu.

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Wewe usilinganishe ka nchi na nchi. Tanzania unalinganisha na Rwanda ? Hauko serious kabisa.hako nchi sawa tu na mkoa wa Geita leo unalinganisha na TZ yetu ? Umekosa kazi ya kufanya pole sana.
Another Fool...!!!
 
Tujadili African countries kulingana na uchumi wetu na jiografia.
Intellectually kufanya Logical Reference hakuangalii sana Geographical Factors bali ni Uhalisia, Uthubutu na Ufanisi wa Watu.

Kwanini baadhi ya Watanzania tena mnaojiita Great Thinkers mnakuwa Weak hivi Mentally katika kukabili Mijadala inayohitaji utulivu wa Ubongo?
 
Hata Hapa kama akatokea kidume akayafanya kama alivofanya Paul Kagame basi basi hii nchi itakuwa Pepo watanzania hawajali raisi atakaa muhula gani lkn wanachojali ni maendeleo tu .Paul Kagame alikijua anachotaka ndio maana leo Rwanda inapaa katika anga za kimataifa na kuipata itachukua 100 yrs kwa Tz .
Safi sana Ndugu. Umemaliza kila Kitu.
 
Wizi wa rasilimali DRC na mauaji ya innocent lives kweli wametuzidi, ila Kigali iliyo sawa na Iringa town, na huko mbugani wanakojivunia sokwe 17 tu, sidhani kama wanatuzidi kitu.

Everyday is Saturday.............................. 😎
I never knew that you are also this Fool.
 
Inapaa kwa lipi ? Kwa kutawala kwa fimbo ya chuma ?
Hata Hapa kama akatokea kidume akayafanya kama alivofanya Paul Kagame basi basi hii nchi itakuwa Pepo watanzania hawajali raisi atakaa muhula gani lkn wanachojali ni maendeleo tu .Paul Kagame alikijua anachotaka ndio maana leo Rwanda inapaa katika anga za kimataifa na kuipata itachukua 100 yrs kwa Tz .
 
Kuna mengi ya kujifunza kutoka Rwanda hasa kwenye nidhamu ya watumishi wa umma na maendeleo.
Ukimpa PK hii Tanzania kuna watu watapiga kelele kuomba msaada kwa Armstadam na haki za binadamu,Rwanda ilipofika sasa ni kwasababu Kagame acheki na nyani,wakati unaandaa kongamano la katiba mpya na yeye anakundalia makazi ya milele.Rwanda ukila rushwa alafu ukabainika nusu utakua hai nusu umekufa.
hakuna cha kujifunza kutoka rwanda wao ndo wajifunze kutoka kwetu, unaweza kujifunza nini kutoka kwenye nchi isiyo na demokrasia na uhuru wa kujieleza? watumishi wamejaa nidhamu za uoga tu
 
Nchi yetu ilipaswa kugawanywa kwenye majimbo ili iwe rahisi kusimamia maendeleo kea mfumo wa magavana!!ingekuwa rahisi Sana kusimamia maendeleo kuliko mfumo wa mikoa ambao ni ngumu Sana wizara kusimamia mapato na matumizi!!
 
Nchi yao ndogo na serikali yao inawaonyosha wale wabadhilifu...
 
Back
Top Bottom