PostGE2025 Hata mkiua mashahidi kama Kenyatta na Rutto walivyofanya mwaka 2014, hamuwezi kupona mwaka 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mkuu hongera lkn ❗️

Mkuu jambo moja au mawili ujatutendea Haki
1)
Umesema viongozi kina Ruto na Uhuru Kenyata hawakuwa na
nguvu ya uhongozi

Swali kwanini usingesema tu kunyoosha maneno kwamba❗️
1 William Rutto
2 uhuru Kenyata

Walikuwa ni Viongozi wa Upinzani ndiyo walibebeshwa dhima ya yale Mauaji ya watu zaidi ya 1000+ na Mahakama ya ICC 👈

2
Mwaibaki akiwa ndiyo Rais mtetezi hakushtakiwa👈

kwakuwa hakuusika kushawashi zile Fujo👈

badala yake yeye jukumu lake lilikuwa kutuliza zile Fujo kurudisha Amani kwa Wote pale Kenya 👈

Tukiwa wakweli kile kimetokea Kenya hakina tofauti yoyote na Tanzania

Manake Tanzania napo wameusika kushawishi ni Wapinzani

Jukumu la Rais lilikuwa kurudisha Amani

Ndiomana ICC kisheria hawawezi kumshtaki Rais wa Jamhuri kwa kadhia iyo ya Mo29

Niliwai sema uko nyuma Rais Dk Samia Suluhu Hassan Yumkin yeye kosa lake kwasasa ni kuwalinda Wachochezi👈

lkn kama ICC wangeweza kuja Tanzania kwa%90
Wangechunguza zaidi kabla ya tukio Wachochezi kinanani ❗️👈

Wakukamatwa ni Wachochezi

sio Wazuiyaji wa zile Fujo

Taratibu za ICC
Kisheria Jamhuri hawakupanga zile Fujo kabisa
hawakuchochea✅️

Wametimiza jukumu la Kurejesha Amani kwa Binadamu wote na viumbe wote ndani ya Jamhuri ✍️
 

Kumbe mnajua. Wamefanya Fujo Uvamizi Uchomaji wengine lkn Ajabu

Wapumbavu wanataka Eti Wazuiyaji wa matendo yale ndio wao Wakamatwe

Sasa ikiwa ivyo na Sheria zinaendeshwa ivyo ‼️

Ipo siku tutaamka Asubuhi hatuna Airport hatuna Bandari hatuna Umeme

Vyote vimechomwa na Wachochezi wafanyafujo

Mbaya zaidi iyo miundombinu Pesa zake za i Mikopo kutoka uko uko IMF Nk
Sasa tutalipaje ikiwa mnatetea Wachomaji miundombinu

Ndiomana ICC
Wako zaidi kutafuta Wachochezi
Na Makundi ya kichochezi👈

Sio Wazuiyaji wa Fujo✍️
 
Mimi nimewahi kukaa na wasomali kadhaa na kuwauliza inakuaje wanaweza kukopeshana pesa bila maandishi au mali yoyote bila maandishi?

Walinijibu sababu moja kuu ni kujua chimbuko la mtu hadi kule chini mfano wewe ukisema ni Warsame basi unajulikana ni wa ukoo upi utapewa pesa ukoo wako ndio utakua dhamana hivyo usiporudisha umeleta madhara kwa ukoo mzima hivyo hiyo ilijenga uaminifu.

Sasa narudi katika upepo huu wa October 29 , kiukweli matukio mengi Tanzania yalitokea na baada ya muda yakasahaulika ila hizi damu za October 29 naona bado na haziwezi kusahaulika mpaka uwajibikaji uwepo na usipokuwepo vitaanza visasi hadi chini huko ngazi ya ukoo sasa msije kushangaa kuona familia fulani miaka 2 hadi 3 mbele wanaanza kuzika ndugu mfululizo na baadae hata kukimbia nchi , hili suala la October 29 halitawahi kumalizwa kwa propaganda, uchawa , rushwa wala tume uchwara za kulinda muuaaji na aliyetoa amri, muda utasema.

Huwezi kuua ndugu zetu na sisi tukakuangalia tu , maana kama wewe hugusuiki basi una ndugu,kama mama, baba, mjomba ,shangazi, binamu na kadhalika basi maumivu utayapata kuanzia huko.

October 29 haijaisha hadi iishe.
 
Kudai mambo ya Sheria za Uchaguzi na kuchoma Miundombinu vinausikaje tena mpaka ya watu Binafsi

Sitaki siku moja kuamka kuambiwa hatuna Airport hatuna Bandari hatuna Chochote

Jielekezeni Mahakamani kudai mambo ya Uchaguzi nk

sio kwenye Miundombinu ya Watanzania wote hapana❌️

Risasi ndio dawa ya kiburi ✍️
 
Hivi hiyo ICC ambayo mnasema inatetea haki za Binadamu ni hii hii ambayo Trump anashinikiza mataifa yajiondoe na kuachana nayo maana imejaa ubabaishaji tu na kuibagaza kuwa sheria na mahakama za Marekani zina nguvu zaidi yake?

Kama ICC ingekuwa ina nguvu kweli si ingeshughulika na mauaji ya kule Afghanistan na kuwachukulia hatua Taifa la Israel kwa mauaji ya vichanga na wanawake kule Palestine.
 
Reactions: Nus
Muda sasa umeshafika ule ufalme umeanza kufitinika na haupo mbali kuanguka
 
Huu ndio UKWELI.
 
Zipo options kadhaa sisi wenye madaraka tutakavyofanya;

Mosi: Kuwakabidhi mabeberu rasilimali zetu zote wanazotaka iwe migodi, vitalu vya mafuta n.k

Pili: Kumwongezea muda aliyepo, atawale hadi mauti yatakapomkuta

Tatu: Nusu Mkate, kuwepo na Serikali ya mseto, bahati mbaya mhusika wa kusaidia hili bado anashindana na wenye Mamlaka akiwa Selo
 
Mkuu, nami nikuulize suali moja.

Vyombo vya ulinzi na usalama Tanzania vina uwezo wa kuzuia ghasia bila kumwaga damu (kuua watu hovyo) au havina?

Na kama havina ni kwanini vilitenda uovu ule na viachwe tu bila hata mtu mmoja kuwajibishwa?

Hata kama viliambiwa vijiandae kwa ajili ya October 29th lakini pia hiyo haikumaanisha kwamba vijiandae kwa mitutu ya bunduki kuua watu waso na hatia hadi akina mama waja wazito.

Suala ni kwamba hakuna aliewajibishwa na familia za walouawa hazijazika hadi leo.

Hivi haya mambo yakuingia kichwani mkuu?
 
The west is not easy to bribe. Wanamulikwa sana na taasisi zao. Pia wapo very strategic linapokuja suala zima la mustakabali wa maslahi yao muhimu ya taifa. Hawachukui rushwa yeyote tu. Halafu tuna nini sasa cha kuwahonga? Twiga? Hatuna confirmed rare earth minerals, hatuna readily available fossil fuels za kuwahonga.
 
Mkuu hapo kwenye uhuru wa tanganyika na mataifa na washirika wa magharibi tafadhali fafanua kidogo
 
Huyo ni mzanzibar alafu pia ni mwarabu huoni hata kiswahili tu ni shida kwake, ata umueleweshe vipi hawezi kukuelewa kwa sababu ana sababu zake binafsi za kusupport mauaji, usimuone mjinga ana yake huyo
 
Sio tu October 29 hata leo hii mkikata watu vidole muibe mali za watu na kuchoma masheli achilia mbali kuvamia vituo vya polisi na kuachia majambazi mtauliwa kama kuku tena safari hii tunaua sisi wananchi mnaotubia kisha serikali ije ibebe mizoga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…