Mkuu Genta huyo sidhani kama ni timamu kichwani na hata hao waandishi wanaomhoji kila siku nao nafikiri pia hawako timamu vichwani mwao. Haiwezekani mtu kila siku anazungumza pumba tu na uwongo wa wazi kabisa halafu kesho yake tena wanaenda kumhoji lazima anayehoji na anayehojiwa watakuwa wana matatizo kwenye vichwa vyao. Na huyo yupo hivyo halafu kila siku ndio huwa anajisifu mtandaoni bila aibu kuwa siku hizi ndio mshauri wa viongozi wa Simba wakati wowote anawapigia simu kuwapa ushauri. Halafu Simba ikifungwa mara tano na mtani wake na ikikosa kombe misimu minne watu wanalalamimika wanatafuta mchawi wakati upande wa pili washauri wa viongozi ni wakina Davis Mosha, Malegeri, Seif Magari, Ally Mayayi and the likes.
TCRA nao ifike mahali ipitishe rungu kwenye hizi TV za mtandaoni kama ilivyofyeka waandishi ambao hawakusomea kwenye redio na televisheni. Kuendelea kuziacha hizi TV zifanye kazi zikiwa zinarusha matangazo ya uwongo na vichwa vya habari tofauti na kilichomo ndani ya habari yenyewe ni janga kwa taifa. Na huu uozo sio kwa habari za michezo tu bali hata habari nyingine za kitaifa na kimataifa. Zisipodhibitiwa ipo siku zitakuja kuleta balaa nchini na wakati huo hakutakuwa na muda wa kurekebisha.