Hata Simba wakizidi Mbugani hupunguzwa, Wamaasai wa Ngorongoro wapunguzwe na iundwe sheria

Hata Simba wakizidi Mbugani hupunguzwa, Wamaasai wa Ngorongoro wapunguzwe na iundwe sheria

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Mimi sina mengi ya kuzungumza.

Nilikuwa naishauri serikali, iweke utaratibu muhimu na wakudumu. Iunde sheria ya idadi ya watu wanaotakiwa kuishi hifadhi ya Ngorongoro kulingana na Ecosystem ya pale. Kisha idadi inayozidi wawe wanahamishwa.

Maasai ni Watanzania wenzatu hivyo lazima tujali haki zao, lakini piah hata hifadhi na wanyama ni moja ya Rasilimali zetu muhimu Kwa uchumi na Masuala ya kimazingara. Ni lazima tutende Kwa hekima. Tusiwafukuze, isipokuwa tuongee nao kisha wahamishwe kwenye Maeneo mengine.

Hata Simba au Fisi mbugani wakizidi kuwa wengi Kwa kuzaliana kuna namna ya kuwapunguza aidha Kwa kuwaua, kuwauza, au kuwahamisha mbuga zingine, sasa wamaasai sio wanyama ni watu Kama sisi, hatuwezi kuwaua wala hatuwezi kuwauza, isipokuwa tunaweza kuwahamisha kama sehemu ya ku-balance Ecosystem ya pale Ngorongoro.

Hayo mengine ya Siasa sidhani kama yanaumuhimu wowote.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
 
Tatizo la Ngorongoro ni overpopulation
 
Kumbuka Ngorongoro si national park bali ni conservational area na kinachotunzwa pale si wanyama tu bali hata watu wenye asili ya lile eneo. Kuwahamisha haitakuwa haki hata kidogo ukiachilia mbali wamasai wana asili ya kuhama hama kutoka eneo moja kwenda jingine kwaajili ya malisho na maji ya mifugo yao. Kwahiyo naamini Ngorongoro's nature will balance by itself accordingly
 
Serikali ipunguze kujenga mahoteli makubwa ndani ya hifadhi. Hayo mahoteli yanachukua maeneo makubwa na matatizo kumwangushia mmasai.
 
Kumbuka Ngorongoro si national park bali ni conservational area na kinachotunzwa pale si wanyama tu bali hata watu wenye asili ya lile eneo. Kuwahamisha haitakuwa haki hata kidogo ukiachilia mbali wamasai wana asiri ya kuhama hama kutoka eneo moja kwenda jingine kwaajili ya malisho na maji ya mifugo yao. Kwahiyo naamini Ngorongoro's nature will balance by itself accordingly

Ndio maana hata hao wanyama wakizidi mpaka kuhatarisha Ecosystem wanapunguzwa, sioni ajabu wamasai Kama sehemu ya Ecosystem wanapozidi na kuhatarisha usalama wa eneo Hilo wakipunguzwa kupelekwa sehemu nyingine.
 
Hiv una Elimu ya Uhifadhi Kweli?

Yani watu tunafikiria Simba awekwe kwenye Endangered Species sababu wanapungua kwa kasi sana Tanzania na Duniani. Wewe unasema hata Simba na fisi wanauawa wakizidi.

Hakuna kitu kama hicho kwenye Eco System, Simba atakufa natural death au atauawa na myama mwenzake na sio binadamu ili wapunguzwe. Sasa hivi nchi kama USA ina discourge sana kuweka Simba kwenye Trophy Hunting katika vitalu vya uwindaji sababu wanapungua kwa kasi hadi imekua ngumu kuwaona hata ukienda mbugani.

Nani alikwambia kama Ngorongoro kuna Simba wengi? Kaa ukijua population ya Simba inapotea Ngorongoro ndo maana wahifadhi wanachanganyikiwa sababu ndo mnyama pekee anayeongoza kwa kuleta watalii pamoja na chui.

Tanzania ilikua na Simba zaidi ya elfu 14 na sahizi tunaongelea Simba elfu 3 halafu unasema wameongezeka. Sio kila mada lazima uiandikie uzi hata kama haupo well informed

Hilo la Evacuation ya Wamasai nitakubaliana na wewe kwamba lazima kuwe na Mutual Agreement between the Government ya namna ya ku control population ya Mifugo ambayo ndo kikwazo kikubwa.
 
Ndio maana hata hao wanyama wakizidi mpaka kuhatarisha Ecosystem wanapunguzwa, sioni ajabu wamasai Kama sehemu ya Ecosystem wanapozidi na kuhatarisha usalama wa eneo Hilo wakipunguzwa kupelekwa sehemu nyingine.

Acha upopoma wewe jamaa, wapi wanafanya hivyo? Tofautisha kati ya National Park, Game Reserve na Protected Areas. Halafu ujue ni wapi wanafanya Trophie Hunting na wanyama wanotumika kama bait ni Nyati, Nyumbu na Swala
 
Kumbuka Ngorongoro si national park bali ni conservational area na kinachotunzwa pale si wanyama tu bali hata watu wenye asili ya lile eneo. Kuwahamisha haitakuwa haki hata kidogo ukiachilia mbali wamasai wana asili ya kuhama hama kutoka eneo moja kwenda jingine kwaajili ya malisho na maji ya mifugo yao. Kwahiyo naamini Ngorongoro's nature will balance by itself accordingly
Nakubaliana na wewe kwenye jamii ya kimasai lakini Binadamu ndo mharibifu mkubwa wa Nature, Lazima population ya watu na wanyama iwe controlled na watu wafikie makubaliano ya pamoja otherwise Ngorongoro haita exist Tena
 
Back
Top Bottom