PostGE2025 Hata mkiua mashahidi kama Kenyatta na Rutto walivyofanya mwaka 2014, hamuwezi kupona mwaka 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hao ICC wanachelewa nini? Si waanze sasa kufanya hayo mambo. Hao nao wanatoa matumani hewa tu.
Mmmh
 
Hata msipokubaliana na mimi hakuna kitakachobadilika kwasababu Tanzania haina utofauti na mataifa mengine duniani. Aidha wajiuzulu, wakimbie nchi, wawape nchi mabeberu kama Nigeria au Jahazi lizame halafu tugeuka kuwa kama Kongo.

Hakuna mbadala wa hili....
​
 
Duh! Mada ndeeeefu...
Waonaje ukaingia kuyatekeleza tu hayo matakwa yako?
 
gentleman,
huna haja ya kunialika kwenye mjadala wa porojo useless kama hizo mezani plz 🐒
Zama zimebadilika mzee, umebaki muda mdogo. Polepole alikuwa haamini angeweza kutekwa na kupotezwa. Juzi ukaja na nyuzi za kumpamba Nchimbi. Saa hii hata hutaki kuona jina lake. Hizo ni dalili za awali tu za kinachokuja mbele.
 
Kila nikiiangalia sakata la venezuela , marekani , netanyahu na mwenendo wao dhidi ya icc naona kusupport foreign influence ni kuzidi kudidimia
Kabisa na kuna mifano zaidi ya elfu moja hao anasema watatusaidia wana agenda zao kwa maslahi yao

Hawa Wahuni tuna wamudu wenyewe sio kumtegemea Mungu wala Mzungu
 
Zama zimebadilika mzee, umebaki muda mdogo. Polepole alikuwa haamini angeweza kutekwa na kupotezwa. Juzi ukaja na nyuzi za kumpamba Nchimbi. Saa hii hata hutaki kuona jina lake. Hizo ni dalili za awali tu za kinachokuja mbele.
Gentleman,
siasa ni sayansi,
don't be confused by political dynamics globally
 
Kila nikiiangalia sakata la venezuela , marekani , netanyahu na mwenendo wao dhidi ya icc naona kusupport foreign influence ni kuzidi kudidimia
Watanganyika huwa tunakuwaga wanafiki sana. Nadhani ni moja kati ya tabia mbovu-mbovu ambazo Baba wa Taifa alitufundisha. Kiufupi, huwezi kuongoza nchi bila Foreign Influence. Huwezi kabisa. Na ni ujinga wa hali ya juu kuamini kwamba unaweza kuongoza nchi bila Foreign Influence. JPM alijaribu nchi ikamshinda:

Tanzania tokea kipindi cha Nyerere ilikuwa inaishi kwa Foreign Influence. Uhuru wa Tanganyika umepatikana kwasababu kulikuwa kuna mataifa na mashirika ya Magharibi (The Fabian Society, The Vatican, USA, USSR) yaliyotusaidia msaada wa hali na mali. Hivyo huwezi kukimbia Foreign Influence, ambacho unatakiwa kukikmbia ni Malignant-Unlimited-Foreign Influence ambayo hata kipindi hiki bado ipo na inafanywa sana na mataifa ya Kiarabu wakiwatumia Waislamu kwa kuwarubuni. AU mataifa ya Magharibi yakiwatumia wafanyabiashara wakubwa, NGO's na taasisi za dini ya Kikristo.

Sambamba na hilo: Huwezi kulalamika kuingiliwa na watu wa nje ilhali wewe umeamua kuishi kama hayawani wa mwituni ambaye akiamka tu anawaza damu na nyama mbichi. Uue maelfu ya watanzania kisa tamaa ya mali na fedha halafu usingizie Foreign Influence kweli. HAIWEZEKANI
​
 
Kabisa na kuna mifano zaidi ya elfu moja hao anasema watatusaidia wana agenda zao kwa maslahi yao

Hawa Wahuni tuna wamudu wenyewe sio kumtegemea Mungu wala Mzungu
Wazungu wamewasaidia ninyi watanganyika kumsomesha Nyerere.

Kumsaidia kupata uhuru wa Tanganyika......

Kumsaidia kuitawala Tanganyika baada ya uhuru.........

Mkurugenzi wenu wa IDARA YA USALAMA WA TAIFA, marehemu Augustino Mahiga amesomeshwa Canada na familia ya Rockefeller, huku Mkurugenzi wenu mwingine wa IDARA YA USALAMA WA TAIFA marehemu Hassy Kitine alisomeshwa Canada kwa msaada wa familia ya Pierre Trudeau.

Watanzania mna tabia kama za CHICHI-DODO, ndege ambaye anapenda kula viwavi-mavi (Maggots) lakini anachukia mavi. Ukipenda boga, penda na ua lake. Ukikataa kuingiliwa na wazungu, basi anza kabisa kwa kukataa kupewa misaada ambayo ni asilimia zaidi ya 50% ya bajeti ya nchi yako, na ukatae na mikopo yao uwe Korea Kaskazini. Hapa tutakuelewa.

Ili vinginevyo ni ujinga tu. Yaani uue watu halafu ukikemewa usingizie Forein Influence ?
​
 
Perhaps ningekua nimepotea siku iyo Huwa nasisimka sana nikikumbuka hiyo siku..

Ilikua ivii nilitaka kama saa mbili nikapandisha sokoni nilipanda bajaji.. vituo vya kupigia kura VILIKUA na watu wachache sanaa.

Nikanunua kuku akiwa ana andaliwa nikaenda nunua mazaga yote ya home... Nikaenda sehemu nikaagiza konyagiiii nikawa naipiga nikamaliza kama saa NNE nikasikia usingizi nikabeba vitu KUPELEKA nyumbani

Nililala na kuja kuamka saa 11 jioni mitandao imezimwa.. naona tangazo kwa Tv wambura na nkunda mwisho KUTEMBEA 12jioni lahaula

Hapo nilikua na safari ya kutoka wilaya ya kigamboni naki ishi niende kunduchii kwa rafiki yangu tukapange mambo ya business mzee ile pombe ndio iliniokoa maana ninge enda kunduchii nahakika nisinge toboa au ninge force kurudi ningekutana na RISASI nikawa nime uwawa

Acha tu haya mambo
 
Mkuu labda hatujalewana wote tunasema jambo moja ila approach tofauti

You're arguing against a point I didn't make.
Sijasema Tanzania inaweza kuishi bila Foreign Influence..Sijasema tukatae foreign aid, foreign investment,trade au diplomacy.

Ninachosema ni kwamba we should not outsource our struggle for accountable government kwa wazungu,Hii vita tunaiweza. Kama kweli tunataka political change,Lazima tuwe wamoja tukisisitiza accountability(kama unavyotaka) na kua na institutions zitakazolinda haki zetu.

Kusoma kwa Nyerere Ulaya haina maana kua Tanganyika haiwezi kujiongoza yenyewe. Kusomeshwa kwa Mahiga au Kitine sio sababu ya Tanzania kutegemea serikali za nje kurekebisha matatizo yetu ya ndani,

Kwanini unafikiri muhimu kwa wao kuja kutu rescue?wasipokuja??.

Misaada ya USAID si tulifikiri haki yetu na ARvs?wako wapi sasa hivi?

Watatusaidia wakipenda ila tusichukulie kama permanent entitlement
 
Kabisa na kuna mifano zaidi ya elfu moja hao anasema watatusaidia wana agenda zao kwa maslahi yao

Hawa Wahuni tuna wamudu wenyewe sio kumtegemea Mungu wala Mzungu
nakubaliana nawewe nusu kwenye sentensi ya kwanza. Natilia mashaka sentensi ya mwisho kusema kwamba "tuna wamudu wenyewe" kundi kubwa lililopo kwenye utendaji wa ngazi au kazi yeyote ile ya umma wengi hawana habari ya kubadilisha hata kanuni ndogo ama utendaji mdogo wa kila siku, Nakwasisi wananchi wengi hata sehemu ya kwenda kulalamika ama kufatilia jambo fulani hatufahamu au hatufanyi --- safari ya kurekebisha mambo japo imefika ila bado ndefu.


hiyo ya Malignant-Unlimited-Foreign Influence ndo inayotupa wasiwasi , kwamba sisi ni kukaa na kutulia tu tuje kuokolewa na icc, UN, ulaya na amerika? hawatotaka shukrani? sisi wenyewe tunahusika wapi hasa? hata huku ngazi za chini ? mtaa unaweza muhoji mwenye kiti wa serikali mtaa?, kata inaweza mkalia koo diwani wao? mkuu wa wilaya/mkoa/taasisi? au ndo kila mtu hataki kugombana na serikali? --- kwa hali ambayo tupo kwa muda mrefu sisemi kwamba watu hawajapambana ila kiwango bado kipo chini, tukija kuokolewa tukiwa katika hali hii itahitajika tutoe shukrani tu kwa beberu
 
Ata Mimi Pia Sikuamin Ila Ndio Hivyo Yalitokea
 
Wewe unaamini kwamba nchi yetu bado haijaingiliwa na mabeberu ???​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…