Hata mimi nashangaa


Nyamayao, hapo sasa umsihi nduguyo asilete ushindani, manake mwisho wake si mwema asilani.
 

Hii mechi kweli ni kali inaelekea aitotoa mshindi bali itaishia kuwa droo pamoja na kuongeza dakika za nyongeza. WARNING - Aaangalie tu hicho kisasi anachotaka kulipa kwa mumwe kisije kikamrudia yeye mwenyewe halafu akadhalilika pili kwa wote kutoka nje ya ndoa yao naona tayari wameishajitia unajisi pia inawezekana kuletewa watoto waliotokana na infidelity na trend ndio inaelekea huko I do believe hayo maamuzi anayofanya mwanamke ni kutokana na hasira ila akae akijua kwamba unapojipanga kulipa kisasi kwa mwenzio fahamu fika kwamba kuna mengine makubwa yatakukuta
 
Hilo limdogo lako ambalo pia ni lidogo langu huko upstairs kuko vizuri?

Hebu ngoja nicheki kama kuna nafasi kule Mirembe then ntaku-call tujue la kufanya. Anahitaji tiba huyu binti. Ana matatizo makubwa sana ya Akili...:confused2::confused2:
 
huyo dogo kachemsha... utaratibu siku zote unasema mzigo wa safari lazma upakiwe na mwenye safari, amekua careless na bahati mbaya sana binti naye anonekana mchanga kwenye mambo ya mahusiano... siku zote ukihisi infidenlity cha kwanza ni kutulia na kumbana mwenza kuliko kupeleka mambo hayo nje, maana mwisho wa siku mkipatana mtashindwa hata kutoka pamoja kwasbabu tayari jamii inajua kwamba jamaa alipiga nje

lakini ndo hivyo tena yeshatokea, cha maana mama arudi, amweke jamaa karibu na wasort kwa mpangilio issues zao tena wakiwa wenyewe sio kuvuvuzela kitaa

the lady must appreciate that si rahisi kwa mwanaume kufungasha condom zilizotumika na chupi za wanawake kurudi nazo nyumbani...
 


Duu naona ngoma imepata mchezaji,ila huyu bibie naona anafanya makosa kama anarudi kwa mmewe kufanya revenge ni vyema aachane tu na hii ndoa . maamuzi yake sio sahihi hata kidogo.hapo kutakuwa hakuna mapenzi tena.Nyamayo kaa nae na umpe advice nzuri kuhusiana na ndoa pia mwambie akumbuke ukimwi unaua.
 

FL1 dada yangu.... Huku duniani kuna mianawake mijinga huwezi kuamini! Huyu naye hamnazo kabisa! Kwa taarifa yake anaweza akafanya huo upuuzi wake akatimuliwa na kimimba cha miezi tisa. Sijui atarudi kwa hiyo mijanaume mipumbavu isiyotumia akili wala kondom kumega wake za watu? Tusubiri, haitapita muda nyamayao atatuletea msambaratiko wa hii ndoa. Na mwisho wa siku atakayelia ni MWANAMKE!
 

Kuliko arudi akiwa na fikra hizo ni bora asirudi..
 

Nafikiri Hilo liwe between Man and Wife talk..........Tume ya usuluhishi isiitwe, I mean wakihusishwa watu ni aibu after mapatano.

Situation iko tense as we can all see, but Ni dhahiri hata malaya wa aina ganni asingeweza kuacha hizo clue as he was going back home, I was away some few days, yes kuna situation wahudumu (kujifanya wana jali wateja ) waka assist ku pack.

Nafikiri Mke arudi home and ajaribu kuielewa situation and aipe muda, She cant be fooled all the time. Na huwezijua who is behind that (Dunia imeharibika) Kunaweza kukawa na mtu wa tatu or Wanne hapo!!

Nawasilisha:
 

ndugu yangu weee mie naongea nae kwenye fone, ni mpaka hapo nitakapopata chance ya kuja huko, jana aliongea na dadake(my frnd) na mama, nackia mama amembembeleza sana na kumuomba sana acfanye hiko kitendo lakini ndio kasema hayo ndio maamuzi yake ya mwisho, mie nilivyoongea nae nilimwambia bora ucrudi kama uamuzi wake ndio huo, analia tu anasema sasa hivi ndio tunamwambia ndoa ndio zilivyo, cjui ndio wanaume, kwanini hatukumwambia hayo mwanzoni hata acngeingia kwenye kitu kinachoitwa ndoa, yaani hatuelewani kabisa kwenye fone kwa jinc anavyolia...anasema ni lazima na yeye amuonyeshe maumivu ya kutendwa yanavyokuwa hata miaka 20 ijayo yeye hana shida labda tu mume acjue kama kachezewa rafu lakini atakapojua yeye hana shida atamwambia ndio malipo ya uliyonifanyia wakati ule......mie jamani nachoka kabisa.
 
sasa huyu mbaya wake aliingiaje hotel kufanya yote hayo? au ndio huyu mhudumu alisetiwa afanye hivyo na kama ndivyo kwanini mhudumu ndio apaki nguo? yani amekuwa mzembe mpaka nguo apakiwe na mhudumu?

Binadamu hawaaminiki tena, mimi naweza kukuamini lakini sijui akili yako inawaza nini. Kwani wahudumu wanalipwa shillingi ngapi ili wasiweze kutumiwa? Unaweza kuwa mapokezi ukamtuma mtu akuchukulie bag chumbani, hawezi kutumia mwanya huo kufanya huo ubaya?
 

"nina kazi nzuri dada yangu, amenikuta nipo vizuri tu, nimempenda kwa dhati but kwanini anifantie haya? ctajutia uamuzi wangu kabisa coz uwezo wa kuwalea wanangu nitakuwa nao""
 

hilo analikubali, lakini anachotaka kuambiwa ukweli tu, kwamba mume ali cheat na kwa bahati mbaya aliyefanya nae matuc ndio kamuwekea hivyo virago ""hawezi kunidanganya hivi hivi nikiona, akubali ni kweli alibeba mwanamke au alipata huko huko mwanamke wa chap chap tuelewane tuongee yaishe, sio aone anaishi na mjinga wa kumdanganya kijinga kijinga hivi, yeye kaamua kuniona mie taahira kwa kukataa ishu iliyowazi kabisaa, sasa tutakomeshana""
 
"nina kazi nzuri dada yangu, amenikuta nipo vizuri tu, nimempenda kwa dhati but kwanini anifantie haya? ctajutia uamuzi wangu kabisa coz uwezo wa kuwalea wanangu nitakuwa nao""
Alivo mjinga anafikiri kuwa na kazi nzuri / kipato kizuri ndio supa gluu ya ndoa! Kama anajiona ana uwezo, nini kinamrudisha kwa mumewe? Si aanze maisha yake na kipato chake, ajibadilishie wanaume na mitarimbo tofauti, manake inaonyesha ndicho anachokipenda?

Mwanamke mwenye busara, utu, staha na heshima yake hawezi kujiapiza upumbavu kama huu.... Eti mumewe atamlelea watoto wa wanaume wengine, kama njia ya kulipiza kisasi! Ptuuuuu! na msonyo kwa juu!
 

Huo ndio ushauri maana akishangaa atakuta rafiki yake wa karibu kaingizwa ndani au mdada wa huku JF akimfahamu huyo mwanaume jinsi wanaume walivyoadimika hatachelewa kuchukua mchuma. Si atakuwa anasafiri naye ili asijiokotee wengine akiwa safarini?
 

Nyamayao, katika mazingira kama haya, unaweza kuapa mbele ya miungu ya kwenu na mbele ya Mungu mkuu, kuwa unathibitisha bila shaka yoyote kuwa huyu mume wa mdogo wako alifanya infidelity?
 
"nina kazi nzuri dada yangu, amenikuta nipo vizuri tu, nimempenda kwa dhati but kwanini anifantie haya? ctajutia uamuzi wangu kabisa coz uwezo wa kuwalea wanangu nitakuwa nao""

The bottom line...."HASIRA HASARA".
 

hizi ndoa bwana nazo zinachosha, mtu unaingia tu ili mradi umeingia, cjui ndio wanasema kutoa mkoc wala cjui, mie kwa kweli imebidi niache ishu waiongelee kifamilia zaidi coz kama binti hata mama yake mzazi kamwomba mpaka kumpigia magoti acjrfanya hicho kitendo na hajakubali kubadili uamuzi wake nani mwingine atamshauri akashaurika?...na kwasasa coz hiyo kitu ipo kichwani mwake anaweza kutuitikia kwamba hatafanya lakini nani anajua rohoni mwake?....ki ujumla hii ndoa imeshavunjika tayari.
 
hilo analikubali, lakini anachotaka kuambiwa ukweli tu, kwamba mume ali cheat na kwa bahati mbaya aliyefanya nae matuc ndio kamuwekea hivyo virago""

Akina mama bana sasa akubali kivp wkt yeye hajafanya?
Akubali kamega wkt hajamega inawezekana hiyo? Sasa anamlazimisha akubali?
Akikubali matokeo yatakuwa tofauti na yale anayo kataa?
 
Nyamayao, katika mazingira kama haya, unaweza kuapa mbele ya miungu ya kwenu na mbele ya Mungu mkuu, kuwa unathibitisha bila shaka yoyote kuwa huyu mume wa mdogo wako alifanya infidelity?

kaka yangu mpenzi, mie kwa kweli cwezi kudhibitisha lolote, cna kidhibiti mana mie nafanya kupigiwa na kupewa yanayojiri huko...na cwezi kusema labda mume ni kweli kafany ila kadanganya au hajafanya binti anamfikiria vibaya, naweza sema ukweli anao mume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…