PostGE2025 Hata mkiua mashahidi kama Kenyatta na Rutto walivyofanya mwaka 2014, hamuwezi kupona mwaka 2026

PostGE2025 Hata mkiua mashahidi kama Kenyatta na Rutto walivyofanya mwaka 2014, hamuwezi kupona mwaka 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hadi kufika tarehe 29 Oktoba 2026, saa mbili asubuhi Maafisa Usalama, Makada wa CCM, Polisi na Wanajeshi walikuwa wakiamini kwamba watanganyika hawawezi kufanya lolote lile nchini, ila ndani ya masaa mawili nchi iliingia kwenye umwagikaji damu mkubwa kuwahi kutokea kwenye historia.


🙌
Hiyo siku acha kabisa....
Nahisi Watanzania walikula bangi....

Sio kwa kishindo kile... Kuna Mama mmoja muuza mihogo... Yeye kazi Yale ilikuwa kubeba mawe makubwa na kuyapanga barabarani... Leo ukimwambia yabebe hawezi...

Watu walikuwa na hasira sijawahi kushuhudia.... Kulikuwa na shule ya msingi ndani Kuna kituo Cha kupiga kura...kilifungwa saa 6 mchana ...na wale wote kwenye vituo walipotea kusiko fahamika... Fikiria kituo Cha kupiga kura na kina askari ..lakini hakuna hata mmoja alibaki...
 
4. Lazima tuunde kamisheni za usuluhishi (Truth & Reconciliation Commission) kwa makosa ya kisiasa yalipelekea vurugu kutokea kabla ya Oktoba 2025..
Hili hawathubutu.
Wangekuwa na fikra za hivi wasingekuja na ule UONGO wa tume ya chawa Chande
 
Mwaka 2013-2014 wakati kesi ya Kenyatta na Rutto zinarindima kwenye mahakama ya uhalifu wa kimataifa (ICC-The Hague), njia kuu iliyotumika kuzima sakata ni kuharibu ushahidi kwa kuuficha, na kuua mashahidi wa muhimu. Katika hili wakina Kenyatta na Rutto walifanikiwa sana, japo pamoja na hayo mawakili wao walishitakiwa kwa kosa la kuchezea ushahidi (Evidence Tampering).

Bahati mbaya sanaaaaaa, kuanzia mwaka 2024 Ofisi ya Mwendesha Mashitaka (Office of the Prosecutor) chini ya Ibara ya 68 ya Mkataba wa Roma (Rome Statute) ilitengeneza kanuni mpya za kuwalinda mashahidi na kuchukua ushahidi bila kwenda mahakamani na shahidi kufahamika. Hizi kanuni zinaitwa: The OTP’s 2024 Guidelines on Remote and Protected Witness Interviews.
​
Mwaka 2024 hasahasa baada ya kilichokuwa kinatokea Ukraine na Palestina, ICC walitengeneza kanuni maalumu ambazo zitamuwezesha Mwendesha Mashitaka (Prosecutor) kukusanya ushahidi popote pale ambapo anapafahamu yeye na kuupeleka mahakamani bila hata ya shahidi kuwepo, mradi tu uwe ushahidi halali na umefuata utaratibu. Hapa inamaanisha hata kama leo mtamkamata mtu fulani na kumuweka kizuizini au hata kumuua, lakini kama alishapeleka huo ushahidi kwa Mwendesha Mashitaka (ICC) basi lazima itakula kwako.

Hili liko tofauti kabisa na utamaduni wa kutoa ushahidi ambao nchi zinazotumia mfumo wa COMMON LAW kama Tanzania tunautumia. Ambapo ushahidi unatakiwa kuwa wa moja kwa moja (Direct), na utolewe na mhusika (Adduced by a witness) na nyaraka au vithibiti vifuate mlolongo maalumu ili vikubaliwe (Exhibits must have followed a proper chain of custody).

Hapa Tanzania mtu unaweza kukutwa umeua lakini endapo ikaja kufahamika kwamba kuna nyaraka haikupokelewa vizuri mahakamani, mfano nyaraka ya kumhoji shahidi basi kesi yote inapigwa chini. Mfano Mzuri ni kesi ya MKE WA BILIONEA MSUYA a.k.a Miriam Mrita, ambaye alikuwa anatuhumiwa kumuua wifi yake na ushahidi wote wa vinasaba(DNA Evidence) ulithibitika, lakini alikuja kuachiwa kwasababu kuu mbili tu:

Mosi, Damu ya kwenye kisu ilikuwa haijapimwa kuonesha kwamba ni ya marehemu,.
Pili, Nyaraka alizitumia kukiri makosa hazikufuata mwongozo wa Jaji Mkuu.

SASA kama mnajidanganya kwamba aliondoka yule Mama Waziri, Wakaondoka Madokta, na kipindi hiki mmeshikilia Bwana Yule, mnajidanganya sana. Kama ICC imeweza kukusanya taarifa za uhalifu wa kivita kule Ukraine na Gaza bila hata mashahidi kutoka Urusi na Palestina kwenda na wametengeneza kesi nzuri kabisa, sembuse Tanganyika hapa ???
​
LINGINE BAYA: Tofauti kabisa na mahakama nyingine za duniani, ICC-The Hague ndiyo mahakama pekee ambayo inaruhusiwa kutumia ushahidi kutoka kwenye vyombo vya habari, ripoti za kiuchunguzi kutoka mashirika makubwa ya haki za binadamu (Amnesty International, Human Rights Watch) na ripoti maalumu za kijasusi (Intelligence Reports). Hivyo leo hii kama watu wakiamua tu kutukomalia, mbona ushahidi mwingi utafika huko duniani, tena hadi yale ya chumbani ambayo mnaamini yamefichwa yatafika.
==================================

SASA KUPUNGUZA MATATIZO YAJAYO YA KUINGILIWA NA MABABERU:

​
1. Lazima watu wawajibishwe, hasa maafisa wa TISS+CCM+PT+JWTZ.

2. Lazima tutengeneza mahakama maalumu ya uhalifu kuwashitaki hawa wahuni.

3. Lazima wahanga wote walipwe fidia kwa hasara walizozipata tokea 2025 hadi leo.

4. Lazima tuunde kamisheni za usuluhishi (Truth & Reconciliation Commission) kwa makosa ya kisiasa yalipelekea vurugu kutokea kabla ya Oktoba 2025. Kamisheni iwatambue wahanga wote na kuwataja majina yao. Lakini pia kuwatafuta waliokuwa wanapiga propaganda chafu ambazo zilichangia nchi kupoteza amani. Makada wa siasa, viongozi wa dini misimamo mikali na wafanyabiashara waliokuwa wanafadhili watu na vyombo vya habari katika kupiga hizi propaganda.

5. Taasisi za kiusalama kama TISS + TPDF+ PT zifanyiwe mabadiliko ya kisera na kumfumo, kuhakikisha tunaondoa mamluki na kurudisha hivi vyombo kwenye mikono ya raia kama ilivyokuwa mwaka 1964, 1975, 1983 na 1996. Hizi taasisi zinafanya kazi kama mali binafsi ya CCM (Hasahasa Jakaya Kikwete), Wafanyabiashara wakubwa kama (Rostam, GSM,) na Viongozi wa dini (hasahasa wale wa Kikatoliki na Kiislamu) kwasababu maafisa wengi (recruits) ni vijana wao wa seminary au madrasa.

6. Mkishindwa kufanya haya basi aidha wahusika WAJIUZULU au WAKIMBILIE UARABUNI au WAWAKABIDHI NCHI MABEBERU au WAKUBALI JAHAZI LIZAME ambapo mambo yatachafuka kupita kiasi na tutaumia wote wakiwemo wao na watoto zao. Ile mishahara minono haitakuwepo tena maana kila mtu atakuwa analia kivyake kutokana na machafuko makubwa na anguko la kisiasa na kiuchumi.

================================
​
RUTTO na KENYETTA walipona na ICC kwasababu kubwa zifuatazo:

1. Walifanya makosa wakiwa siyo viongozi wakuu wa nchi kama hapa kwetu.
2. Yale mauaji hayakufadhiliwa na serikali ya Mzee Kibaki (Not State Sponsored).
3. Kenya kiujumla iliacha kufuatiliwa kwasababu walikubali mabadiliko ya kisiasa.
4. Nchini Kenya, Ukabila ndiyo unaendesha serikali hapa Tanzania ni kinyume chake.

================================
​
Hapa Tanzania kadiri siku zinavyoenda ndiyo serikali inazidi kuwa na watu WAJINGA na WAPUMBAVU, ambao wanaamini kabisa kwamba wanaweza kumwaga damu za maelfu ya watu na jambo lolote lile lisitokee. Kwamba hawawezi kutufanya chochote (Sawa inawezekana), lakini hata yule aliyewaumba naye asifanye chochote kweli ???

Hata kama MUUMBA hatawafanya chochote, mnaamini kwamba hata SHETANI naye atawaacha hivihivi, bila kulipia gharama yoyote ile ???

Mwaka 1905 kuna mapinduzi yalifeli nchini Urusi, na shirika la kijasusi la nchi hiyo The OKRANA liliwashughulikia kwelikweli wakina Lenin na wajamaa. Waliamini kabisa yameisha, ila kufika Oktoba 1917, mambo yalibadilika kwelikweli Urusi ikiwa na hali mbaya kiuchumi mapinduzi yalifanyika kiurahisi mno. Maelfu ya watawala walichinjwa kama kuku na wakomunisti wa Kiyahudi ambao walikuwa wanalipiza kisasi cha miaka mingi ya mateso chini ya familia ya Ramanov (The Ramanov Dynasty).

Vladmir Lenin alitoa amri ya kumuua Mfalme Nicholas Ramanov II na familia yake yoteee, kisa tu kisirani kwamba kaka yake Alexandr Lenin alinyongwa na Mfalme Alexander III wa Urusi ambaye ni baba yake na Nicholas Ramanov II.
​
Kule Uchina nako ilikuwa hivihivi: General Chiang Kai Shek aliua maelfu ya wakomunisti bila huruma akitegemea kukingiwa kifua na Marekani, Ufaransa na Uingereza, mataifa ambayo yalikuwa yamewekeza kwa wingi nchini Uchina. Alikuwa anachinja watu, halafu lawama zikija anatumia ule uwekezaji kuwanyamazisha mabeberu. Akawa anahonga rasilimali za nchi kwa mabeberu ili aendelee kutawala. Nchi iliingia kwenye mdororo wa kiuchumi na kina Mao Zedong na wenzake wakambananisha kwenye kona. Waliipindua serikali iliyokuwa na jeshi lenye nguvu ambalo lilikuwa limatoka kupigana vita ya pili ya dunia (A Battle-Hardened Force).

===============================
​
Wale wenye macho, dalili zote za mvua kubwa yenye dhoruba zinaoneka tayari hapa nchini ila watawala ndiyo hamtaki kukubaliana nazo. Hadi kufika tarehe 29 Oktoba 2025, saa mbili asubuhi Maafisa Usalama, Makada wa CCM, Polisi na Wanajeshi walikuwa wakiamini kwamba watanganyika hawawezi kufanya lolote lile nchini, ila ndani ya masaa mawili nchi iliingia kwenye umwagikaji damu mkubwa kuwahi kutokea kwenye historia.

SASA ENDELEENI KUSHUPAZA SHINGO.....

Huko Msoga hamtakaa,
Huko Kizimkazi hamtakaa,
Huko Marekani hamtakimbilia,
Huko Uingereza hamtakimbilia,
Mtakimbilia Uarabuni kama Nduli Idd Amini......
===============================

SISI yetu MACHO
​

Nyarandu yuko DC anakula pesa kwa kupiga picha na viongoxi fake. Hivi kweli kuonana na Rudy Giuliani kunaweza kuisaidiaje nchi....!!? Huu ni utapeli wa hali ya juu.
 
29th October ni laana isiyofutika bila toba ya kweli. Taifa halitapona kiujanja ujanja! Kuna gharama lazima tulipe za kiuwajibikaji na kuombana msamaha na maridhiano. Tusizidi kuchelewa wote tutaumia kuanzia chini hadi juu.
 
Nchi badala ya kwenda mbele inarudi nyuma kwa reverse kali.
 
Mkuu hongera lkn ❗️

Mkuu jambo moja au mawili ujatutendea Haki
1)
Umesema viongozi kina Ruto na Uhuru Kenyata hawakuwa na
nguvu ya uhongozi

Swali kwanini usingesema tu kunyoosha maneno kwamba❗️
1 William Rutto
2 uhuru Kenyata

Walikuwa ni Viongozi wa Upinzani ndiyo walibebeshwa dhima ya yale Mauaji ya watu zaidi ya 1000+ na Mahakama ya ICC 👈

2
Mwaibaki akiwa ndiyo Rais mtetezi hakushtakiwa👈

kwakuwa hakuusika kushawashi zile Fujo👈

badala yake yeye jukumu lake lilikuwa kutuliza zile Fujo kurudisha Amani kwa Wote pale Kenya 👈

Tukiwa wakweli kile kimetokea Kenya haki
ametimiza jukumu la Kurejesha Amani kwa Binadamu wote na viumbe wote ndani ya Jamhuri
Ametimiza jukumu kwa kuua Maelfu ya Watanganyika...??? Na hakuanza kuua hiyo Oct 29 alianza kuua miaka mitatu nyuma...

Unaongea nini wewe????
 
Kudai mambo ya Sheria za Uchaguzi na kuchoma Miundombinu vinausikaje tena mpaka ya watu Binafsi

Sitaki siku moja kuamka kuambiwa hatuna Airport hatuna Bandari hatuna Chochote

Jielekezeni Mahakamani kudai mambo ya Uchaguzi nk

sio kwenye Miundombinu ya Watanzania wote hapana❌️

Risasi ndio dawa ya kiburi ✍️
Rubbish..... Pathetic fool
 
Familia za Msoga na Kizimkazi lazima zitalipa tu, yale mauaji yaligusa maelfu ya familia za watu nchini.
 
MAELEZO
KENYA
Baada ule Uchaguzi kukatokea Mauaji makubwa Wakafa Wakenya
1000+

Haikushutumiwa Serikali ya Mwaikibaki ❌️

Wala Vyombo vya Usalama ❌️


Pamoja na kufa watu 1000+

Badala yake Mahakamani ya ICC
Baada ya Uchaguzi Wakatakiwa kwenda kujibu Mashitaka pale ICC ni
WAPINZANI
Kipindi kile WAPINZANI walikuwa ndiyo kina

1) William Rutto
2) Uhuru Kenyata
3) Martha karua

Awa juu🖕 ndiyo ICC imewaita
Sababu kuu ndio Wachochezi yale Mauaji ya watu 1000+ kuna mpaka mgerugezi mmoja wa media nayeye kaitwa ICC kwa kuchangia kusambaza Chuki za Uchochezi ✍️
 
Tanzania wamekufa watu 500+

KENYA 1000+

RAIS wa KENYA wa kipindi kile rip Mwaibaki hakutakiwa na ICC
Wala Mkuu yoyote wa kiusalama

WAPINZANI Tanzania ambayo kimsingi ndiyo chanzo kikuu cha Mo29
Wanakwambia Muuaji ni Samia
Na kapicha chao cha KUEDIT

Ndiomana Lissu anakunya Lupango
Mwaka sasa nanusu
Yeye ndio chanzo cha Mo29
Anaendelea kunyea Lupango muda mrefu
Mpaka hapate msamaha wa Rais uruma ya Rais

Hajaonewa na yoyote ni upumbavu
Kudai kaonewa

Wkt Yeye mwenyewe
kwenye clip yake kaongea wazi na kitendo anachofanya ni UHAINI
wewe ile clip ujaisikia akiongea

Sasa kama yeye ni
Mwanasheria kakili ni Uhaini

Kwanini wewe unaona
kaonewa ?????

Ukipanda Mpunga utavuna
Mpunga

Mimi sina chuki na mh Lissu
Siku zote nasema kweli mimi sijaumbwa kuwa muongo muongo kama baadhi yenu

Kaonewa uku tumezika
watoto😭 wetu na wengine😭 500+

Watoto wa Lissu wapo wanasoma uko Marekani 🫡

Uruma zengine ni Upumbavu kuutunza kichwani mwako kule Jamhuri imemueka kivyovyote atajifunza kitu lee .

Leo mnaona MAHAKAMANI yeye anayakataa maneno yake mwenyewe tunapaswa kushukuru Jamhuri yetu

Ingekuwa na Uruma
kama yako
uyu mh Lissu tujue anaweza kuratibu tukio lengine kama lile upya siku za mbele❗️

pengine utakufa wewe sasa na Uruma yako✍️
 
Ukiwa mkweli ujue wapo watakuchukia bado kiasi kutamani wakuue tu!!
 
Tanzania wamekufa watu 500+

KENYA 1000+

RAIS wa KENYA wa kipindi kile rip Mwaibaki hakutakiwa na ICC
Wala Mkuu yoyote wa kiusalama

WAPINZANI Tanzania ambayo kimsingi ndiyo chanzo kikuu cha Mo29
Wanakwambia Muuaji ni Samia
Na kapicha chao cha KUEDIT

Ndiomana Lissu anakunya Lupango
Mwaka sasa nanusu
Yeye ndio chanzo cha Mo29
Anaendelea kunyea Lupango muda mrefu
Mpaka hapate msamaha wa Rais uruma ya Rais

Hajaonewa na yoyote ni upumbavu
Kudai kaonewa

Wkt Yeye mwenyewe
kwenye clip yake kaongea wazi na kitendo anachofanya ni UHAINI
wewe ile clip ujaisikia akiongea

Sasa kama yeye ni
Mwanasheria kakili ni Uhaini

Kwanini wewe unaona
kaonewa ?????

Ukipanda Mpunga utavuna
Mpunga

Mimi sina chuki na mh Lissu
Siku zote nasema kweli mimi sijaumbwa kuwa muongo muongo kama baadhi yenu

Kaonewa uku tumezika
watoto😭 wetu na wengine😭 500+

Watoto wa Lissu wapo wanasoma uko Marekani 🫡

Uruma zengine ni Upumbavu kuutunza kichwani mwako kule Jamhuri imemueka kivyovyote atajifunza kitu lee .

Leo mnaona MAHAKAMANI yeye anayakataa maneno yake mwenyewe tunapaswa kushukuru Jamhuri yetu

Ingekuwa na Uruma
kama yako
uyu mh Lissu tujue anaweza kuratibu tukio lengine kama lile upya siku za mbele❗️

pengine utakufa wewe sasa na Uruma yako✍️
Watu kama nyie ndiyo mnaofanya ccm idharaulike
 
Back
Top Bottom