Hata Magufuli aliagiza Uchunguzi wa shambulio la Lissu Ufanyike, Je Ulifanyika? Ujasiri wa kuamini kauli ya Rais Samia mnautoa wapi?

May be Kwa LISU at least unaweza kujenga hoja kuwa alikuwa Mwiba mchungu Kwa serikali ya mwendazake,Sasa huyo Marehemu Ally mbona hata hakuwa MTU mwenye kukinzana na Dola?

Hadi ipelekee auwawe kifo kama Hiko.
Uenda alikua master mind wa nyuma ya pazia.
 
Hakuna uwezekano wowote ule wa kuwaamini viongozi wa CCM, hata kama wewe ni Mjinga kiasi gani, ili uwaamini unapaswa kuwa huna kabisa Ubongo.

Dkt Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM kama alivyo Samia Suluhu leo, Aliagiza waliomshambulia Tundu Lissu watafutwe, na katika ujumbe wake alijidai kusikitishwa sana na Shambulio lile, wako wanaosema Alilia kinafiki na machozi yakamtoka.

Sasa Je Uchunguzi wa Shambulio la Lissu ulifanyika?

Soma Pia: Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao

Ujasiri wa kumuamini huyu Rais wa sasa mnautoa wapi?
Kwa hiyo ulitaka kusemaje!
 
Wewe ndio hukuelewa machozi ya ukweli yalimtoka aliposikia Lissu hakufa.
 
Wenye kusoma kitabu cha bibilia, historia ya Samson na Delilah.
Yule bibi ni Delila na Tanganyika ni Samson.
Mtanikumbuka
 
Swali langu mbowe alifungwa gerezani ilikua lini? Ulikua utawala wa magufuli au Samia? Tuanzie hapo ili tuweze kumpongeza Samia kupambana kumuachia kama ulivyosema
Haijalishi alifungwa wakati wa nani, hao wote wawili ni marais wanaotekeleza ilani ya CCM.
 
Kaka umempongeza Samia kumuachia mbowe ikiwa yeye ndio alimfunga. Hapo huoni unajitekenya?

Kuna mengi mazuri ya kuzungumza Ila msijitoe akili kwa yale ambayo hayapo sawa. Kama hayapo sawa yasemwe
 
Magufuli aliweza kutuhumiwa kuhusu kifo cha Lissu na tuhuma zilifanana na aina ya awamu yake akiwa ni mtu mwenye hasira na asiyependa kukosolewa.

Samia unawezaje ukiwa na akili zako timamu ukamhusisha na mauaji ya huyo Kibao?. Lissu kapigwa risasi na akiwa kalazwa Nairobi ni Samia aliyekwenda hospitali kumjulia hali.

Samia amekuwa kiongozi wa kwanza kuhudhuria mkutano mkuu wa CHADEMA akiwa kaalikwa kwa nafasi yake, anaweza kutuma watu wamuue kiongozi wa kawaida wa CHADEMA?.

Kapambana mpaka Mbowe akatoka gerezani na akarudi uraiani unaweza kumhusisha na kifo cha Kibao?.

Ushahidi wa kimazingira tu unatosha kumuweka mbali Samia ni suala la kifo cha huyo mjumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA.

Mkuu rekebisha hiyo. Lissu bado yuko hai. Vile vile kitendo cha yeye kwenda kumuona hakimfanyi awe innocent. Ni yeye pia ndiye aliyedai kuwa askari wao huwa hawakosi.

Ni yeye yeye aliyemfungulia kesi Mbowe na baadaye kumachia na kuja na hizo R4 ambazo zinampa shida kuzitekeleza. Ninachoweza kukubaliana na wewe ni kuwa anaonyesha ana nia nzuri .... ila watu wake behind the scene ndiyo wanamtoa kwenye reli. That is one possibility.

Another possibility ni kwamba madaraka yamemuingi kichwani sasa anataka kuendelea 2025 kwa kila hali ..... hata kwa damu ya wachache kumwagika ili mradi afanikiwe.
 
Kaka umempongeza Samia kumuachia mbowe ikiwa yeye ndio alimfunga. Hapo huoni unajitekenya?

Kuna mengi mazuri ya kuzungumza Ila msijitoe akili kwa yale ambayo hayapo sawa. Kama hayapo sawa yasemwe
Weka ushahidi wako wazi na kila mtu aone kwamba Rais Samia au JPM ndio alimuua fulani mtoto wa fulani.

Ukikosa ushahidi wa wazi hizo tuhuma zako zinabakia kuwa tuhuma tu, huwezi kuzipeleka mahakamani ukazitumia kama ushahidi unapofungua kesi.
 
Mkuu rekebisha hiyo. Lissu bado yuko hai. Vile vile kitendo cha yeye kwenda kumuona hakimfanyi awe innocent. Ni yeye pia ndiye aliyedai kuwa askari wao huwa hawakosi.

Ni yeye yeye aliyemfungulia kesi Mbowe na baadaye kumachia na kuja na hizo R4 ambazo zinampa shida kuzitekeleza. Ninachoweza kukubaliana na wewe ni kuwa anaonyesha ana nia nzuri .... ila watu wake behind the scene ndiyo wanamtoa kwenye reli. That is one possibility.

Another possibility ni kwamba madaraka yamemuingi kichwani sasa anataka kuendelea 2025 kwa kila hali ..... hata kwa damu ya wachache kumwagika ili mradi afanikiwe.
Unapokosa ushahidi wa moja kwa moja wa watu wa Samia kutaka kumuua Lissu au mwanasiasa yoyote unachokifanya ni hisia mbaya tu, ni kuendeleza negativity ya mitandaoni.

Mauaji yaliyochukua uhai wa mwanasiasa wa CHADEMA yanaweza kuwa ni masuala ya visasi vya kimapenzi, yanaweza kuwa ni masuala ya wivu wa kibiashara, mauaji ya binadamu huwa yana sababu nyingi na sio za kisiasa tu.

Marehemu kuwa mwanasiasa haimuondolei sifa za ubinadamu wake aliouishi kila siku enzi za uhai wake. Apumzike kwa amani.
 
Weka ushahidi wako wazi na kila mtu aone kwamba Rais Samia au JPM ndio alimuua fulani mtoto wa fulani.

Ukikosa ushahidi wa wazi hizo tuhuma zako zinabakia kuwa tuhuma tu, huwezi kuzipeleka mahakamani ukazitumia kama ushahidi unapofungua kesi.
Kaka hujanielewa, sijasema hao wameua na siwezi hata siku moja kusema hivyo. Kwa nihi unanukuu kitu sijasema

Nisome tena kile nimekiandika. Nimesema mabaya yakitokea basi tusijitoe akili, tuseme hili ni baya linapaswa kukomeshwa
 
Mheshimiwa SSH keshalaani hayo mauaji na ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike.
 
Unapokosa ushahidi wa moja kwa moja wa watu wa Samia kutaka kumuua Lissu au mwanasiasa yoyote unachokifanya ni hisia mbaya tu, ni kuendeleza negativity ya mitandaoni.

Mauaji yaliyochukua uhai wa mwanasiasa wa CHADEMA yanaweza kuwa ni masuala ya visasi vya kimapenzi, yanaweza kuwa ni masuala ya wivu wa kibiashara, mauaji ya binadamu huwa yana sababu nyingi na sio za kisiasa tu.

Marehemu kuwa mwanasiasa haimuondolei sifa za ubinadamu wake aliouishi kila siku enzi za uhai wake. Apumzike kwa amani.

Kwa hiyo visasi ni kwa wananchama wa CDM peke yao....!!? Kama ingekuwa ni hiyo ingekuwa inatokea randomly kwa kila mtu regardless chama. Halafu hao wenye mashangingi na maV80 na pingu wanasubiri tu revenge .... yah right.
 
Ubinadamu wa enzi za uhai wa marehemu haukwepeki, zipo kona nyingi za kujua ni nini haswa kilichosababisha wauwaji wakamuua.
 
Back
Top Bottom