Binafsi nilijua tutamkumbuka lakini siyo kwa haraka na mapema namna hii.
Nchi yetu sasa ni hatari zaidi kuwataja watekaji kuliko kuwa mtekaji, kuliko ujitokeze uwakemee wauaji utakamatwa na dola!!
Nchi yetu sasa ni hatari zaidi kuuchambua ufisadi ulioibuliwa na CAG kuliko kufanya ufisadi, yani sasa hivi ndani ya nchi yetu utalindwa na dola kwa kuambiwa kula kwa urefu wa kamba yako, lakini ukipinga ufisadi na kuwataja waliofanya ufisadi utaambiwa humpendi mama na serikali yake.
Ndani ya nchi yetu sasa hivi mafisadi, majizi na wazembe kazini wako salama kwani wanalindwa zaidi kuliko awamu nyingine yoyote ile!
Baada ya Freeman Mbowe kukutwa na kesi ya kujibu kuhusu ugaidi na kupanga njama za kuuwa viongozi wa serikali na kukaa jela kwa miezi 8, sasa Tundu Lisu nae yuko jela kwa kesi ya uhaini.
Nape na January Makamba wamebwagwa huko si mawaziri tena.
Paul Makonda ni mkuu wa mkoa tena.
Flyover mpya hakuna na uhamasishaji ujenzi wa viwanda Umedorora.
Bwawa la umeme limekamilika ujenzi wake lakini bei ya umeme iko juu vilevile.
Job Ndugai alifukuzwa uspika wa bunge baada ya kutoa ushauri wake kuhusu nchi kukopa hovyo.
Askofu Gwajima amefutiwa kanisa lake la Ufufuo na uzima kwa kosa la kuwakemea hadharani watekaji.
Ukiondoa watekaji, wauaji, mafisadi na wazembe kazini, hakuna mwingine mwenye furaha ndani ya nchi yetu.