Source AI!?
AI hii inayokwambia Kenya Ina bullet trains!?
Uwe na siku njema.
Marekani sio miji tu ipo vizuri kushinda China kwenye aspect nyingi sana
Angalia miji ya China ilivyo, yote ina style ileile, ina maghorofa mengi marefu yaliyokusanyika sehemu moja, hali ya hewa ya baridi na zaidi ya 95% ya wakaz in ni Wachina
Kwa USA angalia New York City ina mwonekano wa kivyake, angalia Miami ni sehemu yenye joto, starehe za kila aina, beach nzuri nk
Los Angeles ni hub of entertainment in the world kuna kila kitu na studio kubwa za filamu duniani zinapatikana hapa. Ni mji wa kitofauti sana na New York au Miami
Angalia Washington DC mji mzuri ambao maghorofa yake ni mafupi, barabara pana na yana rangi nyeupe. Vibe la DC ni tofauti kabisa na NYC, Miami au LA
Angalia Las Vegas, jiji zuri lililojengwa jangwani na ni moja ya maeneo yenye starehe sana duniani
Angalia mji wa Leavenworth, huu mji ukiuangalia unafanana sana na miji ya Ulaya kwa architecture kumbe ni Marekani hapohapo
Kuna miji kama San Francisco ambayo Wachina wanapapenda, Marekani ni diverse sana na kila kona iko tofauti na sehemu nyingine
Ila China miji yao niliyoifuatilia mingi inatoa vibe lilelile Beijing, Shanghai, Shenzhen, Guangzhou nk ni miji mikubwa sana yenye infrastructure za kutosha kuliko miji mingi ya Marekani lakini inafanana tu style yake ya ujenzi, watu nk
Hong Kong kidogo imechanganya species nyingi sana za watu, huku kunafaa hata mtu mweusi ukienda hawakushangai kama Mainland China
Ila mainland China jiji ninalolipenda ni Chongqing. Hili ndio jiji ambalo linanishangaza kuliko majiji yote ya China. Nimependa jinsi walivyolijenga mtu uko ghorofa fulani floor ya 26 ukiangalia chini upande wa kulia wa jengo unaona ni mbali sana halafu ukija upande wa kushoto wa jengo unaona nje kuna mtaa uko level sawa na floor ya 26 uliyokuwepo. Huu ndio mji kidogo naona uko tofauti na hiyo mingine