MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
Mwaka 2013-2014 wakati kesi ya Kenyatta na Rutto zinarindima kwenye mahakama ya uhalifu wa kimataifa (ICC-The Hague), njia kuu iliyotumika kuzima sakata ni kuharibu ushahidi kwa kuuficha, na kuua mashahidi wa muhimu. Katika hili wakina Kenyatta na Rutto walifanikiwa sana, japo pamoja na hayo mawakili wao walishitakiwa kwa kosa la kuchezea ushahidi (Evidence Tampering).
Bahati mbaya sanaaaaaa, kuanzia mwaka 2024 Ofisi ya Mwendesha Mashitaka (Office of the Prosecutor) chini ya Ibara ya 68 ya Mkataba wa Roma (Rome Statute) ilitengeneza kanuni mpya za kuwalinda mashahidi na kuchukua ushahidi bila kwenda mahakamani na shahidi kufahamika. Hizi kanuni zinaitwa: The OTP’s 2024 Guidelines on Remote and Protected Witness Interviews.
Hili liko tofauti kabisa na utamaduni wa kutoa ushahidi ambao nchi zinazotumia mfumo wa COMMON LAW kama Tanzania tunautumia. Ambapo ushahidi unatakiwa kuwa wa moja kwa moja (Direct), na utolewe na mhusika (Adduced by a witness) na nyaraka au vithibiti vifuate mlolongo maalumu ili vikubaliwe (Exhibits must have followed a proper chain of custody).
Hapa Tanzania mtu unaweza kukutwa umeua lakini endapo ikaja kufahamika kwamba kuna nyaraka haikupokelewa vizuri mahakamani, mfano nyaraka ya kumhoji shahidi basi kesi yote inapigwa chini. Mfano Mzuri ni kesi ya MKE WA BILIONEA MSUYA a.k.a Miriam Mrita, ambaye alikuwa anatuhumiwa kumuua wifi yake na ushahidi wote wa vinasaba(DNA Evidence) ulithibitika, lakini alikuja kuachiwa kwasababu kuu mbili tu:
Mosi, Damu ya kwenye kisu ilikuwa haijapimwa kuonesha kwamba ni ya marehemu,.
Pili, Nyaraka alizitumia kukiri makosa hazikufuata mwongozo wa Jaji Mkuu.
SASA kama mnajidanganya kwamba aliondoka yule Mama Waziri, Wakaondoka Madokta, na kipindi hiki mmeshikilia Bwana Yule, mnajidanganya sana. Kama ICC imeweza kukusanya taarifa za uhalifu wa kivita kule Ukraine na Gaza bila hata mashahidi kutoka Urusi na Palestina kwenda na wametengeneza kesi nzuri kabisa, sembuse Tanganyika hapa ???
2. Lazima tutengeneza mahakama maalumu ya uhalifu kuwashitaki hawa wahuni.
3. Lazima wahanga wote walipwe fidia kwa hasara walizozipata tokea 2025 hadi leo.
4. Lazima tuunde kamisheni za usuluhishi (Truth & Reconciliation Commission) kwa makosa ya kisiasa yalipelekea vurugu kutokea kabla ya Oktoba 2025. Kamisheni iwatambue wahanga wote na kuwataja majina yao. Lakini pia kuwatafuta waliokuwa wanapiga propaganda chafu ambazo zilichangia nchi kupoteza amani. Makada wa siasa, viongozi wa dini misimamo mikali na wafanyabiashara waliokuwa wanafadhili watu na vyombo vya habari katika kupiga hizi propaganda.
5. Taasisi za kiusalama kama TISS + TPDF+ PT zifanyiwe mabadiliko ya kisera na kumfumo, kuhakikisha tunaondoa mamluki na kurudisha hivi vyombo kwenye mikono ya raia kama ilivyokuwa mwaka 1964, 1975, 1983 na 1996. Hizi taasisi zinafanya kazi kama mali binafsi ya CCM (Hasahasa Jakaya Kikwete), Wafanyabiashara wakubwa kama (Rostam, GSM,) na Viongozi wa dini (hasahasa wale wa Kikatoliki na Kiislamu) kwasababu maafisa wengi (recruits) ni vijana wao wa seminary au madrasa.
6. Mkishindwa kufanya haya basi aidha wahusika WAJIUZULU au WAKIMBILIE UARABUNI au WAWAKABIDHI NCHI MABEBERU au WAKUBALI JAHAZI LIZAME ambapo mambo yatachafuka kupita kiasi na tutaumia wote wakiwemo wao na watoto zao. Ile mishahara minono haitakuwepo tena maana kila mtu atakuwa analia kivyake kutokana na machafuko makubwa na anguko la kisiasa na kiuchumi.
================================
RUTTO na KENYETTA walipona na ICC kwasababu kubwa zifuatazo:
1. Walifanya makosa wakiwa siyo viongozi wakuu wa nchi kama hapa kwetu.
2. Yale mauaji hayakufadhiliwa na serikali ya Mzee Kibaki (Not State Sponsored).
3. Kenya kiujumla iliacha kufuatiliwa kwasababu walikubali mabadiliko ya kisiasa.
4. Nchini Kenya, Ukabila ndiyo unaendesha serikali hapa Tanzania ni kinyume chake.
================================
Hapa Tanzania kadiri siku zinavyoenda ndiyo serikali inazidi kuwa na watu WAJINGA na WAPUMBAVU, ambao wanaamini kabisa kwamba wanaweza kumwaga damu za maelfu ya watu na jambo lolote lile lisitokee. Kwamba hawawezi kutufanya chochote (Sawa inawezekana), lakini hata yule aliyewaumba naye asifanye chochote kweli ???
Hata kama MUUMBA hatawafanya chochote, mnaamini kwamba hata SHETANI naye atawaacha hivihivi, bila kulipia gharama yoyote ile ???
Mwaka 1905 kuna mapinduzi yalifeli nchini Urusi, na shirika la kijasusi la nchi hiyo The OKRANA liliwashughulikia kwelikweli wakina Lenin na wajamaa. Waliamini kabisa yameisha, ila kufika Oktoba 1917, mambo yalibadilika kwelikweli Urusi ikiwa na hali mbaya kiuchumi mapinduzi yalifanyika kiurahisi mno. Maelfu ya watawala walichinjwa kama kuku na wakomunisti wa Kiyahudi ambao walikuwa wanalipiza kisasi cha miaka mingi ya mateso chini ya familia ya Ramanov (The Ramanov Dynasty).
Vladmir Lenin alitoa amri ya kumuua Mfalme Nicholas Ramanov II na familia yake yoteee, kisa tu kisirani kwamba kaka yake Alexandr Lenin alinyongwa na Mfalme Alexander III wa Urusi ambaye ni baba yake na Nicholas Ramanov II.
===============================
Wale wenye macho, dalili zote za mvua kubwa yenye dhoruba zinaoneka tayari hapa nchini ila watawala ndiyo hamtaki kukubaliana nazo. Hadi kufika tarehe 29 Oktoba 2025, saa mbili asubuhi Maafisa Usalama, Makada wa CCM, Polisi na Wanajeshi walikuwa wakiamini kwamba watanganyika hawawezi kufanya lolote lile nchini, ila ndani ya masaa mawili nchi iliingia kwenye umwagikaji damu mkubwa kuwahi kutokea kwenye historia.
SASA ENDELEENI KUSHUPAZA SHINGO.....
Huko Msoga hamtakaa,
Huko Kizimkazi hamtakaa,
Huko Marekani hamtakimbilia,
Huko Uingereza hamtakimbilia,
Mtakimbilia Uarabuni kama Nduli Idd Amini......
===============================
SISI yetu MACHO
Bahati mbaya sanaaaaaa, kuanzia mwaka 2024 Ofisi ya Mwendesha Mashitaka (Office of the Prosecutor) chini ya Ibara ya 68 ya Mkataba wa Roma (Rome Statute) ilitengeneza kanuni mpya za kuwalinda mashahidi na kuchukua ushahidi bila kwenda mahakamani na shahidi kufahamika. Hizi kanuni zinaitwa: The OTP’s 2024 Guidelines on Remote and Protected Witness Interviews.
Mwaka 2024 hasahasa baada ya kilichokuwa kinatokea Ukraine na Palestina, ICC walitengeneza kanuni maalumu ambazo zitamuwezesha Mwendesha Mashitaka (Prosecutor) kukusanya ushahidi popote pale ambapo anapafahamu yeye na kuupeleka mahakamani bila hata ya shahidi kuwepo, mradi tu uwe ushahidi halali na umefuata utaratibu. Hapa inamaanisha hata kama leo mtamkamata mtu fulani na kumuweka kizuizini au hata kumuua, lakini kama alishapeleka huo ushahidi kwa Mwendesha Mashitaka (ICC) basi lazima itakula kwako.Hili liko tofauti kabisa na utamaduni wa kutoa ushahidi ambao nchi zinazotumia mfumo wa COMMON LAW kama Tanzania tunautumia. Ambapo ushahidi unatakiwa kuwa wa moja kwa moja (Direct), na utolewe na mhusika (Adduced by a witness) na nyaraka au vithibiti vifuate mlolongo maalumu ili vikubaliwe (Exhibits must have followed a proper chain of custody).
Hapa Tanzania mtu unaweza kukutwa umeua lakini endapo ikaja kufahamika kwamba kuna nyaraka haikupokelewa vizuri mahakamani, mfano nyaraka ya kumhoji shahidi basi kesi yote inapigwa chini. Mfano Mzuri ni kesi ya MKE WA BILIONEA MSUYA a.k.a Miriam Mrita, ambaye alikuwa anatuhumiwa kumuua wifi yake na ushahidi wote wa vinasaba(DNA Evidence) ulithibitika, lakini alikuja kuachiwa kwasababu kuu mbili tu:
Mosi, Damu ya kwenye kisu ilikuwa haijapimwa kuonesha kwamba ni ya marehemu,.
Pili, Nyaraka alizitumia kukiri makosa hazikufuata mwongozo wa Jaji Mkuu.
SASA kama mnajidanganya kwamba aliondoka yule Mama Waziri, Wakaondoka Madokta, na kipindi hiki mmeshikilia Bwana Yule, mnajidanganya sana. Kama ICC imeweza kukusanya taarifa za uhalifu wa kivita kule Ukraine na Gaza bila hata mashahidi kutoka Urusi na Palestina kwenda na wametengeneza kesi nzuri kabisa, sembuse Tanganyika hapa ???
LINGINE BAYA: Tofauti kabisa na mahakama nyingine za duniani, ICC-The Hague ndiyo mahakama pekee ambayo inaruhusiwa kutumia ushahidi kutoka kwenye vyombo vya habari, ripoti za kiuchunguzi kutoka mashirika makubwa ya haki za binadamu (Amnesty International, Human Rights Watch) na ripoti maalumu za kijasusi (Intelligence Reports). Hivyo leo hii kama watu wakiamua tu kutukomalia, mbona ushahidi mwingi utafika huko duniani, tena hadi yale ya chumbani ambayo mnaamini yamefichwa yatafika.==================================
SASA KUPUNGUZA MATATIZO YAJAYO YA KUINGILIWA NA MABABERU:
1. Lazima watu wawajibishwe, hasa maafisa wa TISS+CCM+PT+JWTZ.SASA KUPUNGUZA MATATIZO YAJAYO YA KUINGILIWA NA MABABERU:
2. Lazima tutengeneza mahakama maalumu ya uhalifu kuwashitaki hawa wahuni.
3. Lazima wahanga wote walipwe fidia kwa hasara walizozipata tokea 2025 hadi leo.
4. Lazima tuunde kamisheni za usuluhishi (Truth & Reconciliation Commission) kwa makosa ya kisiasa yalipelekea vurugu kutokea kabla ya Oktoba 2025. Kamisheni iwatambue wahanga wote na kuwataja majina yao. Lakini pia kuwatafuta waliokuwa wanapiga propaganda chafu ambazo zilichangia nchi kupoteza amani. Makada wa siasa, viongozi wa dini misimamo mikali na wafanyabiashara waliokuwa wanafadhili watu na vyombo vya habari katika kupiga hizi propaganda.
5. Taasisi za kiusalama kama TISS + TPDF+ PT zifanyiwe mabadiliko ya kisera na kumfumo, kuhakikisha tunaondoa mamluki na kurudisha hivi vyombo kwenye mikono ya raia kama ilivyokuwa mwaka 1964, 1975, 1983 na 1996. Hizi taasisi zinafanya kazi kama mali binafsi ya CCM (Hasahasa Jakaya Kikwete), Wafanyabiashara wakubwa kama (Rostam, GSM,) na Viongozi wa dini (hasahasa wale wa Kikatoliki na Kiislamu) kwasababu maafisa wengi (recruits) ni vijana wao wa seminary au madrasa.
6. Mkishindwa kufanya haya basi aidha wahusika WAJIUZULU au WAKIMBILIE UARABUNI au WAWAKABIDHI NCHI MABEBERU au WAKUBALI JAHAZI LIZAME ambapo mambo yatachafuka kupita kiasi na tutaumia wote wakiwemo wao na watoto zao. Ile mishahara minono haitakuwepo tena maana kila mtu atakuwa analia kivyake kutokana na machafuko makubwa na anguko la kisiasa na kiuchumi.
================================
1. Walifanya makosa wakiwa siyo viongozi wakuu wa nchi kama hapa kwetu.
2. Yale mauaji hayakufadhiliwa na serikali ya Mzee Kibaki (Not State Sponsored).
3. Kenya kiujumla iliacha kufuatiliwa kwasababu walikubali mabadiliko ya kisiasa.
4. Nchini Kenya, Ukabila ndiyo unaendesha serikali hapa Tanzania ni kinyume chake.
================================
Hata kama MUUMBA hatawafanya chochote, mnaamini kwamba hata SHETANI naye atawaacha hivihivi, bila kulipia gharama yoyote ile ???
Mwaka 1905 kuna mapinduzi yalifeli nchini Urusi, na shirika la kijasusi la nchi hiyo The OKRANA liliwashughulikia kwelikweli wakina Lenin na wajamaa. Waliamini kabisa yameisha, ila kufika Oktoba 1917, mambo yalibadilika kwelikweli Urusi ikiwa na hali mbaya kiuchumi mapinduzi yalifanyika kiurahisi mno. Maelfu ya watawala walichinjwa kama kuku na wakomunisti wa Kiyahudi ambao walikuwa wanalipiza kisasi cha miaka mingi ya mateso chini ya familia ya Ramanov (The Ramanov Dynasty).
Vladmir Lenin alitoa amri ya kumuua Mfalme Nicholas Ramanov II na familia yake yoteee, kisa tu kisirani kwamba kaka yake Alexandr Lenin alinyongwa na Mfalme Alexander III wa Urusi ambaye ni baba yake na Nicholas Ramanov II.
Kule Uchina nako ilikuwa hivihivi: General Chiang Kai Shek aliua maelfu ya wakomunisti bila huruma akitegemea kukingiwa kifua na Marekani, Ufaransa na Uingereza, mataifa ambayo yalikuwa yamewekeza kwa wingi nchini Uchina. Alikuwa anachinja watu, halafu lawama zikija anatumia ule uwekezaji kuwanyamazisha mabeberu. Akawa anahonga rasilimali za nchi kwa mabeberu ili aendelee kutawala. Nchi iliingia kwenye mdororo wa kiuchumi na kina Mao Zedong na wenzake wakambananisha kwenye kona. Waliipindua serikali iliyokuwa na jeshi lenye nguvu ambalo lilikuwa limatoka kupigana vita ya pili ya dunia (A Battle-Hardened Force).===============================