Hiv una Elimu ya Uhifadhi Kweli?
Yani watu tunafikiria Simba awekwe kwenye Endangered Species sababu wanapungua kwa kasi sana
Ukisoma uwe unaelewa mantiki ya kilichoandikwa.
Naona unamaarifa mengi lakini unashindwa kuelewa logic ya vitu vidogo Kama nilichoandika.
Simba, fisi au mnyama yoyote ambaye ningemtumia angekuwa mfano endapo ataonekana kuzidi mbugani au hifadhini hadi ikaonekana anaathiri Ecosystem ya eneo hilo hupunguzwa.
Binadamu ni sehemu ya ecosystem, na Kwa muktadha wa ngorongoro inaonekana ongezeko Lao na shughuli zao zinaathiri viumbe wengine.
Kila kiumbe ni endangered species kutokana na matumizi yake yakizidi Kwa viumbe wengine.
Moja ya sababu ya kiumbe kuwa endangered species ni pamoja na;
1. Mabadiliko ya tabia ya nchi
2. Ongezeko la watu linalosababisha shughuli na matumizi ya viumbe Fulani kuwa kubwa
3. Ongezeko la baadhi ya wanyama hasa wala nyama.
Overpopulation inapelekea uhaba wa malighafi.
Iwe overpopulation ya mnyama, binadamu au mimea.
Umezungumzia kuhusu natural death, sijui kama unajua maana yake,
Hiyo natural death Kwa nini haimkumbi mwanadamu mpaka azidi na kuiathiri hifadhi au mbuga?
Lazima ujue kuwa kuna viumbe ambao wanatumiwa na viumbe wengine wengi na wapo ambao hawatumiwi Sana. Na zipo sababu za Jambo Hilo; Kwa mfano, baadhi ya viumbe ni sumu Kama vikiliwa na viumbe wengine, na pili baadhi ya viumbe vinaakili na utashi mfano binadamu hivyo hujihami na kuepuka kuuliwa au kuliwa na viumbe wengine.