Hata Mungu hawezi vumilia huu uhalifu wa kutaka kuivuruga amani ya nchi

Hata Mungu hawezi vumilia huu uhalifu wa kutaka kuivuruga amani ya nchi

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Nimeona watu wengi wakitamka kuwa Mungu atalipa kwa yaliyotokea baada ya uhalifu uliofanyika. Mimi kama mkristo ninayeijua biblia vizuri niwakumbushe tu kuwa waliofanya uhalifu kuanzia siku ya uchaguzi ni kuwa Mungu pia hafurahishwi na huo upuuzi. Mungu hutoa adhabu kali sana kwa watu kama hao.

Mungu huyu tunayemuamini wakristo kwa sasa anachochea moto vizuri kwa waliofanya uhalifu. Wasipotubu iko wazi kuwa watachomwa moto. Hakuna namna. Cha kushangaza pia Mungu huyuhuyu atasamehe wote wanaotuhumiwa kupiga watu risasi endapo watatubu. Wale askari mnaosema ni wauaji msishangae wakaingia mbinguni na kuishi na malaika.

Mungu wetu huwa hachekei ujinga. Mr Onani aliuwawa na Mungu kwa kosa la kumwagia nje alipofanya mapenzi na mke wa marehemu kaka yake. Anania na Safira waliuwawa hapohapo kwa kosa la kutotoa sadaka kamili. Watu wa Yeriko waliuwawa wote bila kosa ili kuwapisha wateule wana wa Israel. Hata Misri wazaliwa wa kwanza wote waliuwawa bila kufanya kosa ili kumfanya farao awaruhusu waisrael kuondoka. Huko Jangwani iliwekwa sanamu ya shaba na watu wakaamriwa kuiabudu na usipofanya hivyo nyoka waliotumwa na Mungu wanakuua kwa kugonga.

Mimi ninadhani badala ya kulialia hovyo na kumtaja Mungu ni bora kufuata sheria na kutumia njia sahihi ya sanduku la kura kuiondoa CCM madarakani. Hata kama mnaandamana iwe maandamano ya amani. Katika makosa ambayo Mungu yanamkera ni kutaka kuipindua serikali. Tunaambiwa huko shetani na wafuasi wake walitimuliwa mbinguni kwa kutaka kumpindua Mungu.

Badala ya kupost mistari ya biblia nendeni muwawekee mawakili nguli vijana wenye kesi ya uhaini mahakamani.
 
Afande Sele angeachana na ulevi holela pengine angekua hata Katibu Mkuu kiongozi wa Chama fulani.
 
Dah!
Kabisa na ume-connect VPN kabisa ili kuandika huu utumbo!
 
Back
Top Bottom